Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Chadema mnaomba kupewa jengo moja la CCM mlifanye Ofisi?
 
Kwani Chadema inashindwa nini kuhamasisha wananchi wawajengee Ofisi ya Chama?
 
Wanawanyanganya maeneo ya wale ambao ni wapinzani tu....

Ova
 
Kwani Chadema inashindwa nini kuhamasisha wananchi wawajengee Ofisi ya Chama?
Mbona watu tunawajua marais wastaafu na coincidí wengine wa ccm wana maeneo makubwa na hayaendelezi kabisa na hamwagusi,Ila mtu akiwa mpinzani wa serikali tu basi ni shida Lazima anyanganywe malí zake

Ova
 
Tafadhari alie na ushahidi wa kiwanja ama mradi wowote mkubwa uliojengwa kwa nguvu ya wana ccm baada ya vyama vingi kuanza,na kama hakuna uwezo huo mliupoteza lini na kwa sababu gani?
Nyanyueni macho tizameni hapo kenya nini kilitokea baada ya kanu kuondolewa madarakani kumbukeni hata KICC ilikuwa mali ya kanu
 
Kwani Chadema inashindwa nini kuhamasisha wananchi wawajengee Ofisi ya Chama?

Huu ni udhaifu wa wazi wa cdm hata wao wanaufahamu. Kwa bahati mbaya mimi sio mwanachama wa cdm bali ni mshabiki tena wa kutupwa. Hivyo nafasi yangu ni hapa hapa jukwaani na sehemu nyingine ambapo cdm hushirikisha wanachama, washabiki na wapenzi wake. Ila hili la ofisi nimewahi kuhoji zaidi ya mara moja, haswa huyo Lowasa alipojiunga na kugoma kwenda hapo ofisini kufanyia vikao vya chama kisa hakuna hadhi yake. Nilisema iwapo kweli Lowassa ana mapenzi na chama na sio kutumia ukubwa na umaarufu wa chama kujipatia madaraka, basi naye mchango wake ajenge ofisi yenye hadhi ya cdm kwani amekuwa akitoa michango ya ujenzi kwenye nyumba za ibada. Sikuishia hapo nilihoji pia ibunifu wa katibu mkuu wa chama alipoingia kuhusu ofisi inayoendana na hadhi ya chama kwani hii ni aibu kwa sisi tunaojali nyumba/ofisi zenye hadhi.
 
Naunga mkono hoja.
Kwa Uamuzi Huu, Pongezi Sana Rais Wetu Magufuli, Utabarikiwa na ...

P.
 
Nikuulize chadema ilinunua lini magari kwa jasho lao zaidi ya kutumia pesa za ruzuku za walipa kodi? Rudisheni magari serikalini mabwege nyie

Hapa una hoja kuhusu cdm hata wao wanaona hii imekaa vibaya kwa upande wao. Ila naona unachanganya hoja, hoja ni umiliki wa mali zilizopatikana kabla ya mfumo wa vyama vingi. Je huko nyuma ccm ilizipata mali hizo kama ruzuku ya chama au ilikuwa ni miradi ya umma iliyoratibiwa na chama? Nakumbuka miradi hiyo mingi ilipatikana kwa michango ya hiari na sanasana kwa lazima aidha fedha au nguvukazi. Na michango hiyo iliwahusu wote bila kujali ni mwanaccm au sio mwanaccm. Hapa ndio utata ulipo.
 
Hivi unamtetea vipi mtu mwenye ekari 300 eti ni mpinzani? Vp kuhusu Manji naye ni mpinzani? Wakati mwingine mnatupa hofu sana kuwapeleka ikulu mtatuuza mpaka raia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Huyo anayemiliki hiyo heka 300 hakuanza kuimiliki jana, kaanza miaka na miaka na sio yeye tu, hata hao viongozi wengine aliokuwa nao ccm mpaka leo wanamiliki hivyohivyo lakini nchi haijauzwa bado. Kwasababu hiyo tunaona ni siasa chafu tu, japo naye Sumaye hatumtetei kihivyo kwani naye alipokuwa ccm aliona ni sawa wapinzani kufanyiwa hivyo.
 
Tukipata Rais KM wewe Mahanju TUta kuunga mkono Kuya taifisha Hayo Maeneo yetu ina tuuma sana mengi tunaya jua na Tulishrikishwa kwa hali na Mali
 
Hivi unamtetea vipi mtu mwenye ekari 300 eti ni mpinzani? Vp kuhusu Manji naye ni mpinzani? Wakati mwingine mnatupa hofu sana kuwapeleka ikulu mtatuuza mpaka raia.

Sent using Jamii Forums mobile app
MAMBO ya manji wanajuana huko huko ccm,kuhusu maeneo kupigwa bado Kuna coincidí wengi wanayo na hawajaendeleza
Kila Siku anayeporwa ni sumaye tu na mbowe we hapo nyomi ni chuki za kisiasa

Ova
 
CCM Kama chama tawala pekee kilipewa ruzuku na serikali na kuchangiwa na Wafadhili wa Ndani na nje Wanachama Na wasio wanachama WA Ndani ya nchi na nje ya nchi kwa kippesa kimali na kiardhi Kama ambavyo mfumo wa vyama vingi chadema inachangiwa na serikali kwa ruzuku na kuchangiwa kimali kipesa na kiardhi na kimajengo na wanachadema na wasio chadema wa Ndani na nje ya nchi. Mleta hoja lofa na wanaounga mkono mabwege na malofa iwe chini ya mfumo wa chama kimoja au vingi.mleta hoja hoja zake za kibwege na kijinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…