Sasa swali langu linakuja. Wewe income yako ni kama GSM? Mimi nimetoka kwetu napata kila kitu, nikaanza kazi nijihudumie,
Umekuja kunioa ukasema niache kazi nilee watoto , nyumbani unaniachia elfu moja ya dagaa wanangu wale, wewe unaenda kukesha bar, kwakuwa mama yako hakusoma, baba yako alikupeleka shule ya kata unataka na wanangu wasome kata kwakuwa wewe huna uwezo, nakaa nyumbani nafubaa kama mzee wa miaka 60 kisa mume wangu hataki nifanye kazi nibaki nilee watoto,
Ukirudi nyumbani unanikuta nimefubaa huvutiwi tena na mimi ulienioa miaka 7 nyuma nilipokua najinunulia lotion ya 35,000. Saizi unanipakisha minara coconut oil. Unaenda kazini kwako unakutana na secretary anapaka lotion ya 20,000 anapendeza anawaka unamtamani unakaa ukimwambia mke wangu hana mvuto tena. Wanaume mna utindio si eti?
Nani aliwadanganya kuwa kupinga 50/50 ni lazima mwanamke abaki nyumbani? Personally huo ujinga wa 50/50 siutaki kwangu hata sukari ikiisha sinunui bila mahesabu. Nilishamtengenezea Mr kwamba mimi ni support yako. Pale unapotoa mimi ndo ntaongeza kama kuna ulazima. Gharama zangu za maisha ni kubwa, hujanioa ili u shrink my standards otherwise ungeenda kuoa kijijini kwenu sitimbi huko. Na kazi nafanya na wanangu nalea. Hivi mfano kazini umefukuzwa ghafla na akiba huna tunaishije nyumbani? Mwanaume huna uwezo wa kunitunza huna unakomalia nikae nyumbani nivae madera. Are you serious? Kazi nafanya kama kawa na familia yako utaihudumia maana wewe ndo baba.
Wanaume wengi mnataka mwanamke ambae anakaa nyumbani ili umnyanyase. Au sio.
Muwe na uwezo wa kuwahudumia basi sio mke anamiaka 30 anafanana na kabibi ka miaka 65.
50/50 ni kwenye fursa kwa sababu hawa waliosoma waende wapi? Kama wanaume mngekua that smart si mngekua mnaongoza peke yenu madarasani. Ndo maana kuna vilaza na kuna wanawake wanaongoza. Acheni ubinafsi.
Most of us submissive women tuko makazini na ndoa zetu wanaume tunawaheshimu vizuri tu.
Tena wanawake acheni leo niwape siri, ukitaka kumcontrol mwanaume kuwa submissive. Yani shingo ndo inazungusha kichwa. Sitawafundisha kila kitu. Mwanaume akirudi nyumbani muoneshe heshima zote, mkiwa public mtreat kama mfalme uone kama hato fall for your desires.
Hawa wa jamii forum wengi wanachuki za bure na wanawake na kuna mahali wanashindwa kuelezea wanachotaka. Chanzo cha wanawake kutokua na heshima sio kazi walizo nazo bali ni jinsi wanaume mlivyoshindwa ku play part zenu,yani mwanaume anashinda bar, ana shinda anabet, kila akirudi hana hela, watoto wanarudishwa ada. Na mke alisoma ana kadregree akae nyumbani kisa mume atajiskia vibaya? Stupid
Its like unawaongelea wanaume wenye character sita ndani ya mtu m'moja. Yaani huyo huyo ni abuser wa wanawake, huyo huyo ni masikini anayetokea familia au ukoo wa mafukara, huyo huyo ana kazi nzuri ambayo ofisini kwao anakutana na secretary pisi kali jambo ambalo ni ngumu kukutana nae kama mwanaume anafanya kazi kampuni ya zoa maji taka, huyo huyo mwanaume ni mbabe etc.
Sasa maswali yangu kwako nitakuuliza, hivi kwa uelewa wako, mwanaume wa kawaida ana asilimia ngapi za uhakika wa kumpata binti wa kishua akamuweka ndani kama mkewe wa ndoa so umeassume huyu binti anatoka tu kwao na kuanza maisha, hakuna process za mahari, posa, kuchunguza maisha ya mwanaume before hamjaanza ishi pamoja?
So kwenye hii imaginary scenario yako umeassume kuwa waume wanachotaka ni kumharibia mkewe maisha yaani wanaume hawa hawafikirii kabisa maendeleo yaani akirudi nyumbani hawazi hata kutazama tamthiria au kukaa na mkewe wapange maisha, anachowaza ni kumharibia maisha amuone amefeli kabisa, kweli hivi ndivyo inavyofikiria? [emoji848]
Kwahiyo umetengeneza mwanaume kwenye fikra zako kama kiumbe mwenye wazimu asiyejua maisha ni nini ila mwanamke ndie ana akili ya Maisha kwamba mwanamke atalosema na kuwaza ndilo litafanya maisha yasonge mbele ila mwanaume kila atakalo amua litakuwa na mwisho wa kufeli? Unaona akili za mabinti wa kisasa ambao kidogo mlipata fursa ya kujiendeleza kielimu? [emoji848]
Kwahiyo umeassume kuwa mwanaume kutotaka mkewe asifanye kazi basi imaanishe akae ndani kama yai, wanaume wa namna hiyo huwa mnakutana wapi hebu tuambie maana hata mimi nimesoma ulichoandika huwa nakiskia tu na kukiona kwa nadra sana kwenye jamii sio jambo la kusema ni prevalent kwenye maisha na jamii yetu, wewe mwenzetu haya unayaona wapi, au unatazama sana tamthiria za jua kali unahisi ndio maisha hali ya watu yale? [emoji848]
What if mwanamke anafanya kazi ambayo ni ya kusafiri sana na boss wake na wapo pamoja muda wote, mwanaume akitaka kuokoa ndoa yake na kumtaka mkewe kuacha hiyo kazi afanye biashara zao atakuwa anakosea? Kwako mkataba wa kazi ya miaka 20 ni kipaumbele kuliko mkataba wa ndoa wa kudumu? [emoji848]
Kuna vitu vingi umeongea na hoja imenyooka kwa maana maelezo yanasomeka ila umeongea vitu kinadharia sana unaonekana maisha unayatengeza kwa scenario za kutunga kichwani badala ya kuobserve kinachotokea kwenye uhalisia.
Acha kujitisha. Unaona mfano mimi nimekusoma tu nimeshajua kuwa haujui maisha yanaendaje sababu unawazungumzia watu kwa character tofauti ambazo huwa ni ngumu mtu azibebe zote kwapamoja kwasababu Maisha humshape mtu kuwa na tabia au haiba fulani ni ngumu mtu kubeba zaidi ya haiba moja. Huwezi kuwa mchoyo halafu tena uwe mkarimu, huwezi kuwa mnyanyasaji wa wanawake halafu uwe na mapenzi ya kweli, huwezi kuwa binti kutoka familia ya single mother ukawa na tabia za kufanana na binti aliyelelewa familia ya baba na mama, huwezi kulelewa na mama mdangaji halafu uje kuwa sista wa kanisani historia yako ya malezi na background yako vitakuhukumu utafeli mission ya usista.
Nadhani unahitaji exposure ya maisha kwasababu unaumba mtu kama director wa movie ila unasahau maisha sio movie. Nimalizie kwa kusema, women view life as fairytale male view life as practical physics and mathematics assignments.