Katikati ya harakati za 50/50 kinyume chake wanawake wengi siku hizi hawana furaha

Katikati ya harakati za 50/50 kinyume chake wanawake wengi siku hizi hawana furaha

Hapa nakuunga mkono kwa asilimia zote. Mwanamke akitaka aishi kama malkia basi anitii na kuniheshimu. Lazima niwe mtumwa kwake. Huu ukweli umesemwa tangu na tangu.
Nilipoigundua hii siri maisha yamekua mepesi.
 
Hii bibie sio hoja ya msingi, sababu tupo tuna vipato vya chini ya hao ulio wataja ila wake zetu wanaishi maisha mazuri na wanapendeza kuzidi nyinyi mnao fanya kazi. Hapo cha msingi ni upate mwanaume wa kweli na wewe mwanamke ujitambue na uishi katika uhalisia sio uishi maisha ya wenzako kwamba mama fulani kavaa hiki na wewe uvae au mfano wake.
Kuna point umeitaja nzuri kwamba upate mwanaume mwenye kujali.

Mashindano ni hulka ya mtu na sio nzuri. Ila kama mwanamke alizoea anajitunza inampa shida sana kuacha na kujikita iwenye kuwa mama wa nyumbani per se anafubaa na mwishoe mwanaume anaenda kutafuta michepuko huku akilalamika mwanamke wake amezeeka
 
Nani aliwadanganya kuwa kupinga 50/50 ni lazima mwanamke abaki nyumbani? Personally huo ujinga wa 50/50 siutaki kwangu hata sukari ikiisha sinunui bila mahesabu. Nilishamtengenezea Mr kwamba mimi ni support yako. Pale unapotoa mimi ndo ntaongeza kama kuna ulazima. Gharama zangu za maisha ni kubwa, hujanioa ili u shrink my standards otherwise ungeenda kuoa kijijini kwenu sitimbi huko. Na kazi nafanya na wanangu nalea. Hivi mfano kazini umefukuzwa ghafla na akiba huna tunaishije nyumbani? Mwanaume huna uwezo wa kunitunza huna unakomalia nikae nyumbani nivae madera. Are you serious? Kazi nafanya kama kawa na familia yako utaihudumia maana wewe ndo baba.

Hapa inaonekana unaleta tafsiri yako mwenyewe ya 50/50, hii package nzima nzima bibie kuanzia akili mpaka mitazamo, sababu katika hiyo 50/50 mwanamke kajazwa ujinga ya kuwa mwanaume ndio adui yako namba moja na ni mshindani wako pia, kitu ambacho si sahihi.

Asili ya mwanamke ni kubaki nyumbani hii ni tangu na tangu, mwanamke kutoka ni kumtafutia matatizo kama anayokumbana nao leo, shida yenu sio wakweli katika maneno wala vitendo.

Usidanganye watu bibie huwezi kufanya kazi na ukafanikiwa katika malezi, hili halipo bibie. Hizi kazi zenu za maofisini sio kweli.

Malezi ni mjumuiko wa vitu vingi, ni kutoa elimu, kuhudumia, kudumu muda mwingi na mwanao na kurekebisha, watoto wenu mnao waachia dada wa kazi useme unalea ? Au unafikiri kulea nikumchambisha tu mtoto, au kumlisha au ?
 
Mashindano ni hulka ya mtu na sio nzuri. Ila kama mwanamke alizoea anajitunza inampa shida sana kuacha na kujikita iwenye kuwa mama wa nyumbani per se anafubaa na mwishoe mwanaume anaenda kutafuta michepuko huku akilalamika mwanamke wake amezeeka

Hapa tatizo ni la mwanaume kukosa uanaume. Mwanaume halisi lazima awe na huruma kwa wale anao wasimamia akiwemo mke wake.

Shida yako unamuelezea mwanaume aliyekosea katika matunzo ya mke wake kama marejeo ya ujumla hii sio sahihi. Kwa minajili hii unakosa hoja, sababu hoja yako umeijengea katika udhaifu na si ukamilifu.
 
Hapa inaonekana unaleta tafsiri yako mwenyewe ya 50/50, hii package nzima nzima bibie kuanzia akili mpaka mitazamo, sababu katika hiyo 50/50 mwanamke kajazwa ujinga ya kuwa mwanaume ndio adui yako namba moja na ni mshindani wako pia, kitu ambacho si sahihi.

Asili ya mwanamke ni kubaki nyumbani hii ni tangu na tangu, mwanamke kutoka ni kumtafutia matatizo kama anayokumbana nao leo, shida yenu sio wakweli katika maneno wala vitendo.

Usidanganye watu bibie huwezi kufanya kazi na ukafanikiwa katika malezi, hili halipo bibie. Hizi kazi zenu za maofisini sio kweli.

Malezi ni mjumuiko wa vitu vingi, ni kutoa elimu, kuhudumia, kudumu muda mwingi na mwanao na kurekebisha, watoto wenu mnao waachia dada wa kazi useme unalea ? Au unafikiri kulea nikumchambisha tu mtoto, au kumlisha au ?
Nikuibie tu siri, nilishakaa nyumbani kulea watoto wangu kwa miaka mitatu mfululizo. Nilifunga biashara zote na kazi nikaacha.

Sasa nakuuliza swali. Mwanamke anatakiwa akae nyumbani what if mumewe kafa?

Alafu hiyo 50/50 mnayoiongelea mbona mi siielewi? Hivi kuna mwanamke anapenda kutumia ela yake sawa na mwanaume? Mi mwanaume atambe anavyoweza ila anizidi ela na zangu asiniombe ntaumwa. Sasa sielewi 50/50 mnayoisema ni ipi? Kwahiyo watoto wakienda shule mama anabaki anasugua ukuta wa nyumba au inakuwaje em nielewesheni nielewe nilale sasa maana Mr kasafiri kikazi nipo hapa nabishana na mabachela sijui
 
Viongozi 50/50 sio shida zao, wamechagua wanapopamudu na familia zimeendelea kuevolve bila shida

Hakuna mwanaume kiongozi anaye kubali 50/50. Itakuwa huijui silika ya uanaume na hujui mtawala ni nani. Mwanaume kiongozi lazima arudi katika asili sababu huko ndiko mambo hurejeshwa.

Mwanaume kiongozi ambaye ni mtawala lazima atamuongoza mkewe katika kumuonyesha udhaifu wa 50/50 na madhara yake.

Kingine kuna tofauti ndogo sana katika matamko haya mawili yaani mtawala na kiongozi, mtawala lazima awe ni kiongozi, tofauti ni ule uongozi ameupata vipi. Kwahiyo si sawa kusema kuna mtawala na kiongozi. Kwa ufupi mtawala huchukua nafasi ya mtangulizi wake na hakuna kinyume chake.
 
Hapa tatizo ni la mwanaume kukosa uanaume. Mwanaume halisi lazima awe na huruma kwa wale anao wasimamia akiwemo mke wake.

Shida yako unamuelezea mwanaume aliyekosea katika matunzo ya mke wake kama marejeo ya ujumla hii sio sahihi. Kwa minajili hii unakosa hoja, sababu hoja yako umeijengea katika udhaifu na si ukamilifu.
Nikuulize kitu kaka. Mfano mkeo ana sherehe ya ndugu na anatakiwa achangie kama alivyochangiwa kwenye sherehe yenu. mwanamke hana kazi anakuomba ela ya mchango na gauni labda na kiatu. Huwa mnatoa bila masimango!? Huwa mnazo za kutoa kwenye hizi shughuli?

Haya umemkuta mkeo ana wadogo zake alikua anawasomesha. Hadi unamuoa hukumwambia kwamba hutaki asomeshe ndugu zake. Ameingia kwenye ndoa u amwambia aache kazi na hapo hamjaanza kuzaa bado yani kuna vitu nashindwa kuvielewa hadi kichwa kinauma. Anyways men will always be men
 
One thing men should know. YOU ARE NOT DOING A FAVOR MARRYING WOMEN! Ni kwasababu tunategemeana.

Huwa mnalichukulia hili suala la ndoa kama msaada hivi! Utaskia si ashukuru flani kamstiri!

Wanawake wangapi wanastiri mashoga na watu wasio na uwezo wa kupandisha jongoo kwenye mtungi, ila mwanamke anahangaika sijui na dawa za kimasai ili we punda uitwe baba. Saizi mnanguruma huku.

Kama mna uwezo sana si mzalishane wenyewe wanaume kwa wanaume. Mpite labor mkaone shughuli yake. Mnachukulia wanawake ni kama voodoo dolls ya kutoboa toboa tu. A whole head passed through my vagina, I created a brain and oh a title for you ungrateful set of lunatics to be called fathers eti leo mnajifanya mnakashfu wanawake.

I call out gays in every men who talk down on women. Kaeni na wake zenu ndo muwaachishe kazi. Kwani lazima kila mtu awe kama mama ako au mkeo! Hao hao vilaza waliokubali wametosha! Wa wenzenu wako makazini na miradi wanafungua.
Shkamoo.
 
Nikuibie tu siri, nilishakaa nyumbani kulea watoto wangu kwa miaka mitatu mfululizo. Nilifunga biashara zote na kazi nikaacha.

Sasa nakuuliza swali. Mwanamke anatakiwa akae nyumbani what if mumewe kafa?

Maswali kama haya huwa si ya msingi mpaka pale yatokee. Shida ya kutengeneza tatizo ili upate jibu ambalo si sahihi. Vipi je ukifa wewe ndio maisha yasiendelee ? Bibie mumeo anaweza akafa na ukaishi maisha mazuri kuliko hata kipindi mumeo yuko hai. Shida kuna vitu watu wanakosa.
 
Ndo nakuuliza mkuu, mwanaume kafa ghafla, mke alishamuachisha kazi. Nini kinafuata? Kwani scenario kama hizo ni ngeni maskioni kwako? Kwamba hujawahi kuskia mwanaume amekufa au?

Anaishi maisha mazuri yeoi wakati hakua na kipato! Na ndo ukute mwanaume ana ndugu kama utitiri wanafuata mali ya kaka utadata🤣
 
Nikuulize kitu kaka. Mfano mkeo ana sherehe ya ndugu na anatakiwa achangie kama alivyochangiwa kwenye sherehe yenu. mwanamke hana kazi anakuomba ela ya mchango na gauni labda na kiatu. Huwa mnatoa bila masimango!? Huwa mnazo za kutoa kwenye hizi shughuli?

Haya umemkuta mkeo ana wadogo zake alikua anawasomesha. Hadi unamuoa hukumwambia kwamba hutaki asomeshe ndugu zake. Ameingia kwenye ndoa u amwambia aache kazi na hapo hamjaanza kuzaa bado yani kuna vitu nashindwa kuvielewa hadi kichwa kinauma. Anyways men will always be men

Ndio maana nikasema hivi hoja zako zinakosa nguvu sababu umezijenga katika udhaifu wa mtu mmoja mmoja na si ukamilifu. Ukienda kwa mtindo huu lazima ukosee.

Narudi katika hoja yako kwangu hili nalifanya hasa kwa ajili ya kumpa furaha mke wangu japo si lazima kwamba ukichangiwa na wewe uchangie, watu wanatakiwa wajue na waishi katika kanuni ya kufanyiana wema tu.

Aya ya pili nayo nayo inaingia katika udhaifu ule ule. Hili jambo ni la makubaliano kwetu sisi waislamu mnaruhusiwa kuingia mkataba wa baadhi ya mambo hasa ya kihuduma na mkikubaliana basi yaliyomo kwenye mkataba kama hayaendi kinyume na maagizo ya Mungu yanafanyika, kama hilo la kuwasomesha wadogo zako. Yaani namaanisha ya kuwa mnawekeana terms na lazima zitekelezwe. Haya yanafanyika awali kabisa.
 
Ndo nakuuliza mkuu, mwanaume kafa ghafla, mke alishamuachisha kazi. Nini kinafuata? Kwani scenario kama hizo ni ngeni maskioni kwako? Kwamba hujawahi kuskia mwanaume amekufa au?

Anaishi maisha mazuri yeoi wakati hakua na kipato! Na ndo ukute mwanaume ana ndugu kama utitiri wanafuata mali ya kaka utadata🤣

Swali lako mbona nimelijibu kwa ufasaha sana. Bibie hatuishi kwa kubahatisha japo hayo hutokea lazima tuishi katika uhalisia. Maisha lazima yaende wangapi wamefiwa ghafla na waume zao na wakaishi maisha mazuri kuliko kipindi ambacho waume zao walikuwa hai ? Hujaliona hili ?

Watakuja kumsaidia wale wenye vipato na maisha yataenda au unahisi unaishi kwa kujitegemea mwenyewe pasi na kutegemeana ? Sababu hata mume wake alipokuwa hai alikuwa hapati kipato pasi na sababu au na kutegemeana.

Jipe muda utafakari haya ninayo kwambia.
 
Ndio maana nikasema hivi hoja zako zinakosa nguvu sababu umezijenga katika udhaifu wa mtu mmoja mmoja na si ukamilifu. Ukienda kwa mtindo huu lazima ukosee.

Narudi katika hoja yako kwangu hili nalifanya hasa kwa ajili ya kumpa furaha mke wangu japo si lazima kwamba ukichangiwa na wewe uchangie, watu wanatakiwa wajue na waishi katika kanuni ya kufanyiana wema tu.

Aya ya pili nayo nayo inaingia katika udhaifu ule ule. Hili jambo ni la makubaliano kwetu sisi waislamu mnaruhusiwa kuingia mkataba wa baadhi ya mambo hasa ya kihuduma na mkikubaliana basi yaliyomo kwenye mkataba kama hayaendi kinyume na maagizo ya Mungu yanafanyika, kama hilo la kuwasomesha wadogo zako. Yaani namaanisha ya kuwa mnawekeana terms na lazima zitekelezwe. Haya yanafanyika awali kabisa.
Kaka unaongelea maswala ya makubaliano wakati wanaume wenzako huko juu wanaongelea amri.

Kaka mimi nazijua kuta za mahakama, wajane wanavyoteseka huwezi kuelewa ndo maana nakuoa scenario hizo. Sasa kama kusingekua na precedents mimi ningekua nabishana hapa? Najua nnachokipigania. Hao wanaume wanaishi kwa nadharia. Wengi wanakua hawajajipanga kama unavyosema.

Kama huo mfumo unaosema ungekua umenyooka mbona mambo yangekua sawa tu nani angelalamika? Tatizo linakuja watu hawajajipanga na bado wanaishi kwa mkumbo. Kama wewe umejiweka sawa sijui kidini sijui kimila it’s okay, kuna hawa wanaoishi kiholela. Naongea kwasababu hizi issue nimekutana nazo
 
Swali lako mbona nimelijibu kwa ufasaha sana. Bibie hatuishi kwa kubahatisha japo hayo hutokea lazima tuishi katika uhalisia. Maisha lazima yaende wangapi wamefiwa ghafla na waume zao na wakaishi maisha mazuri kuliko kipindi ambacho waume zao walikuwa hai ? Hujaliona hili ?

Watakuja kumsaidia wale wenye vipato na maisha yataenda au unahisi unaishi kwa kujitegemea mwenyewe pasi na kutegemeana ?

Jipe muda utafakari haya ninayo kwambia.
Hii dunia unasema watu watakusaidia baada ya mume kufa?? 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Usiku mwema mkuu
 
Kaka unaongelea maswala ya makubaliano wakati wanaume wenzako huko juu wanaongelea amri.

Bibie narudia tena usijenge hoja kwenye makosa ya watu jenga hoja katika kupatia ili uwe upande salama na hoja iwe na maana. Naandika haya mara ya tatu sasa au zaidi.

Wanaume wanakosa uanaume nielewe ninachokwambia.

Sasa rekebisha kwanza kiti chako kisha ukipambe.
 
Hii dunia unasema watu watakusaidia baada ya mume kufa?? 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Usiku mwema mkuu
Ina maana hata huyo mume alipokuwa hai alikuwa hasaidiwi au unaelewa ya kuwa kusaidiwa ni kuomba omba ?

Na wewe pia bibie.

Ukiwa na hoja ya maana utanistua.
 
Bibie narudia tena usijenge hoja kwenye makosa ya watu jenga hoja katika kupatia ili uwe upande salama na hoja iwe na maana. Naandika haya mara ya tatu sasa au zaidi.

Wanaume wanakosa uanaume nielewe ninachokwambia.

Sasa rekebisha kwanza kiti chako kisha ukipambe.
Nadhani tunachoshindwa kuelewana ni upande tuliposimama.

Mimi nasimama kwenye positive na negative wewe umeng’ang’ana kwenye positive na unanilazimisha niamini kwamba the world is only full of butterflies na unanilazimisha nijione kwamba sina hoja. Sawa. Uko sahihi. Acha nibaki na mtazamo wangu wa kwamba hii dunia haiko fair, baki na dhana kwamba hii dunia hata usipokua na kazi utaishi tu. Yote ni sawa na unaweza kuwa sawa zaidi yangu.
 
Ina maana hata huyo mume alipokuwa hai alikuwa hasaidiwi au unaelewa ya kuwa kusaidiwa ni kuomba omba ?

Na wewe pia bibie.

Ukiwa na hoja ya maana utanistua.
Mwanaume akiwa hai anasaidiwa na nani? Umewahi kuona mwanaume gani anasaidiwa kila siku dunia hii? Akishasaidiwa analipaje huo msaada? Inamaana wanaume wote wanasaidiwa? Wale wasio saidiwa wanaishije?

Eti nikiwa na hoja nikustue. Sasa hapa ndo unanirudisha kwenye point kwamba acha wanawake wafanye kazi. Uwezo wa wanaume wengi wa kufikiri ya baadae una walakini kidogo.

Nikuage tena. Usiku mwema mkuu. Hoja yangu imeishia hapo
 
Huwa nakutana na wanawake wengi wanasema wanatafuta hela kiukweli wanawake wengi wa kitanzania wanafanya kazi zisizo rasmi ambapo vipato za hizo kazi ni kiduchu.
Utawakuta migahawani, ujenzi na kazi zingine ambapo vipato vyao ni vidogo kwa siku analipwa 3,000 mpk 5,000.
Mazingira ya kiafrika yamembana sana mwanamke kiuchumi na mwisho wa siku huishia kudanga na kuwa single mom tu na hakuna mafanikio wanayopata.
Mwanamke wa kiafrika bila kuolewa na mwanaume mwenye akili timamu na mpambanaji ataishia kuteseka tu.
Hiyo 50/50 inawadanganya sana, hayupo mwanaume yoyote duniani ambaye atakubali kuishi na mwanamke ambaye hamueshimu na hamsikilizi
Tena naongezea mkuu! Waajiri wengi wanapenda kuajiri wanawake maana ni cheap labour! Hawana majukumu ya kifamilia hata akiambiwa 120k per month anakubali anajua huko atadanga.
 
Back
Top Bottom