Iko wazi, tuseme karibu ya Viwanja vyote vya michezo Tanzania vinamilikiwa na CCM, sina shida na hilo...
Shida yangu ni kutaka viwanja hivi vipewe serikali, kupitia halmashauri za wilaya hata ikiwezekana kwa ubia, CCM hawawezi kuviendeleza, srikali ikipewa itaviemdeleza.
CCM ndio inayoshika dola, maendeleo yetu kama nchi tunategemea kusimama na kutekelezeka kwa ilani ya CCM, CCM itoe hata kwa ubia viwanja hivi kwa serikali, vikarabatiwe na wote serikali na CCM watanufaika kwa mapato.
Tukivipata hivi viwanja na vikaboreshwa hata ligi yetu itakuwa ni bora sana, badala ya kujenga vipya vya serikali