Kukosa mtoto wa kiume inawasumbua sana wanaume kufanya wakose amani

Kukosa mtoto wa kiume inawasumbua sana wanaume kufanya wakose amani

Kiasili watu wengi huwa wanapenda kuwa na watoto wa kiume, hili halijalishi mzazi wa kike au wa kiume. Huu ndiyo ukweli.

Ila asikwambie mtu mtoto ni mtoto, cha msingi mzazi uwalee vyema hasa kwa malezi ya dini, hutakuja kujutia, sababu mtoto mwema anafaida na wewe ukiwa hai na hata ukifa. Sasa ni wajibu baba au mama kuangalia wapi pa kupanda mbegu zako.

Kwa imani yetu sisi ni kuwa ukijaaliwa watoto wa kike kisha ukawalea vizuri kwa malezi bora na tabia njema yaani dini, mpaka wa kaolewa wewe utalipwa Pepo. Hapa utaona fadhila na ubora wa kuwa na watoto wa kike.

Mola atupe vizazi vyema na vyenye kheri na sisi.
 
HAPANA, familia nyingi ukiona mtoto wa kiume kasahau kwao bhasi angalia huduma inayopelekewa familia ya mke wake. Usishangae hata hao watoto wa kike wanaosifiwa utakuta wanapush waume zao wapeleke huduma kwao na sio alipozaliwa mwanaume. Ni familia nyingi tu utakuta ndugu wa mke wanajiachia for years ila wa mume akikaa hata wiki mbili tayari anatamani kuondoka ndio maana watu wengi hujihisi comfortable kuishi kwa dada na sio kaka

Kama umezaa watoto wa kiume wengi trust Me, huwezi kukosa yule atakaeijua thamani yako kwa asilimia zote lakini kubwa kuliko waombee wapate wake watakaokuwa wanawapush kukumbuka. Ila ukipata watakaokuita mnoko au mchawi, hasara ni yako
Umesema kweli ila penye hasara hapo ndo pakubwa na wengi tu wameila na mie huenda nikawa miongoni mwao,😂
 
ukweli usemwe mwanaume kizazi chake huendelezwa na mtoto wa kiume....mtoto wa kike huendeleza kizazi cha mume wake....
 
Mtoto wa watu umkute amesomeshwa wewe uje kusema unamiliki mtoto na mzazi wake. Huu ni utomvu wa adabu.
Matokeo ya kutokuwa na mtoto wa kiume kwenye familia yako....kubali uzeeni kwako ukalelewe ukweni....na ni udhaifu mkubwa....na hapo kale kamsemo ketu ka kujifariji kuwa watoto wote ni sawa huwa kana poteana.....
 
Umesema kweli ila penye hasara hapo ndo pakubwa na wengi tu wameila na mie huenda nikawa miongoni mwao,😂
🤣🤣🤣 utafanyaje sasa au ndio unatafuta kakike kwa nguvu. Ila ukitazama kabisa kiundani

mtoto toka akiwa mdogo unaiona tabia yake, sasa muangalie yule anaekupenda sana au ana huruma sana na wewe bila choyo

Ukimpata, kamtolee sala na sadaka ya mwanamke na kizazi chake kwa mwamposa 🤣
 
Mungu asikie kilio changu sio siri, nimpate mrembo na mimi loh!

Wapo watoto wa kiume wanaofanya vizuri kuzidi wa kike, nakumbuka baba yangu alimuuguza mama yake(bibi) ilifikia hatua, anamuamsha anamkalisha anajisaidia anamnawisha anamvisha na kumbeba kumrudisha kitandani,, nilikuwa mdogo wakati huo lkn nikikumbuka nasisimkwa na si kwamba bibi hakuwa na watoto wengine ama wa kike hawakuwepo ila ni baba tena kitinda mimba wake ndiye alikuwa akifanya hayo😥
 
ukweli usemwe mwanaume kizazi chake huendelezwa na mtoto wa kiume....mtoto wa kike huendeleza kizazi cha mume wake....
Kati ya mtoto wa dada na wa kaka kibaolojia nani ni ndugu yako? watoto wa kiume tuna risk kubwa ya kubebeshwa watoto ambao sio wetu kwa kiasi kikubwa, unasema unaendeleza ukoo kumbe mtoto puga 2,
 
Mungu asikie kilio changu sio siri, nimpate mrembo na mimi loh!

Wapo watoto wa kiume wanaofanya vizuri kuzidi wa kike, nakumbuka baba yangu alimuuguza mama yake(bibi) ilifikia hatua, anamuamsha anamkalisha anajisaidia anamnawisha anamvisha na kumbeba kumrudisha kitandani,, nilikuwa mdogo wakati huo lkn nikikumbuka nasisimkwa na si kwamba bibi hakuwa na watoto wengine ama wa kike hawakuwepo ila ni baba tena kitinda mimba wake ndiye alikuwa akifanya hayo😥
Yeah ni familia nyingi tu watoto wa kike hawatimizi majukumu yao. Hivyo ni kumuomba Mungu tu akujaalke mtoto atakaekuwa na huruma juu yako
 
Yeah ni familia nyingi tu watoto wa kike hawatimizi majukumu yao. Hivyo ni kumuomba Mungu tu akujaalke mtoto atakaekuwa na huruma juu yako
Tuseme Amina,🙏🙏
 
Dah! Mmenikumbusha Dada yule anayelia kila kukicha ametelekezwa na mmewe hii ni baada kujaliwa watoto wakike tu watano mpaka sasa.

Swali: Hivi kwenye kutafuta jinsia ya mtoto wa kuzaliwa kuna upande unapaswaa kulaumiwa kwa kuikosa jinsia Fulani ya mtoto??
 
hata wewe na ukubwa huo unaweza ukaingiwa na tamaa ukachenji gia angani, ukawa kama hao "mashoga" zako wawili uliowataja. karibu sana ndg.
Hatushindani mkuu ila nakushauri tu mzee. Ombea sana watoto wako mkuu na uwalee vizuri.
 
Mtoto ni mtoto ndiyo, lakini bado najiuliza mbona kwenye biblia ukisoma sijui uzao wa Isack, Yakobo, Yoseph nk. Unaona wakibarikiwa mzao wa kwanza, pili... Wote wa kiume. Na Kama Mwenyezi Mungu alimuahidi mtu mtoto basi alikuwa wa kiume! Kuna kitu hapo
 
pamoja na ugangwe wangu wote, nilitoa machozi ya furaha ile siku nilipopewa taarifa kwamba shemeji/wifi yenu kanizalia salama mtoto wa kiume.

that feeling is something i can't explain, wababa wenzangu waliobahatika kupata watoto wa kiume wanajua nazungumza nini.

kwa sasa jembe langu yupo standard two halafu he is a real version of me copy and paste. mdogo wake aliyemfatia pia na yeye ni kidume, sura kama kaka yake utadhani mapacha.
Basi omba Mungu isije ikatokea siku moja akakuambia kapata mchumba, kwa furaha unamwambia amlete umwone akakuletea bonge la kidume rijali... mindevu kama yote, abs za kueleweka .... ndio utasema bora ile siku ningevaa condom au ningepiga punyeto

Mambo mengine bora tukae kimya na kumshukuru Mungu kwa maamuzi yake.

Mtoto ni mtoto tu. Kuna wengine wanamtafuta hata huyo wa kike na wanamkosa. Wengine wanalea watoto kwa kujishaua kumbe mama ndio anajua mtoto ni wa nani....
 
Mtoto ni mtoto ndiyo, lakini bado najiuliza mbona kwenye biblia ukisoma sijui uzao wa Isack, Yakobo, Yoseph nk. Unaona wakibarikiwa mzao wa kwanza, pili... Wote wa kiume. Na Kama Mwenyezi Mungu alimuahidi mtu mtoto basi alikuwa wa kiume! Kuna kitu hapo
Ni wanawake wachache wameandikwa kwenye Bible, zamani hesabu ilifanyika kwa wanaume tu.
 
Bwana Mchanga alipata nafasi ya kwenda masomoni nchi za Scandinavia, alibahatika kupata mke wa Kizungu na baraka ya mabinti watatu. Baada ya masomo Mrs Mchanga alikataa kurudi Tanzania. Waliachana kwa amani na bwana Mchanga kurejea nyumbani.

Alipata ajira serikalini kama afisa mwandamizi. Alikutana na Ruth na wakafunga ndoa. Ruth alipata mtoto wa kike, Mchanga alikua mvumilivu, wapili akaja binti mrembo. Hapa Bwana Mchanga uvumilivu ulimwishia. Alikwenda kijijini kwao na kuoa kabinti kigori kabisa. Kwakua uwezo wa fedha alikua nao alimjengea nyumba nzuri pale kijijini.

Huku kwa Ruth alimuacha akiwa mja mzito na alijaliwa kupata mtoto wa kiume. Ruth hakua na habari kuwa mume wake ana mke kijijini. Kila weekend Mchanga alikwenda kijijini akidai anajiandaa kugombea Ubunge. Ruth slipata habari mume wake ana mke mwingine yeye akiwa na mtoto wa pili wa kiume.

Huyu mke wa kijijini alianzisha leagu na Ruth, Ruth akiwa career woman hakuwa na muda huo, aliachana na Mchanga na kugaiwa mali zake. Maisha yanaendelea na watoto wakakua.

Mchanga akianza familia mpya kijijini. Umri nao unasogea. Sasa Mchanga anastaafu akiwa na watoto wanasoma shule ya msingi. Wale mabinti wa Scandinavia wameolewa na wameanza familia.

Katika jitihada za kutafuta mtoto wa kiume sasa Mchanga anatumia mafao ya kustaafu kulea watoto.
Waje na wake zao niwape mbegu za giant
 
Ni wanawake wachache wameandikwa kwenye Bible, zamani hesabu ilifanyika kwa wanaume tu.
Naam!!! Na ile ya Yesu kuwa na wanafunzi kumi na wawili unaionaje? kiukweli mtoto wa kiume ikiwezekana tumwombe Mwenyezi Mungu awepo kwenye familia.
 
Nikiangalia navyohangaika na home kwetu, pamoja na ndugu zangu,,sio siri naona kabisa mtoto wa kike Ni muhimu Sana kwenye familia kuliko hao wa kiume, wanawake hatubebi majina ya koo zetu ila hatusahau makwetu hasa wazazi, tofauti kabisa na wa kiume akipata familia kwao ndio hata hawafikilii kabisaa

Nikiangalia hapa nimejaza madume tu naiwaza hasara nitakayopata miaka ijayo nakosa nguvu kabisa[emoji26],
Usiseme hivyo mkuu
 
Back
Top Bottom