Katikati ya harakati za 50/50 kinyume chake wanawake wengi siku hizi hawana furaha

Kaza fuvu as you want. Ila sikua namjibu mleta mada nilikua namjibu mpuuzi mmoja aliesema a woman should stay home only! Nenda kwenye page ya kwanza utamuona alipo tolea mfano wa gsm. Hapo ndo tulipoachana njiani. Na ntakisimamia hiko hadi siku naingia kaburini.
 
Mie nina experience na hivi vitu kuliko udhaniavyo. Uhalisia ndio unafanya mfano wako uwe irrelevant.
Nina experience na hivyo vitu vya mahakama.
Kuna kesi na kesi za kupeleka primary court kuhusu familia/mirathi.
Zingine madawati ya jinsia serikali za mitaa wanamalizana nazo.
Ila Mahakama ya Chang'ombe ya mirathi na familia ni mahakama pekee ya utatuzi wa masuala ya mirathi.
Na pale mwanamke hupewa kipaumbele kuliko udhaniavyo wewe.
Nimehudhuria kesi nyingi moja wapo ikiwa yangu na mkewangu wa kwanza tuliotalikiana,wanawake wanapewa sana kipaumbele.
Tena ukienda TAMWA ama TAWLA no charges unalipwa hulipi hata shinkumi.
 
Namnyenyekea mume wangu vizuri tu kwasababu his manhood turns me on. Ni mtu ambae akiamua lake ni hilo labda atake ushauri wako tu. Kanikuta nna kazi, nilipoacha ili nilee watoto akanitaftia niendelee so kindly, hii sampuli ya wanaume wa humu jf inanichefua. Very intimidated
 
Safi, sasa nikuulize. Ni wote wanaojua pa kwenda kuomba msaada?

Ni kitu gani huwa kinapelekea hadi wanawake wanapitia hizi shida zote hadi wanashinda kuzurula mahakamani wanateseka na depression hadi kesi iishe inachukua miezi na miezi.
 
Mimi sijawahi kufanya kazi na mwanamke akawa hata supervisor huwa naona dharau kubwa sana.

Aisee tulifanya kazi na supervisor wa kike alikuwa ndio ametoka kupata mtoto ananyonyesha mtoto ana kama mwaka na miezi 2. Tulisafiri na yule mtoto wake maana ilikuwa ni kazi ya field na yeye ndie supervisor. Yaani ilikuwa ni Hell kwangu binafsi.

Kwenye gari tupo na mtoto na beki tatu wake na wenzangu watatu pamoja na dereva. Yaani tulikuwa tunapambana na malezi utadhani ile kazi ni day care. Mtoto amedekezwa so ana tantrums za kindezi kulia lia bila sababu. Yaani nilikuwa naomba tumove na kufika haraka location ili tushuke mzee.

Dah halafu ndio wale wadada ambao wana mawenge ingawa yeye personally ni mtu poa habanii ila ni ile kupelekeshana halafu ukionyesha dalili ya kutokubaliana nae anakuona kama tatizo anakumind ile ya utaona kama utapata tena huu mchongo wa kusafiri.

Dah aisee me ndio maana napenda sana kufanya kazi na team za wanaume tupu kusiwe na mademu, mtacheka, mtataniana, mtazinguana, mtatukana kwa uhuru, mtapiga kinywaji, mtapeana makavu. Yaani full amani.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umepanic bi dada sasa unaanza kuongea kama mlevi. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ungekuwa na busara ungekausha ila sasa zero unazidi kuchafuka. Unataka kukimbizana na kengedere twende kazi, utachoka wewe. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Safi, sasa nikuulize. Ni wote wanaojua pa kwenda kuomba msaada?

Ni kitu gani huwa kinapelekea hadi wanawake wanapitia hizi shida zote hadi wanashinda kuzurula mahakamani wanateseka na depression hadi kesi iishe inachukua miezi na miezi.
Kwanza elimu sahihi inahitajika mwanamke kujua kuhusu haki zake na wapi anatakiwa akapambanie haki zake.
Pili kunahitajika mtu wa kumshika mkono huyu mwanamke atajayemtia moyo na kumpa sapoti,maana hizi kesi ngumu sana zaweza kukukatisha tamaa mapema kama hauna wa kukushika mkono.

Hapo mwisho sijaelewa nifafanulie samahani,unauliza sababu ama chanzo cha hizi kesi ama unauliza kwanini inawachukua muda wao kumaliza kesi!!??
 
Huna hoja una jichekesha kama malaya kaona danga jipya
 
Hahahah

Unapochanganya hisia wakati wa kujibu maswali yangu ni lazma utakosa mantiki katika jibu lako.

Hisia zisikuendeshe unapojenga hoja. Huenda ukawa mke bora kwa mume wako au ukawa mke mzuri kwa mume wako.

Msingi wetu si kuona mwanmke anajiingiza kwenye tundu bovu yeye mwenyewe. Kwasababu maamuzi mabaya ya mwanamke humrudia yeye mwenyewe. Hivyo basi Tathimini sahihi pekee ndiyo itamfanya aonekane bora, tofauti na hapo usiwalaumu walimwengu.

Ndio maana unapaswa utambue madhara ya feminism ya karne ya 21 kisha ujue kwa namna gani inawaarhiri.
Huenda ukawa miongoni mwa watu utakaowakomboa wanawake wenzako.
 
Unazungumzia hii post??
 
Nauliza huwa ni kwanini mwanamke akifiwa na mume lazima ateseke kupambania mali za mume wake na watoto? Lakini mwanamke akitangulia akabaki mume hamna anaesumbua hata kama mali alizichuma mwanamke kwa bidii.

Hii scenario imekuja ofisini last month siwezi kuielezea hapa maana victim anaweza kuwepo jf akaumia au akaona natoa siri zake. Kwa ufupi tu, baba aliwatelekeza akaenda kutengeneza familia nyingine, mama akapambana na mtoto wake wakajenga nyumba from the scratch, sasa mama yao kafa yule mzee karudi anasema ile nyumba ni ya mkewe na hawakupeana talaka so ana haki nayo. Kesi ndo inaanza kusikilizwa mwezi ujao.
 
Reactions: Tsh
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Super Woman ashapaniki stress zimemtia uchizi, huku anatukana kila mchangiaji hadi mleta mada , afu anajisifu, She is a good wife, and beautiful woman kisa hatumuoni,
Huyu asipokuja kuwa Single mother au kuishia na mwanaume bandidu then labda sio mimi. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kuna demu tukiwa chuo alikuwa pisi kali ya kinyiramba. Kuna siku tumeketi nae unajua ile moment mpo na pisi kali mnabonga nayo, nikamuuliza, mahari yako hivi bei gani, akajibu "mimi kwasasa ndoa bado sana anaetaka kuona angoje nimalize kwanza elimu yangu at least masters halafu niwe nimepata hata kamchongo ka kazi ka miaka 3 then ndio tuoane". Tukamwambia sasa bibie namna hiyo si muda utaenda sana. Akatujibu kuwa yeye hana haraka maana siku akitangaza anataka ndoa hapo kwao msururu wa wanaume watakao jipanga kuomba kutoa posa ni sawa na wa wafanyakazi mwisho wa mwezi kutoa pesa kwenye ATM.

Dah fast forward leo hii. Demu alipigwa mimba mbili za fasta na jamaa m'moja dereva wa gari za tour tena yupo broke vibaya. Kalimaliza chuo kakasugua gaga kwa muda kwenye NGO kama tatu hivi, baada ya hapo kaka kutana na jamaa nasikia alikadanganya kuwa ni tour operator company manager ambayo anaimiliki na kaka yake na anafanya humo, demu akaingia kichwa kichwa akakichezea wakafunga ndoa yaliyomkuta hadi sasa ndio hayo anaishi maisha ya kipato cha kubangaiza sometimes mixer kulala njaa. Vitoto vina valishwa mitumba tena ile ya grade ya chini ya kuchakaa, kuna siku jamaa yangu ananitumia picha ya demu amesimama mashineni anasaga lishe ya watoto.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kummmk mambo ya kudharau wakunga na uzazi ungalipo, kutukana mamba kabla ya kuvuka mto, kuchoma madaraja ya njia ya kurudia na kuweka miba njia ambayo unaweza kurudi peku.
 
Ulishawahi kujiuliza ni KWA NINI WANAWAKE ILIFIKA MAHALI ILIBIDI NAO WAANZE KUFANYA KAZI NA SIYO KUSUBIRI WAWE MAMA WA NYUMBANI na KUSUBIRI wahudumiwe KILA KITU na waume zao?
 
Mwanamke asikae tu ananenepa. Fungueni hata mradi wa familia hata duka tu. Si kila wakati mambo huenda sawa, kuna nyakati mambo huenda shaghalabagala. Maoni yangu mkuu.

MUNGU aepushie mbali ila ukikosa uwezekano wa kuimbiwa wimbo wa ulinikuta kazini kwanini ulinitoa utausikia sana.
 
Kuna shida kidogo katika jamii yetu,hii shida ni kwamba mwanaume huwa ana ujazo ama uzito kuliko mwanamke.
Sijui hili nilieleze vipi?
Ila ile nadharia ya muoaji ndio provider imefanya muolewajwi awe inferior katika jamii.
Japo sio katika jamii zote.
Mali alizochuma mume mara nyingi katika jamii zetu za kiAfrica sio tu Tanzania huwa zinachukuliwa ndugu wa mume ndio wana haki,japo kiuhalisia haiko hivyo,mwenye haki ni mke na watoto.
Na ndio maana ni muhimu elimu itolewe kwa kina mama zaidi na zaidi ili watambue haki zao juu ya hili suala.
Mwanamke akitambua haki zake ni ngumu kudhulumika.

Japo hiyo kesi ya huyo mama ni nzito kiasi na inasikitisha,kuna wanaume wana roho mbaya sana aisee.
Mungu amjaalie mambo yaende sawa,ila kama anataka ashinde hiyo kesi,aende mahakama kuu ya mirathi Chang'ombe mbele ya Chang'ombe polisi kama unaelekea Temeke hospitali mkabala na jengo la NIDA.
Pale kesi husikilizwa directly na unalipia hela ya ufunguzi wa kesi tu 11,000/= elfu kumi na moja basi.
Akihangaika kwengine huwenda haki yake ikachelewa sana ama kupotea.
 
Context yako ya mwanaume kutaka mke wa kukaa nyumbani tu ni tofauti na context yetu wanaume kutaka mwanamke akae nyumbani.

Wewe unatazama kama mwanaume anataka mke akae tu kama msukule sababu haujui hata wanaume huwa wanalenga program gani kwa wake zao wakiwa nyumbani.

Mimi huwa nakuwapo nyumbani muda mwingi but i have my ways kumake money ambazo hata mwanamke wangu namtrain na anazimudu so ananisaidia hata nikuwa sipo hapa mjini. So kuna module ya maisha mwanamke anaweza ishi na akatengeza milioni 3 akiwa home yaani ile most of the time unamkuta home.

Mfano tunafuga kuku shambani huko ila hapo home ndipo tunawahifadhi kwenye mafriza na wateja wanakuja kuwachukulia hapo na amesomea accounting anatunza vitabu vya biashara zetu ila hatoki home yupo muda wote anarelax anatazama tv, anakula Netflix, anapika chakula nakuja kula narudi kitaa naendelea na harakati. Na tukipiga total ya mapato tunatengeneza zaidi ya milioni 4.5 kwa mwezi, shida inakuwa wapi?

Sasa wewe sababu ya kukosa kwanza exposure ya mahusiano, maisha ya ndoa, hujui vitu unaishia kutunga tunga unachokiona ni mwanaume akisema mke abakie home unaona mwanamke anaeteswa, amefunguwa kwenye chumba na kufuli, jamaa akirudi anamtandika bakora, anamuua halafu anamuua tena ana mfufua, yaani unaona maangamizi tu[emoji23][emoji23][emoji23]

Ndio maana nakwambia wewe unamatatizo ya akili na haya matatizo yatakuja kukupeleka direction ambayo sio yako. Endekeza tu hizi ligi, maneno yanaumba, ukikiwaza sana kitu kinakuja kukutokea maana si unakiita na mawazo yako?
 
Sasa kama haujaambiwa uache kazi povu la nini unagombana na wanaume wanaotaka wanawake waache kazi! [emoji1787][emoji1787]
 
Yes. Is it relatable na maisha yetu ya kiafrica? Mrs GSM kampa zawadi ya nyumba mumewe recently, ela katoa wapi kama yeye ni mama wa nyumbani?
Anhaa!!
Nahisi mapokezi umeyapokea tofauti madam.
Hii comment inazungumza mengi na ina maana nyingi, ila wanawake hutofautiana vipato.
Wengine wamezaliwa teyari washaundiwa mazingira toka katika familia zao kama huyo mke wa Ghalib Said Muhammed.
Huyo mkewe katoka katika familia ya kitajiri,rahisi kufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…