Huwa mnachekesha sana, yaani kila siku tunayashuhudia tangu vita vinaanza leo unasema uletewe uthibitisho, sijui kwanini huwa mumeshikiliwa akili kijinga hivi.
Kijana, dunia ya leo mtu hauminiwi kwa maneno matupu. Weka fact unazosema unaziona ili tujithibitishie na sisi.
Hauwezi kuniambia kuwa umeona kitu fulan, alafu mimi ambae sijakiona nakubali tu eti na mimi nimekiona.
Huu ndio mwisho wa kulishana matango pori. Jeshi kubwa linaongezewa msaada wa kijeshi, linaita hadi askari wa akiba, mamluki wanaodanganya kuwa wameenda kusomea mashamba, pamoja na wale askari waliostaafu ili kupambana na vijana wasiozidi elf 20 ambao hawana hata kifaru kimoja cha vita!
Nilitegemea kwa vile Gaza ni ndogo na Hamas hawazidi elf 20, basi Israel ingekadiria vijana wake kadhaa na silaha kadhaa kulingana na udogo wa Hamas na eneo wakawamalize na kurudi kuendelea na maisha huku nchi ikiendelea na mipango mingine.
Lakini sasa tunachokiona ni nchi nzima, serikali nzima, jeshi zima hadi askari wa akiba wameingia vitani na nguvu zote kama vile wanapambana na nchi nyingine ambayo ina silaha nzito kama zao, kumbe wanaenda kupambana na vijana wachache waliopo katika kaeneo kadogo tu wanakokakalia na bado wameshindwa, je tukiwapa mission ya kuja kuwatoa M23 wenye dhana bora za kijeshi katika misitu wasioifahamu bila back up ya Marekani wataweza kweli?
Hapo sizungumzii Iran ambayo inatumia vijana wadogo tu kulisumbua taifa zima na vibaraka wao Marekani na EU, tena kumbuka hiyo Iran inaongoza kwa kuwekewa vikwazo vikali na vya muda mrefu zaidi duniani, lakini bado inasumbua nchi isiyowekewa vikwazo, inayopokea misada ya kijeshi kila mwaka kutoka Marekani, na ambayo imekuwa ikiruhusiwa kutengeneza silaha ipendavyo.
Je kama isingekuwa inapewa misaada ya kijehi, na Iran kuwekewa vikwazo hali ingekuaje Mashariki ya kati?