PostGE2025 Kesi ya Ugaidi ina Dhamana? Kwanini Viongozi wa CHADEMA wamepata Dhamana? Kuna presha ya maridhiano?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kwanini una shida na maridhiano? Huoni kama ni afya kwa nchi kama pande mbili zitakuja kwenye maridhiano.

Kumbuka mauaji ya Pemba 2001, Maalim Seif alitembea Ulaya yote kuiomba jumuiya ya Kimataifa iinyime misaada Zanzibar. Mwisho wa siku CUF na Maalim Seif walirudi kwenye meza ya maridhiano. Jumuiya ya Kimataifa sio rafiki kihiivyo kama malengo yao hayatimii. Tujifunze kwenye kisa cha 2001.
Hayo maridhiano kwa chama cha siasa yatakuwa na maana gani kama hawana kiti cha uwakilishi Bungeni,mkiridhiana leo halafu ilifika 2029 wawekwe tena ndani wasishiriki uchaguzi wa 2030???

Hiyo guarantee kuwa mtawala mwaka 2029/2030 kuwa hatafanya kama sasa hivi itatoka wapi?
 
Hamna maridhiano, ni namna ya kuafisha image yao in eyes of international community maana huko nje msala ni mkubwa mno
 
Unataka majadiliano au maridhiano kama hata yatakuwepo yawe ni jinsi gani nyanya vitunguu na unga wa ugali vitashuka bei??
Huwa unaandika kama kichwa panzi ambaye hajui msingi wa chanzo cha matatizo ya hii nchi.
Kama hujui msingi wa matatizo ya nchi yoyote basi huwa ni madaraka, utawala bora, haki, katiba, muundo wa utawala n.k hayo mengine yanahusu kuridhishwa au kuridhika kwa mtu wa chini raia wa kawaida ni matokeo tu ya kuharibika hayo niliyokutajia.
Unashida wewe si bure, na angalia usije ukawa unachukia mtu kisa kwa kushindwa kuelewa kwako.
 
Maridhiano bila UWAJIBIKAJI ni TAKATAKA!
Halafu sisi sio Pemba! Bila watu kuwajibika kwa vifo zaidi ya 2000 vilivyotokea HAKUNA Maridhiano.
Kwenye meza ya Mazungumzo ndio zitawekwa hizo TERMS..hii ni nafasi ADIMU kwa CDM, kikubwa wajipange tu ...jamaa wamejaa
 
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania mtu anayetuhumiwa au kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi hawezi kupata dhamana, kitu ambacho tulikitegemea kwa viongozi wa CHADEMA kina Lema, Heche, Boni Yai na Golugwa. Wawasumbue weee kama wanavyomsumbua Lissu, mwishoni DDP aseme hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Sasa imekuaje kwa viongozi wa CHADEMA waliokamatwa hivi karibuni? Imeakuaje wamepata dhamana kama kutuhumiwa na suala hilo hakuna dhamana?

Pia soma Polisi yawachia kwa DHAMANA viongozi wakuu wa CHADEMA waliokamatwa akiwemo Heche

Au kuna tobo ambalo wanasharia wanaliona sisi wengine ambao hatujui sheria hatuna elimu nalo? Embu mje mtusaidie hapa, hii imekaaje?

Kwa upande mwingine, ni presha ya maridhiano ndio imeleta yote haya baada ya Dunia nzima kusema uchaguzi haukuwa huru na haki? Sasa wanatafuta namna ya kuwapoza viongozi wa upinzani kukubali maridhiano?

Sitegemei Lissu akaja kukubaliana na haya maridhiano batili baada ya wenzetu zaidi ya elfu 2 kuuliwa! Akifanya hivi itakuwa ni usaliti mkubwa sana, yaani sitaki hata kufikiria.
Architect wa kesi ya kubumba ndiye anayeamua kesi iendeje!
 
Muda wa kubembelezwa na kupewa mi hela ndo huu walokufa washakufa.
Ili mjue kuwa ushabiki wa kisiasa sio
 
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania mtu anayetuhumiwa au kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi hawezi kupata dhamana, kitu ambacho tulikitegemea kwa viongozi wa CHADEMA kina Lema, Heche, Boni Yai na Golugwa. Wawasumbue weee kama wanavyomsumbua Lissu, mwishoni DDP aseme hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Sasa imekuaje kwa viongozi wa CHADEMA waliokamatwa hivi karibuni? Imeakuaje wamepata dhamana kama kutuhumiwa na suala hilo hakuna dhamana?

Pia soma Polisi yawachia kwa DHAMANA viongozi wakuu wa CHADEMA waliokamatwa akiwemo Heche

Au kuna tobo ambalo wanasharia wanaliona sisi wengine ambao hatujui sheria hatuna elimu nalo? Embu mje mtusaidie hapa, hii imekaaje?

Kwa upande mwingine, ni presha ya maridhiano ndio imeleta yote haya baada ya Dunia nzima kusema uchaguzi haukuwa huru na haki? Sasa wanatafuta namna ya kuwapoza viongozi wa upinzani kukubali maridhiano?

Sitegemei Lissu akaja kukubaliana na haya maridhiano batili baada ya wenzetu zaidi ya elfu 2 kuuliwa! Akifanya hivi itakuwa ni usaliti mkubwa sana, yaani sitaki hata kufikiria.

Maridhiano ya nini hasa? Chadema na wadau msimamo ni ule ule no reform no election sasa maridhiano mnayo ongelea ni yapi. Walio andamana sio chadema kafanyeni maridhiano na hizo familia mlizo uwa watoto wao.
Kitaifa hakuna Amani bila katiba mpya sio kudanganyana tena
 
Yaani sasa Chadema wana nguvu kuliko kabla ya uchaguzi kwanini watake maridhiano kwa faida ya nani? Katiba mpya ndiyo jibu pekee
 
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania mtu anayetuhumiwa au kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi hawezi kupata dhamana, kitu ambacho tulikitegemea kwa viongozi wa CHADEMA kina Lema, Heche, Boni Yai na Golugwa. Wawasumbue weee kama wanavyomsumbua Lissu, mwishoni DDP aseme hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Sasa imekuaje kwa viongozi wa CHADEMA waliokamatwa hivi karibuni? Imeakuaje wamepata dhamana kama kutuhumiwa na suala hilo hakuna dhamana?

Pia soma Polisi yawachia kwa DHAMANA viongozi wakuu wa CHADEMA waliokamatwa akiwemo Heche

Au kuna tobo ambalo wanasharia wanaliona sisi wengine ambao hatujui sheria hatuna elimu nalo? Embu mje mtusaidie hapa, hii imekaaje?

Kwa upande mwingine, ni presha ya maridhiano ndio imeleta yote haya baada ya Dunia nzima kusema uchaguzi haukuwa huru na haki? Sasa wanatafuta namna ya kuwapoza viongozi wa upinzani kukubali maridhiano?

Sitegemei Lissu akaja kukubaliana na haya maridhiano batili baada ya wenzetu zaidi ya elfu 2 kuuliwa! Akifanya hivi itakuwa ni usaliti mkubwa sana, yaani sitaki hata kufikiria.
Ina dhamana inategemeana aliyekukamata ni nani
 
Maridhiano ya nini hasa? Chadema na wadau msimamo ni ule ule no reform no election sasa maridhiano mnayo ongelea ni yapi. Walio andamana sio chadema kafanyeni maridhiano na hizo familia mlizo uwa watoto wao.
Kitaifa hakuna Amani bila katiba mpya sio kudanganyana tena
Maridhiano yanatakiwa yawe hivi
1. Katiba mpya ndani ya miezi 18 (mwaka mmoja na nusu).
2. Uchaguzi mkuu huru utakaosimamiwa na tume huru ya uchaguzi ndani ya miaka miwili
3. Kuwajibishwa kwa waliohusika na mauaji ya raia October 29 na siku kadhaa mbeleni.
4. Uchunguzi huru wa mamia ya watu waliopotea kuanzia mwaka 2015 uanze ndani ya miezi sita.
5. Kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wenye kesi za kisiasa au zitokanazo na kesi za kesi na kesi hizo kufutwa.
6. Kukubali usaidizi huru kutoka nje kwa viongozi wastaafu wa Africa wanahoshemika ili kutengeneza mazingira ya maridhiano kuaminika.
 
Gwajima akitoka mafichoni yeye atang'ang'aniwa bila dhamana!
 
Hawa ******* kina Katuga na wapumbavuwenzake wanajua kabisa hapo hakuna kesi bali ni uhuni tu wanafanya, ila wajuwa phase II ya maandamano lazima tuwasalimie
 
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania mtu anayetuhumiwa au kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi hawezi kupata dhamana, kitu ambacho tulikitegemea kwa viongozi wa CHADEMA kina Lema, Heche, Boni Yai na Golugwa. Wawasumbue weee kama wanavyomsumbua Lissu, mwishoni DDP aseme hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Sasa imekuaje kwa viongozi wa CHADEMA waliokamatwa hivi karibuni? Imeakuaje wamepata dhamana kama kutuhumiwa na suala hilo hakuna dhamana?

Pia soma Polisi yawachia kwa DHAMANA viongozi wakuu wa CHADEMA waliokamatwa akiwemo Heche

Au kuna tobo ambalo wanasharia wanaliona sisi wengine ambao hatujui sheria hatuna elimu nalo? Embu mje mtusaidie hapa, hii imekaaje?

Kwa upande mwingine, ni presha ya maridhiano ndio imeleta yote haya baada ya Dunia nzima kusema uchaguzi haukuwa huru na haki? Sasa wanatafuta namna ya kuwapoza viongozi wa upinzani kukubali maridhiano?

Sitegemei Lissu akaja kukubaliana na haya maridhiano batili baada ya wenzetu zaidi ya elfu 2 kuuliwa! Akifanya hivi itakuwa ni usaliti mkubwa sana, yaani sitaki hata kufikiria.
Hiyo kesi imekuwa filed kwenye mahakama gani?
 
WATAKUWA WAMESHAFIKA BEI, LISSU KAGOMA NDIO MAANA BADO YUPO NDANI
 
Back
Top Bottom