Okay...ngoja nikujibu kisomi.
1. Wazungu walifuta mila za kuua mapacha, kula mbilikimo kusini mwa Tz, kafara za watu kimila na imani nyingi potofu tulizokua nazo wa Africa.
Bila shaka haya uliyoandika hapa umeyatoa katika vitabu vya wazungu ambavyo vimeandika hivi kwa lengo la kukupotosha wewe mwenyewe, na wengine wanaoamini kilichoandikwa.
Ili na mimi niamini kile ulichoandika, naomba uniweke historia iliyoandikwa na waafrika wenyewe ambayo inazungumzia kuwa sisi waafrika tulikuwa tuna wauwa mapacha, kula mbilikimo kusini mwa Tz na hizo imani potofu unazozungumzia hapa naomba unifafanulie ni zipi?
2. Ukristo ulifika Afrika kabla ya kufika kwa wazungu, Na Ethopia ndio ilikua na biblia ya zamani kabla hata ya ulaya , biblia ya mwaka 1600's.
Una uhakika gani kuwa Ukristo ulifika Afrika kabla ya kufika kwa wazungu Ulaya? Ulikuwepo?
Kumbuka pia Israel ilitakiwa iwe Africa na sio mashariki ya kati!
Wazungu walitumia dini ya haki kutapeli waafrika .
Ewaa hapa nashukuru kwa kuweka wazi kuwa Israel ilitakiwa iwe Afrika, ila wazungu wakaifosi iwe mashariki ya kati ambapo nchi hiyo haikutakiwa kuwa. Kwa maana hiyo wazungu wametudanganya kwa kutulazimisha tuamini kuwa hiyo nchi ya kipalestina ni ya waisrael tena weupe (wazungu) na wakati israel halisi ilitakiwa iwe Afrika kwa waafrika kama mimi na wewe.
Uongo wao unazidi kudhihirika tu kama nilivyoandika.
3. Israeli in jeshi kubwa na la kisasa africa na mashariki ya kati, na wenyewe walisema vita inaweza kuchukua miez 6 had mwaka kwa sababu hawana akili ndogo wadondoshe makomboza ya Jerico 3 gaza ili kuua hamas na wapalestina wote...ambayo ingekua kaz ya saa 1 tu na hakuna mwanajeshi wa israel angeingia kwenye vita vya mjini ambavyo inabidi uuwe gaidi aloyevaa kiraia bila kuua raia, sijui unajua ugumu wake?? Huwez ukajua, ila hata wapelestina wanaokufa ni hitilafu za kivita 2.
1. Israel ni nchi, wakati Gaza ni kamji ambako kanaingia kwa Israel zaidi ya mara kumi.
2. Israel ina jeshi kubwa lenye wanajeshi zaidi ya laki 2 na kitu, huku Hamas ikiwa na vijana wasiozidi elfu 20 ambao wamejitolea kupigania ardhi yao iliyoporwa na wazungu kisha kupewa Israel ambayo kwa mujibu wako walitakiwa wawe huku Afrika na sio Palestina ambapo sio kwao.
Israel kama nchi yenye eneo kubwa zaidi ya Gaza, na jeshi kubwa zaidi ya Hamas, tunaambiwa ina silaha kubwa na za kisasa ambazo wanazitengeneza wao na zingine zinatoka kwa washirika wao haswa Marekani, Hamas wao hawana silaha kubwa, sio za kisasa ambazo nyingi wanazitengeneza wenyewe kwa lengo la kujilinda na uvamizi huo wa wazungu wanaojifanya waisrael.
Sasa kutokana na utofauti nilioueleza hapo juu kuanzia kwenye ukubwa wa nchi, jeshi na silaha, kama kweli israel ina jeshi lenye ueledi basi wangetuma kikosi kidogo kinachoshabihiana na Hamas, wakatenga silaha kidogo zinazoshabihiana na zile za Hamas na pia isingefanya ni jambo la nchi nzima kuingia vitani na kaeneo ambako hakafiki hata robo ya nchi yao.
Kuingiza nchi nzima vitani, kutumia jeshi zima na kuita hadi wale wa akiba, kupeleka midege, meli za kivita, na vifaru kupambana na vijana wachache katika eneo chache na wenye silaha chache, huo ni uthibitisho wa kweli kuwa Israel haina weledi wowote wa kijeshi.
Ndio maana pamoja na kujifanya kuwatetea kuwa eti wanakataa kumaliza vita kwa siku moja ili wasiuwe wapalestina na Hamas sikubaliani na wewe kwa sababu kama kuuwa wapalestina washawauwa maelfu ya wasiokuwa na hatia, tena watoto wachanga na kina mama wasioweza kushika hata kisu.
Ni sawa na wewe, mkeo, watoto zako na wadogo zako mchukue mapanga, marungu, vyundo na silaha zingine kubwa za hatari muende kwa jirani mkapambane na watoto wadogo waliompiga mtoto wako ambao pamoja na udogo wao lakini pia hawana silaha kubwa kama ulizoenda nazo wewe. Hapo mkiwapiga hao watoto na misilaha yenu pamoja na kundi lenu lote, utajisifu kuwa nyinyi mna nguvu kweli kwa sababu ya kupambana na watoto?
Silaha na nguvu anazotumia Israel alitakuwa azitumie pale anapopigana na nchi nyingine yenye jeshi kamili, silaha kamili na nguvu kamili. Sio kutumia misilaha yake na ile ya Marekani kupigana na kakundi kadogo kwa zaidi ya miezi mitatu bila kufanikiwa walichopanga na bado wapuuzi kadhaa wanawaona eti ni wanajua vita.
4. Hakuna mzungu aliyesema kwa uhakika kwamba 2likua nyani. Inaitwa Theory, unajua maana ya theory ww? Leo ukisema bunadam 2mejengwa na tofali na ukatoa viashiria na vikashawishi wataalamu wataiongeza nayo iwe Theory...theory inabaki theory hadi ipingwe kwa evidence na mtu mwingine na hyo evidence ikubaliwe na wataalam.
Wazungu kuna wanaoamin nyani, wengine Mungu aliumba, wengine wanapinga zote kama wewe, na hamna anayekulazimisha uamin hv au vile
Uliza maswali ukiwa unajua nn unasema
4. Hii kwa namna fulan umeandika kinachoeleweka. Na kwa vile mimi sio mnafiki basi kwenye namba 4 sina cha kuongeza.
Mengine nakushukuru kwa kunirahishia kazi ya kile nilichoandika kule juu, yani kifupi na wewe umeiimarisha hoja yangu, na kukazia yale yale niliyoandika bila wewe mwenyewe kujua.