Kwanini baadhi ya "wanajeshi" wetu wana vitambi?

Kwanini baadhi ya "wanajeshi" wetu wana vitambi?

Ningekuwa mimi ndo amiri jeshi Mkuu, hayo yote yenye vitambi ningeya-demote au kuyashusha vyeo. Kwa askari/mwanajeshi kuwa na kitambi ni kukosa nidhamu.
 
iu
Huyu amemeza kabisa wahalifu...
 
Hicho kitambi mnacho sema...kwenye mambo yetu yale...huwa kinarudi nyuma na kuwa kibiongo...huku show ikiendelea mujarabu...
 
Walengwa hapa ni JWTZ, POLISI, JKT, Magereza na Zimamoto!

Wengi wa askari wenye vitambi ni "mabosi'

Vitambi kwa askari wa vyeo vya juu vina manufaa gani kwao na kwa Taifa?

Wanajua kuwa hivyo vitambi vinatusababisha "sisi" tusio na uzoefu wa masuala ya Kijeshi tuwaone kuwa ni wazembe? Mbona wenzao wa China, North Korea , na Rwanda hawana vitambi?

Wanajua kuwa wao ni mfano wa askari wa chini? Kwa kuwa wanasema "like the son, like the father", watajisikiaje siku moja wakigundua kuwa askari wote wanaowaongoza nao wan vitambi kama wao?

Hivi kukitokea dharura itakayowalazimu kukimbia kwa masaa matatu mfululizo si wanaweza wakahisi ulimi unataka kutoka?

Kwa nini "wanajeshi" wetu, japo siyo wote, wana vitambi?
Picha tafadhali
 
Sio wanajeshi tu. Mwanaume yeyote kuwa na kitambi ni upumbavu na kutokuwa smart.

Watu smart kichwani hawafugi matumbo.

Ukiondoa wachache ambao ni kutokana na changamoto za ugonjwa, waliobaki ni kutokana na ulafi wa
kulakula hovyo bila kuwa na kiasi lakini pia uvivi wa kufanya mazoezi
Kama kuna ka Ukweli hapa
 
Hata Amiri Jeshi Mkuu ashaliona hilo
 
Attachments

  • RAIS_SAMIA_AWAGEUKIA_ASKARI_WENYE_VITAMBI_-___NIMEVIONA_VITAMBI,_WARUDI_WATOE_VITAMBI_WAWE_WEP...mp4
    4.6 MB
Walengwa hapa ni JWTZ, POLISI, JKT, Magereza na Zimamoto!

Wengi wa askari wenye vitambi ni "mabosi'

Vitambi kwa askari wa vyeo vya juu vina manufaa gani kwao na kwa Taifa?

Wanajua kuwa hivyo vitambi vinatusababisha "sisi" tusio na uzoefu wa masuala ya Kijeshi tuwaone kuwa ni wazembe? Mbona wenzao wa China, North Korea , na Rwanda hawana vitambi?

Wanajua kuwa wao ni mfano wa askari wa chini? Kwa kuwa wanasema "like the son, like the father", watajisikiaje siku moja wakigundua kuwa askari wote wanaowaongoza nao wan vitambi kama wao?

Hivi kukitokea dharura itakayowalazimu kukimbia kwa masaa matatu mfululizo si wanaweza wakahisi ulimi unataka kutoka?

Kwa nini "wanajeshi" wetu, japo siyo wote, wana vitambi?
nachukia sana kitambi
 
Nadhani askari yeyote mwenye kitambi ni matokeo ya uvivu. Uniform za majeshi yetu pia zibadilishwe. Hawa wenzetu wanapendezeshwa na nini? Mavazi? Urefu? wembamba?... au wanahenya muda wote? 😳 View attachment 2890251
Nimejaribu kuwaangalia kwa makini lakini sijamwona mwenye tumbo kubwa.

Au hawali vizuri?
 
Matokeo ya ulaji mbovu na kubweteka.
Tafsiri yako yaweza kuwa ni sawa, lakini wanabwetekaje wakati kwenye majeshi michezo pamoja na training ni lazima bila kujali cheo?

Tunakutana nao mabarabarani wakifanya collective sports nadhani kila siku za jumanne na ijumaa!

Kunenepeana kwenye majeshi hakutokani na kubweteka bali kunatokana na kuubwaga moyo(kuridhika).

Hakuna cheo unaweza enjoy kama cheo cha jeshi.

Unapokuwa na cheo chenye mamlaka na namna sheria za jeshi zilivyo, asiyeweza kunenepa ni yule mwenye mwili asili ya Obama.

Maana yake ni kwamba, ukiwa na cheo chenye mamlaka, chochote utakachokisema lazima mtu unayemzidi cheo aitikie kwa unyenyekevu mkubwa na usiotia shaka, tena haitikii kupokea maagizo huku akitembea, huitikia huku yuko attention kwa umakini wa kutekeleza unachomuagiza!

Mambo yote mema lazima kwanza wewe uyapate ndiyo yashuke kwa wengine na unachokiagiza ama unachokitaka lazima kitekelezwe, staff wa chini yako wanakutii kuliko ambavyo mkeo ama watoto wako wanavyokutii.

Hapo kwa nini mtu asinenepe?
 
Back
Top Bottom