Jitenge nae ili usijue matatizo yake!
Nani kati ya mawaziri aliyekuwa na maisha duni ili aujue mchungu wa maisha ya wananchi.
Wafanye masikini wa kutosha ili uweze kuwatawala.
Mdomdogo serikali inachukua hata kile kidogo walichonacho wananchi ili wawe tegemezi kwa serikali.
Mshahara kiduchu, waajiriwa wanalia leo unawaletea shida nyingine.
Tutegemee ufanisi mdogo kwa wafanyakazi wenye mishahara midogo.
Nauli za mijini huu ni mwiba mkubwa sana.

Tusubili tuone!
 
Hii table imeandikwa ovyo ovyo sana. Angalia hapo Dodoma kwenda Iringa kupitia Mtera. Waiandike upya, waache ubabaishaji.
 
Hizo nauli hazitumiki Mkoa wa Mbeya,Sisi Mbeya dereva na kondakta ndo huamua nauli ziweje😁😁!
Nimepanda daladala nanenane nashukia Simike nauli ni tsh 1500!!

MBEYA HAYA HAYATUHUSU!NAULI ZILIPANDA MARADUFU HATA KABLA YA TANGAZO HILI.
MBEYA HAKUNA LATRA
 
Wanajamvi

LATRA imepandisha bei ya nauli ya mabasi na daladala wanasema ni kutokana na gharama za uendeshaji na bei ya mafuta kupanda hivyo basi wakakaa na wadau wa vyombo hivyo vya usafiri na kukubaliana upandaji huo wa nauli.

SWALI

1. Kwanini upandaji wa nauli unahusisha LATRA na wadau wa usafiri tu na kuwaacha abiria ambao ndio walaji na wahusika wakuu?

2. Tumeshuhudia mara nyingi LATRA wanapandisha bei ya nauli kila mara inapotokea mafuta yamepanda LAKINI huwezi kuwasikia wakishusha bei ya nauli inapotokea mafuta yameshuka bei.

LATRA tunaomba majibu au kama kuna mtu anaweza kueleza hili atujuze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…