Jana katika baraza la Idi Karimjee,Rais Magufuli alionyesha kuchukizwa na waislam walioshirikiana na matajiri kupora maeneo ya jumuia hiyo.Hilo lilikuwa chukizo zuri sana!Pamoja na kuwa Rais Magufuli sio mnafiki na anachukizwa na uporaji wa mali za jumuia za wananchi kwenda kwenye vikundi vya watu,nataka kumwambia kuwa kikundi kidogo kiitwacho CCM kilipora na kunyanganya viwanja vilivyojengwa na wananchi!Karibia mikoa yote Tanzania vipo viwanja vya michezo kama Mkwakwani-Tanga,Kambarage-Shinyanga,Al Hassan Mwinyi-Tabora,Kirumba-Mwanza,Jamhuri-Dodoma,nk vilijengwa na wananchi wote kipindi cha mfumo wa chama kimoja.Tofauti na ilivyokuwa kwa shule za mashirika ya dini kurejeshwa serikalini,viwanja hivyo vikaporwa na chama!!Je,Rais kama mlinzi wa mali za umma,ni lini atatoa tamko juu ya urejeshwaji wa viwanja hivyo?