Katikati ya harakati za 50/50 kinyume chake wanawake wengi siku hizi hawana furaha

Nikiwa darasa fulani la sheria mwaka 2018 niliwahi kuuliza hivi "je, kwa harakati hizi za 50/50, mizani ikizidi yaani wanawake wawe juu zaidi, zitaanza harakati za kuwashusha wanawake na kuwainua wanaume?"
 
Je bibi hakuwa anafanya kazi? Ndio mnawadanganya wanawake ili muwape mikopo uchwara ya biashara n.k inayowapelekesha resi kama wanevuta bangi

Sijakuelewa Mkuu.

Bibi yangu alikuwa Mwalimu kipindi cha Nyerere, Mwinyi na Mkapa.
Kwetu Mwanamke lazima afanye kazi iwe ya kuajiriwa au kujiajiri.

Kuchukua mkopo ni ishu nyingine Mkuu.
Kwani wanaume hatuchukui Mîkopo?
Taifa lako unajua linadaiwa kiasi gani?
Marekani ambaye ndiye kiranja wa dunia unajua anadeni kiasi gani?

Kama mwanaume ni vizuri kujadili mambo kwa mantiki ili kulinda heshima ya uanaume ambayo Mungu alitupa.

50*50 hata mîmi sikubaliàni nayo katika baadhi ya muktadha lakini hiyo haimaanishi kuwa muktadha mwingine isitumike.

50*50 katika kupata haki za kupata huduma za kijamii kama elimu, afya, fursa, n.k. ni sahihi.

50*50 katika wajibu na majukumu ya kifamilia hapo lazima umakini uwepo. Huu itatokana na kuwa familia ni taasisi aû ufalme mdogo unaojitegemea
 
Huyu mtoa mada hanaga linguine zaidi ya kuongelea 50/50 kama li mke lako ni Limama la nyumbani then tulia, hii vita ya kusafisha 50/50 won't get you anywhere...pumbafu.
Af wenzie wanamtetea eti hajaongelea kwa ubaya🤣 tushawahi kupopoana kwenye mada na huyu jamaa mwaka 2022 alikua anatukana wanawake kinoma. Nahisi kaoa jitu gani sijui au bosi wake ni mwanamke basi anamsumbuaa
 
Dunia haimsubiri mtu, kaeni hapo kusubiri wanawake wabadilike muone kama dunia inarudi nyuma. Stress ni part ya maisha ya mwanadamu, kivipi stress itumike kama tusi?

By far kunafaida lukuki za maisha katika mfumo wa sasa, kuliko mfumo wa uzamani, ndio maana baba na mama zenu waliona ni vyema kumuwezesha mwanamke ili ajitafute kiuchumi kuliko walivyopata kuishi wao.

Zamani wanawake hawakuwa na stress au hakukuwa na social interaction ya kudisplay hizo stress zao? Msipende kuwaongelea wanawake wa zamani kabla hamjavaa viatu vyao kuona how did they feel about the world... wanawake wazamani kupigania uwezeshwaji wa mtoto wa kike, ni ushahidi tosha kuwa walikuwa na stress zao, zilizopelekea wao kuona mwanamke akiwezeshwa kuna aina ya stress itaondoka, unfortunate imeondoka hiyo imekuja stress mpya, which
is okay, mnategemeaje maisha bila stress? Again we are tired with ya'll weak minds mnaotamani dunia ambayo ni stress free... mko delulu.

Mnajadili mada makini kibinafsi na kiufunyu wa fikra sana, na haisaidii wala haijengi.
 
Kabisa, hawa wanaojiita wanaharakati wanawaharibia wenzao tu wengi wenyewe wameshapigwa matukio. Shida ni pale tunapotaka mwanamke afanye majukumu ya mwanamme na mwanamme afanye ya mwanamke. Hii ni shida sana tusipokuwa makini kulinda utamaduni wetu tutaishia kama watu wa west, kuwa na maisha mazuri bila furaha kwani wanawake wamechukua power sana kiasi family zinayumba kila leo.
 
Umeongea kwa hisia lakini umeongelea aina moja ya mume sasa swali kwako, je kama una mume anayewajibika kama mume. ana provide mahitaji yote muhimu, akitoka job yuko nyumbani tu na wewe na akitoka na family yake, kujumla anatimiza kwa uwezo wake mahitaji yako kifedha, mapenzi na uaminifu. Kama mke nini zaidi utataka kwa mume? Point moja muhimu umeongea mume mnyime chochote lakini red line ya mume ukimvunjia heshima kama humuheshimu basi ndoa inaenda kufa.
 
Hakuna nyumba ikasimama imara ikiwa mke anamtawala mume hata kama mke ana kipato kikubwa kuliko mume lakini kama humpi nafasi ya mume kuwa kiongozi wa family basi haitadumu. Ila kuongezea hapo hata mume kuwa kiongozi sio kwamba ndio awaburuze tu hapana, mume mwenye busara kama kiongozi ni kumshirikisha mke katika mambo ya maamuzi hata kama yeye ndio mwenye sauti ilajenga mapenzi.

Umeongelea mume zero brain, sasa wakati unamkubali hukujuwa kama ni zero brain? Mfano mmoja tu, ofisi unayofanya kazi labda una Manager lakini haina maana kuwa hakuna watu wa chini labda wana uwezo kuliko huyo Manager lakini ni lazima utampa heshima kama kiongozi basi na family is the same.
 
Unahoja ila umesimanga sana mkuu 😀. Hata talaka zimekuwa nyingi, achilia mbali uoaji wenyewe pia ni kama unatoweka.
 
There is an exception to the general rule.

Sasa mimi kinacho nishangaza ni vile wanaume wa jf wanavyo generalize kwamba wanawake wote wanaofanya kazi ni madume
Jike as if hao wote waume zao ni sweet loving husbands. Wanahesabika mkuu. Sijui niwaambiaje
 
Turudi miaka 50 nyuma, wanawake hawakuwepo kwenye nafasi mnazosema walikua wanashinda majumbani kulea watoto, je, wote waliolewa? Wote walidumu
Kwenye ndoa zao miaka yote? Hapakua na single moms? Wanaume ndo walikua wanazaa kama kuku mnakuja kujua siku za misiba.

Wanawake walikua wananyanyaswa kwasababu hawakua na kipato. Ndo chanzo cha harakati. Na harakati zilipoanza hawakumaanisha 50/50 kwenye familia bali kwenye fursa ili wanawake wajitafute wasiwe wananyanyasika majumbani.

Sasa mnataka turudi kwenye zile zama ili tuwe tunapigwa au shida ni nini?

Hao wanawake wanaofanya kazi waache waende kudanga ndo mfurahi?? Au mnataka wote wawe wauza baa.

Baadhi ya wanaume kuna kitu kina nipa alert mna shida mahali. You are intimidated by women’s success kwasababu hata wanawake ambao hawana kazi bado mnawa cheat, bado mnawazalia watoto mnawaleta kwasababu mnajua hawana pa kwenda. Hicho ndo mnachotaka.

Men step up your game. Vaeni mamlaka sio kulalamika kwenye forums. Kazaneni kufanya kazi mtuzidi vipato.
 
Nikisoma maandishi yako, sio bure una stress na Kuna vitu ume/unapitia...pole, ila tafuta professional counseling.
 
Hili sio sawa kila familia ina changamoto zake wengine ni lazima kila mmoja afanye kazi ili maisha yaende ila kubwa la msingi haijalishi unafanya kazi au mke wa nyumbani basic ni zile zile kuheshimiana. Labda wale wanawake wakianza kufanya kazi basi wanajiona wako sawa na mume. Tujikumbushe hotuba ya Rais wetu, alisema pamoja kuwa yeye ni Rais wa nchi lakini kwa mume wake anampigia goti, powerful message.
 
Hiki sicho ambacho wana ki advocate wanaume wenzio humu. HAWATAKI MWANAMKE AFANYE KAZI! Sijui tunaelewana. Yani hilo suala la heshima ni la kwako wewe. Kwasababu sio kweli kwamba wanawae wanaofanya kazi wote hawaheshimu ndoa zao na sio kwamba wasiofanya kazi wanaheshimu waume zao.

Kuna mentality hapa ipo na ndo nnayoikataa. Wenzako hawataki wanawake wafanye kazi because wanaamini automatically mwanamke atakua na dharau. Sijui kwanini wako negative kiasi hiko.
 
Labda ndio tujiulize kwanini? Mimi nadhani wanakuwa wanaona wanachowafanyia wake za watu huko makazini au wanaona sasa inawatia hofu japo hata mke wa nyumbani tu anaweza kufanya. Ila lazima tukubali kuna mambo yapo yanatokea ndio chanzo cha hii hofu. Yes sio wote ila chance ya kushawishika huko ni kubwa lakini nasema tena sio wote.

Sasa mimi kama mimi, sipendelei mke wangu afanye kazi ya kuajiriwa ila ni wajibu wangu kutimiza part yangu, na sababu ziko nyingi. Mkiwa mna familia changa Mme katoka asubuhi mke katoka asubuhi mnarudi jioni watoto wako na dada hii inanipa shida sana, gharama zake huko mbeleni zitakuwa kubwa sana. Ndio maana nimesema tugawane majukumu mimi nitafute wewe angalia familia. Tukianza kuingiliana majukumu ndio shida inakuja hapo.

Mke akiwa home tu hakuna mtu atauliza kwanini, sababu yuko kwenye jukumu lake lakini mwanamme akikaa home tu inakuwa issue, mke mwenyewe atamwambia mume wangu toka uhangaike sababu sio sehemu ya jukumu lake kukaa home tu.
 
Hongera kwa kutumia neno baadhi. Sasa ndo unaelewa nnaposema wenzio wana generalize. Yani mimi niko kazini na sijawahi kuwa na mahusiano na mtu yoyote. Na kwa maisha ya sasa hivi mwanamke tegemezi ana kipengele cha maisha ya manyanyaso asipokua makini.
Rai yangu: wanaume wabaki na matamanio yao ya kuoa wanawake wa kuwaweka ndani ila wakawatoe kijijini, sio hawa ambao wazazi wao wamewasomesha hadi nchi za nje af uje umuachishe kazi.

Hawa mnaowaona mjini kama wanaliwa kwani ni wa kwenu? Kila mtu apambane na ndoa yake.

Kinachonishangaza zaidi kila siku ni mada kuhusu wanawake lakini hakuna anaeongelea kuhusu hawa wanaume marioo, yani huyu anataka atumie ela za mwanamke kwenda kufanyia uanaume
Wake wa kuzaa nje, kuna vitu vinachekesha sana
 
Kuna mdada jana nilikaa zangu sehemu kuna kama kagiza hivi akaawa amekuja na mwenzake mimi simfahamu ila namfahamu huyo mwenzake na huwa tuna utani wa kuitana mama na mtoto wake.

Sasa jana, akaja na huyo dada dukani mimi nimeketi kwa pembeni kuna kama kagiza hivi nimevaa sweater la hood nimejifunika ngumu mtu kunijua.

Sasa walipofika, yule dada ninayemjua akaniamkia kwa adabu na yule mwenzake akaunga tela kuniamkia, nikawaitikia kwa sauti ya uzito hawakunijua, wakaenda dukani na kutoka sasa wakati wakirejea kutoka dukani ndipo nikawaita kwa kumwita yule ninae mfahamu, aliponijua akacheka sana akawa ameanza utani kwa kunambia nimepokea shikamoo wakati mtoto wa juzi tu hapa najifanya mzee. Me kwa masihara nikamjibu sasa shikamoo kupewa na mwanamke si ni halali kwanza mwanaume mkilingana umri au akikuzidi hata mwaka m'moja unatakiwa kumuamkia. Akacheka sana halafu akawa anamwambia mwenzake kuwa tumemwamkia bwana mdogo huyu atupe shikamoo zetu.

Sasa yule demu akawasha tochi ya simu akanimulika usoni, mimi nikamwambia yule ambaye ninamfahamu kwamba yeye anamind shikamoo yake wakati mwenzake ameridhika kabisa kunipa shikamoo tena kwa adabu. Weeeeee yule demu ghafla sura ikabadilika. Anaonekana ni msimbe wa kama miaka 34 kama sio 35.

Aiseee sura ikawa utadhani mtu aliyemuona X wake aliyemtelekeza na watoto. Akasema yaani me najua ni mtu mziiiima kumbe katoto tena ka elfu mbili, me nikamwambia kwan kama nimezaliwa 2000 kuna ubaya gani ukinipa shikamoo yangu kama kidume, akajibu kidume utakuwa wewe me nikupe shikamoo kwa kipi unachostahili? Imagine huyu mtu hatujuani ndio kwanza nimemuona hapo kwa mara ya kwanza ila ndio ameanza kuwa na maneno ya kashfa kwa kitu ambacho kingeweza kuwa utani tu na tukamalizana bila alterations zozote.

Akawa sasa kama mtu amepigwa na shoti midomo,sura na mwili unamuona kabisa inatetemeka anaonekana kama alipatwa na jazba kali akawa kama anataka kuanzisha tifu ili tuanze rushiana maneno. Mwenzake akashtukia akaanza muondoa ile ya utani huku ananiambia hiyo shikamoo utarudisha hata kwa makonzi. Me nikawa namzingua yule mwenzake nikamwambia sirudishi tena ya mwenzako nimeipenda nataka tukikutana tena ndio iwe utaratibu, demu akajibu nenda nyumbani ukabadilishwe Pampers na mama haraka unachelewa. Hapo uso alioweka ni ule wa hasira.

Sasa unachosema mleta uzi si jambo la uongo kabisa ni ukweli kabisa hii kitu na si kawaida. Sijui ni chakula, hormones, hali ya hewa ama kitu gani, wanawake wa sasa hata mama zetu wanakiri kuwa kuna shida eneo la tabia. Tukiwasema wanasema tunawaandama.
 
Muachishe huyo zombie wako kazi. Kwani walioko makazini nao ni wake zenu? Mbona mna uchungu nao sana!

Au mnatamani muwe mnavaa pedi pia maana sielewi hasira ni za nini!
Duh unaonekana una hasira wewe...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…