Kuanza leo usiku mpaka Nov ndio tutajua kama nchi hii nayo ina Deep State au namna gani?

Umenena ukweli mtupu, huwa mi nashangaa sana pale watu wanapodhani kwamba nchi yetu ina espionage ya hali ya juu sana, ni kwamba nchi yetu bado sana sana ndiyo maana Kuna mambo mengi ya kifisadi yanaendelea
 
Mama si mchezo....ukijichanganya umepotea mazima!!!!!
 
Nimeona jinsi Dodoma ilivyotengenezwa kwa ajili yao wengi wapo kule na mahekalu ya maana.

Siku zijazo Dodoma itakuwa yatawaliwa na wale elites tu security organs na vyombo vingine nyeti.

CCM itashinda uchaguzi ujao lakini ukweli wabakia kuwa palepale, hautakuwa uchaguzi huru na wa haki bali ni kwa maslahi ya wachache.
 
Umenena ukweli mtupu, huwa mi nashangaa sana pale watu wanapodhani kwamba nchi yetu ina espionage ya hali ya juu sana, ni kwamba nchi yetu bado sana sana ndiyo maana Kuna mambo mengi ya kifisadi yanaendelea
Mkuu, Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye "espionage" ya hali ya juu barani Afrika.

Isipokuwa kama aelezavyo DeepPond mazee wametulizwa na watunzwa na kutuzwa vema.

Lakini "Espionage" ipo "intact" palepale.
 
Ukizungumzia "Uchaguzi huru na haki" tambua Hilo sio MIONGONI mwa "maslahi ya taifa" . USIJITIE MGUMU KUELEWA
Wengi wachanganya sana maana halisi ya neno Maslahi ya Taifa. Pia kuna maslahi ya Umma.

Zamani tulikuwa mara wasikia RTD kuna meneja au mkurugenzi fulani ameachishwa kazi kwa manufaa/maslahi ya umma.

Serikali ya Mwalimu Nyerere wakati huo ilichukua njia hiyo ya kutangaza mtu kafukuzwa kazi ili kutisha kuwa ukichezea madaraka na ofisi ya umma basi weye kazi huna.

Nchi zingine khasa zile ziliondelea hawana simile na ofisi za umma, ukichezea tu basi kazi huna na husema ni kwa maslahi ya umma (public interest) ama umetumia fedha za walipa kodi vibaya au hata kufanya ngono ofisini.

Sasa turudi kwenye neno maslahi ya taifa nini maana yake?

Kwa mujibu wa mwandishi wa sayansi ya siasa wa Marekani Hans Morgenthau, maana ya maslahi ya taifa ni pale utaifa kwenye siasa, tamaduni na nchi kama nchi yanapolindwa dhidi ya uvamizi kutoka mataifa mengine, na endapo hapa patapotoshwa basi hakuna masuala kama uchaguzi huru na wa haki.

Na katika kitabu chake kingine kiitwacho "The Six Political Principals of Realism", pointi namba sita, huyu bwana asema hivi,

"Political realism is aware of the tension between the moral command and the requirements of successful political action."

Sasa hiyo "Moral Command" ndo yaweza kumsumbua alie madarakani kwani mahitaji yake ya kuendelea kushika madaraka yaenda sambamba na hatua kadhaa za kuhakikisha haondoki madarakani, ambayo ndo hiyo "requirement of successful political action" nadhani wanipata hapo.

Hivyo twaweza kuangalia yalotokea hadi TL yupo Ukonga ni katika hayo ya kuhakikisha alie kwenye kiti aendeelea kuketi hapo bila hofu ya kuondoka kwani wale wanomzunguka ni katika haohao DS, mfumo wa Kleptokrasia na wengine wa Ad-Hoc.

Kwa maana hio basi, DEEP STATE yaweza kabisa kuwepo katika nchi kama ya kwetu lakini mfumo wake na utendaji wake wa kazi vyaweza kuwa twaita kwa kiingereza "Hybrid" yaani mfano wa gari inotumia jiwe la umeme lakini hapohapo laweza kutumia mafuta kama petroli au diesel.
 
Ukingia mtandaoni unaweza zani nchi IPO kwenye taharukii,,afu ukiwa KITAA mambo ni normal watu wanakula konyag na kupiga mishe hawana mpango na no reform wala kutiki
Sure indeed 😁
 
Nakuelewa sana
 
😁😁😁😁🙌
 
😁😁😁😁

Hapa ni sawa na kusema kwamba wana tufanyia divide and rule , Yaani wao kazi Yao ni kupiga Ngoma tu ili sisi tuicheze
 
Nakuelewa sana mkuu. Tumelishwa matango pori kuwa Marekani inaendeshwa kwa kuzingatia Democracy kumbe ni corporate oligarchy.
Ukitazama Kwa kina hiyo democracy haipo that's why wao pia wamesha waumiza watu wengi sana waliokuwa wanaipinga system Refer -- kifo Cha Malcom x And the likes

Hakunaga democracy Duniani maana binaadamu ni kama kiumbe wengine sote tuna tawaliwa na tamaa iliyovuka mipaka
 
Kuna UDOKOZI, WIZI NA UJAMBAZI. Ni kweli free election haipo ulimwengunu na hili ni sababu ya imperfection by nature za Wanadamu.Mifumo yote ina limitations - sababu ya ubinadamu.

Lkn tunatofautiana kati ya nchi na nchi, kuna wanajitahidi licha ya changamoto, nguvu ya watu na majority unaiona.
KUNA NCHI ZINA UDOKOZI KWENYE ELECTION,ZINGINE ZINA WIZI,ZINGINE ZINA UJAMBAZI.
SISI MIFUMO YETU NI MAJAMBAZI YA UCHAGUZI.
Wewe kilichotokea mwaka jana uchaguzi wa Serikali za mitaa ulikiona???Hizo ni ishara za waziwazi tusivyokua na viongozi wenye maslahi na taifa.

KUNA DEEP STATE INAYOLINDA MASLAHI YA WATAWALA NA KUWAHAKIKISHIA USALAMA WAO ILI WAENDELEE KUTUPIGA.
KUANZIA deep state, polisi, usalama, jeshi kote ni hovyo.
HAIWEZEKANI MAMBO YANATOKEA YA HOVYO HATUONI MSAADA WA VYOMBO.
 
Mkuu we juchanganye tu kwamba jf ni anonymous ?
We endelea tu ujichanganya mwenzako Titicomb anakili hapo kwamba alipewa warning ⚠️ Kwa kutumia majina anayotumia humu

Kimsingi humu haiwezekani tukawa anonymous kwakua siku wakiwa na SHIDA na wewe hakuna ambacho hawata kijua kukuhusu
 
Nafahamu maana ya Deep State.
 
safari ya kuyafikia mabadiliko kwa njia tunayoitaka (demokrasia ) bado sana
 
Hakika mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…