Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Mkuu,

Kuna watu wanataka kuwa control wanawake tu.

Hata wasiowajua.

Hata wale ambao hawatakutana nao.

Hata wale ambao hawajazaliwa bado.

Hata wale ambao watazaliwa baada ya wao kufa.

Yani kwao hii ni ligi, wanaona raha mwanamke akiwa chini.

Na mwanamke akianza kupata uhuru kidogo tu, wanaona vibaya sana.
 
Mkuu kuhusu mm kuwa mwanaune anaye mtaka huo uongo, ukweli ni kuwa amedoda sasa walio kuwa wanamfanya anikatae kwa sasa wote hawamuhitaji tena😃😃😃😃.
Alafu hata kama hiyo ingekuwa kweli mm nimesha oa na hilo nimesha mwambia sasa mbona haelewi?
Dahh itakuwa kakosa options kabisa!
Kuhusu pesa mm nina kipato cha kawaida tu kinacho niwezesha kuishi mjini tu na kubadilisha mboga na kukidhi mahitaji ya msingi ya kifamilia tu sina hizo pesa za kumfanya mwanamke anibabaikie.
Kuna watu hiyo inatosha kwao! Hahha huyo kakosa pa kwenda mpk kutafuta alowakataa😅 pole yake aandae retirement plan tu mwenyewe nmeshaandaa hapa lazima uwe na plan b🤣
 
Nilipitia hali hiyo, niliulizwa maswali, nililetewa wachumba, nikakalishwa chini kuulizwa kwa kituo, nikawaambia mimi sivutiwi na wanaume, nikaibua mjadala mzito ajabu baba angu na kaka zangu hawakushughulika na mie ila mama na mabinti zake walinivalia njuga.... hatimae nikawaletea mtoto/mjukuu walipoa na sasa wanaanza tena ooh ongeza mwingine, lol, waswahili huwezi kuwaridhisha, ishi maisha yako vile unavyotaka..... i send you my warm hug
 
Kinachochangia kwa vijana wengi kushindwa kuoa au kuolewa mapema ni pamoja na kuwa na vipaumbele elimu kwanza, ajira, sehemu ya kuishi nzuri hata ya kupanga lakini wakati mwingine mambo huenda hovyo na hapo ndipo changamoto zinapoanza kumbe kipaumbele cha kwanza ingekuwa kuolewa au kuoa Yawezekana isingekuwa shida kwenye hili suala la ndoa.

Ukiachana na masuala ya Kiafya naambo mengine tatizo kubwa ni vipaumbele nilivyoviandika hapo juu vikifeli kila kitu kinapoteza muelekeo na tunaoishi mjini mtindo wa maisha unaharibu sana muonekano wa miili yetu
Umeandika kweli yote,hata mleta mada upo uwezekano wakati wa usichana wake alitokea/walitokea wenye nia ya kumuoa ila akafungwa na uamuzi wa elimu kwanza familia baadae unfortunately sasa yupo tayari waoaji hawamuelewi.

Na mbaya sana hii inakula zaidi kwa wanawake mwanaume umri wowote ana uhakika wa kutokuwa rejected ila mwanamke kuna age akifika hata kama msafi vipi maswali yatakuwa mengi kwa waoaji.
 
Sijui ni mie ama Niko sensitive sana?

Ninapokutana nao katika maongezi nikipigwa Hilo swali najikuta na-blush huku ndani naumia, mchangayiko na aibu na huzuni. Natoa majibu ya hapana bado. wakiendelea najikuta nashindwa hata kujieleza napata kigugumizi.

Shida sio kupata mchumba, shida ni njia zimetofautiana,njia anayopitia mwingine haiwezi kuwa sawa na anayopitia mwingine. Jambo linaweza kuwa rahisi Kwa mwingine lakini upande wa mwingine likawa tofauti.

Jamii yetu ime-adapt kama ndio njia sahihi impasayo kupitia Kila mtu Kwa wakati fulani, pale utakaposhindwa kuipita kwa wakati inageuka maumivu.

Binti uko over 30 huna hata mchumba, huna mtoto wanabaki eeh🙄
Na je, ikiwa mtu ataamua Kwa maamuzi yake kubaki hivyo ni kosa?

Kwa upande wa wengine mapungufu yanachangia, ndio tuna mapungufu ya hapa na pale kama changamoto za kiafya, kimwili zinazopelekea kukosa mwenza. Dhahama na magumu utayokuwa unayapitia mwenyewe na Ile hisia unaipata mwenyewe lakini wengine hawawezi kuuhisi huo mzigo unaoupitia.

Utasikia "jikubali mbona wapo wengi tu wanaingia kwenye ndoa, Wana familia? Wanakushangaa. Shida ni hawajui ni rejection ngapi unapitia, hawahisi mzigo wa maumivu unaobeba.

Hakuna anaependa kukosa kitu, Kila mtu anatamani kukipata on time, lakini kuweka kama utamaduni mtu kuwa na kitu Fulani katika wakati fulani mi naona ni kuumiza hisia na moyo wa mtu Ambae kwake ni ngumu kupata.

Yangu ni hayo Kwa Leo🥹
Tumekuelewa, wanakuja DM.
 
Kama ikitokea ndio
Tulia necha iamue ,hizo presha NI sehemu Tu ya KElele za chura hazitamzuia Tembo kunywa maji😂😂😂

Pole Kwa maswali unayopitia wewe sio Mbaya ila muda na Mtu wako vipo njiani au wewe ndio upo njiani bado hujafika.

Haya mambo NI mtiririko wa mambo mengi hivyo tulia Kwanza ,utakuta kuna mtu anakusoma Kwanza iliajeajivishe mabomu😂🤣🤣🤣
 
Dahh itakuwa kakosa options kabisa!

Kuna watu hiyo inatosha kwao! Hahha huyo kakosa pa kwenda mpk kutafuta alowakataa😅 pole yake aandae retirement plan tu mwenyewe nmeshaandaa hapa lazima uwe na plan b🤣
Na bora asingenikataa kwa nyodo kwanza huyu demu hana aibu kabisa maana kwa Yale maneno aliyo nitamkia siamini kama ndo yeye ambaye sasa hivi eti ananisumbua sijui lengo lake nn na hakati tamaa.
Sasa hivi nimekaa kimkakati maana anavyo nisaka anaweza kunipiga kipapai akaniteka nikatelekeza familia.
Nakatika kitu ambacho siwezi kuthubutu kufanya ni kumkubalia kwa lengo eti la kupiga na kukimbia inaweza kujidanganya kumbe ni mtego nikanasa mazima nitakuwa fala wa mwisho Dunia hii.
 
Halafu tukaendelea poa tu.

Mshua kwanza kuulizia tu kama issue tunaweza kuiongelea alionesha anaijua dunia. Hakutaka kujipa manyota tu kwamba kwa sababu yeye Baba basi issue inaongeleka tu.

Halafu kukubali jibu hilo bila hiyana alionesha aliomba ruhusa kweli, si kimaigizo tu😂😂

Ninaposikia hizi hoja nakumbuka sana siku ile.

Natamani wazazi, wazee, ndugu, jamaa, marafiki wote wangekuwa na adabu hivyo.
Ila Kiranga😂😂😂😂
 
Pole mkuu, tujitahidi kuwahimiza wadogo zetu, wakiwa kwenye nafasi ya kuoa au kuolewa wasifanye makosa. Ukishavuka 25+ ngumu sana kumpata mwenza sahihi.
 
Back
Top Bottom