Kwanini siku hizi vijana wengi mnamchukia Mungu, mmegombana nae?

Hayo matendo yanaendana na maandiko?
 
Mpaka sasa huwezi kujua kama na support au la
Hio ni topic nyingine haihusu uwepo wa Mungu
Wewe unazunguka nimekuuliza swali dogo Ila unazunguka mno, jibu moja ndio au hapana, maana Kiranga alisema ndio anasupport maana haoni uwepo wa Mungu wewe vipi huoni uwepo wa Mungu una-support ushoga na usagaji ?
 
Lakini kweli tukiangalia wanaoenda kanisani au wanaomuamini Mungu Maisha Yao ni tofauti kabisa wasioamini au wasio enda kanisani unakuta wanamaisha mazuri Zaid sa sijui tatizo Ni nini au Imani Haba by the way mi amini uwepo Wa Mungu na nguvu zake ni muumini mzuri tu Wa kilokole church mara Kwa mara sitting ya nyuma kule
 
Mungu ametuagiza tusamehe 7 mara 70, ila yeye kashindwa kumsamehe shetani. Ufafanuzi wa hili sijui ukoje.

Mungu alisema kuua ni dhambi lakini kwenye vitabu vya dini mara kadhaa Mungu ameua wale waliomchukiza.
Shetani aligoma kuomba msamaha.
MUNGU aliwafuta waovu waliokataa kutii baada ya kuwapa mda wa kutubu ikiwemo kuwapelekea wajumbe wakawagomea na kuwaua.
Ndivyo atakavyofuta hiki kizazi kiovu na kuleta kipya.
Huwa Mungu anaifuta Dunia kwa kuweka kizazi kingine kila baad ya mda fulani
 
Noted ✍️
 
Huyo anakuwa ajakomaa kiroho,aliyekomaa kiroho anao uwezo wa kuishinda dhambi.
Ngono sio basic needs,pia mwili unayo namna yake ya kujibalance
 
Waambie wathibitishe hoja yao ya kwamba Mungu hayupo.
Theist wanataka "Atheist" wathibitishe Mungu hayupo na wenyewe Hawawezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kama wewe una amini Mungu yupo na huwezi kuthibitisha uwepo wake,

Na Atheist ni hivyo hivyo Hawa amini uwepo wa Mungu na hawa wezi kuthibitisha kutokuwepo kwake.

Kila mtu abaki na aheshimu imani na mtazamo wa mwenzake.

Ukiita Atheist wana utindio wa ubongo na wewe mwenyewe wakati huo huo Huwezi kuthibitisha uwepo wa Mungu ni sawa na kurukwa Akili

Unataka proofs na wewe mwenyewe huwezi kutoa proofs...
 
Kuendelea kumkataa Mungu, ni moja ya dalili kubwa saana ya udhihirisho wa Mungu na utimilifu wa unabii ktk zama hizi za mwisho.
 
Angekuwa hayupo tusingewapinga hao wenye mtindio wa ubongo.
Tunawaita Wana mtindio sababu maandiko yanasema Wana mtindio wa ubongo.
Zipo bilions reasons za kuthibitisha uwepo wa Mungu
 
Aahaaaaa
 
Angekuwa hayupo tusingewapinga hao wenye mtindio wa ubongo.
Tunawaita Wana mtindio sababu maandiko yanasema Wana mtindio wa ubongo.
Zipo bilions reasons za kuthibitisha uwepo wa Mungu
Leta hizo Billions reasons za kuthibitisha uwepo wa Mungu tuzi chambue.

Unajua Theist Hawawezi kujenga hoja Hamuwezi kufikiria nje ya imani yenu.

Ubongo wenu upo programmed na maandiko ya kidini kama roboti.

Hamuwezi kujenga hoja nje ya hapo.

Maandiko ya kidini ni Rimoti ya kuwa control msihoji chochote zaidi ya kuamini.
 
Lete hoja kuhusu
. Chanzo cha uhai,
.Kwann viumbe vinazeekaa na kufa
.Kwann ukikiuka kanuni za asili ni lazima zikurudi
.Kwann ukikosa oxygen lazima ufe
.
 
Kinyume chake pia, watu wanaoamini bila kufikiria wameongezeka.
Mtu kama Masanja anapiga hela kupitia ujinga wetu
kuna jamaa alikuwa anaigiza kama mchungaji, siku hizi amekuwa mchungaji ana kanisa lake hapo jijijni
watu wanaamini blindly
 
Ni kila baada ya muda gani?? Kwanini Mungu mkamilifu anatengeneza vitu asivyoweza kuvi control/visivyovikamilifu? Anatengeneza viumbe na kuvipa uwezo wa kukosea alafu vikikosea ana viadhibu?? Kama kazi ya mungu ni kutengeneza kizazi then kikikosea anafuta analeta kingine inamaanisha bado yupo kwenye majaribio ya kuleta kizazi kikamilifu??
 
mkuu dini ni dhana ya zamani na tunapoelekea dini zitatoweka kabisa..... sayansi na teknolojia vinazidi kukua kwa kasi. Mambo ambayo yangeonekana uchawi zamani kama usafiri wa anga, sasa ni vitu vya kawaida sana....
 
Dini kupitia vitabu,hasa ukristo kwenye biblia inatoa majibu ambayo hayapatikani popote.
inatuambia kuhusu chanzo cha uhai, na kifo na pia jinsi ya itakavyokuwa baada ya kifo
biblia iliandika vitu vikatokea na vipo vinaendelea kutokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…