Lissu angekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ingekuwa vizuri, Mbowe akae pembeni
Kama Magufuli aliweza kuwa mwenyekiti na rais wa Tanzania, hakuna chocolate Lisu atashindwa. Tofauti ya Magufuli na Lisu ni kuwa mmoja Yuko jehanamu, na mwingine Bado Yuko hai duniani. Lakini kitabia wako sawa kabisa. Sema unajua kwa misimamo mikali ya Lisu ni rahisi kuingiza nchi hii kwenye machafuko maana Hana Tabia za kikondoo, Wala busara za kujipendekeza.
Lisu ni mwanaharakati zaidi kuliko mwanasiasa.
 
Lisu ni mwanaharakati zaidi kuliko mwanasiasa.
Mwanasiasa ni yule anayekubali kufanyiwa uhuni na kutulia, ila mwanaharakati ni mwanasiasa mwenye misimamo mikali ama? Hebu nipe tafsiri ya mwanasiasa na mwanaharakati ili nione tofauti yake, isije ikawa ww ni wale bendera fuata upepo kwa maneno hayo.

Kumbuka Nyerere aliitwa mwanaharakati na wakoloni, same kwa Mandela wakati wa kupambana ubaguzi wa rangi. Huenda na ww umetekwa na propaganda hiyo hiyo.
 
Kina Pascal Mayalla wanasema siasa za confrontational politics zimewaumiza zaidi Chadema kuliko kuwasaidia kwani dola ilitumia mwanya huo kuwakandamiza.

Hivyo 'radical elements' kama kina Heche wataipata Chadema wakati mgumu kutoka vyombo vya dola, bora kina Mbowe anagalu wanaumwa ila Kuna mida wanapulizwa na kupakwa spirit.

JokaKuu zitto junior Kalamu brazaj

Hii ngoma inataka kwenda all out war. Nguvu zote ziwe consolidated. Hakuna kupoa.

F9hWDBUXcAAu_HR.jpeg

Kwenye ukombozi hakuna kupoa na haitakuwa rahisi.

Tuikatae mifarakano.

Kina Mwabukusi, Slaa, na wote walilodhamiria kutaka katiba mpya Sasa na kumwondosha CCM pasi na kuchelewa tena, wote hao ni wenzetu.
 
Bila kujali lengo lako mleta Uzi, ukweli ni kuwa kiongozi mzuri wa kuchaguliwa ni yule asiyezidisha miaka 10 kwenye nafasi Moja. Iwapo atazidisha miaka 10 kwenye nafasi Moja hasa ya juu kabisa ya taasisi ama nchi, lazima ataanza kutawala kwa mizengwe, na ubora wake utazidi kushuka.

Mifano ya viongozi waliokaa madarakani zaidi ya miaka 10 na kuishia kuharibu ubora wao, ama kuishia kutawala kwa mabavu, mizengwe nk ni:
  1. Nyerere
  2. Mugabe
  3. Moi
  4. Mobutu
  5. Gaddafi
  6. Hosni Mubarak
  7. Paul Biya
  8. Elbashir
Hao wote hapo juu waliishia kutawala kwa mizengwe, mabavu ama ubora wao kushuka baada ya kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Mbowe ni sehemu ya hiyo list hapo juu. Mbowe hakupaswa kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm baada ya kosa la kumpokea fisadi Lowassa na kumpa nafasi adhimu, huku Lowassa akiwa haamini katika falsa za Cdm. Kama aliona aibu kujihudhulu kwa kosa lile, hakupaswa kugombea tena uenyekiti kipindi kilichopita. Anachofanya sasa Mbowe ni kuharibu hata mazuri aliyofanya.
Mbowe akiwa mwenyekiti wa Chadema maisha yake yote sidhani kama kuna athari yoyote kwa taifa. Tatizo ninaloona mimi ni madhara ya utawala wa ccm na tanu kwa miaka 60 katika nchi hii.
 
Mbowe akiwa mwenyekiti wa Chadema maisha yake yote sidhani kama kuna athari yoyote kwa taifa. Tatizo ninaloona mimi ni madhara ya utawala wa ccm na tanu kwa miaka 60 katika nchi hii.
Maoni yako yanaheshimika na kuthaminiwa.
 
Kina Pascal Mayalla wanasema siasa za confrontational politics zimewaumiza zaidi Chadema kuliko kuwasaidia kwani dola ilitumia mwanya huo kuwakandamiza.

Hivyo 'radical elements' kama kina Heche wataipata Chadema wakati mgumu kutoka vyombo vya dola, bora kina Mbowe anagalu wanaumwa ila Kuna mida wanapulizwa na kupakwa spirit.

JokaKuu zitto junior Kalamu brazaj

..mimi naona Mbowe na Lissu wanafanya vizuri kama Mwenyekiti na Makamu wake.

..Chadema kuna uhuru wa mawazo na sio chama ambacho kinakwenda kwa kufuata haiba ya Mwenyekiti.
 
Binafsi naona Mbowe angeachia kijiti cha uenyekiti wa Chama ampe Lissu au Heche John

Nachotazama ni utendaji, sasahiv upinzani wanahitaji apatikane mtu mwenye misimamo mikali sana sio mtu mpole mpole kama Mbowe.

Chama kinahitaji watu kama Lissu au wengineo ndo waongoze Chama sio Mbowe

Mbowe sasa imetosha!! Mkabidhi mtu mwingine kijiti sasa!
Mkuu kimsboy, karibu uangalie hili ni bandiko la lini CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
Wanabodi,

Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja yenye impact ikiwemo kuyashika majiji makubwa katika mikoa the big five!, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga mkao wa kichama tawala, ili kikabidhiwe nchi, kitawale, Chadema bado kimekaa kichama harakati, hivyo kuna wengi wanakiona kama bado hakijakomaa kiasi cha kukabidhiwa ikulu yetu!.

Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu kwa sasa japo kipo juu, lakini bado hamjakomaa kufikia kiwango cha kukabidhiwa nchi, bado mko kiuana harakati zaidi kuliko ki chama tawala, na hamjajipanga kwa sura ya kitaifa na utayari wa kutawala nchi.

Kwa upande wa Chadema, lazima kibadilike, first and foremost, anzeni na Mwenyekiti wenu Freeman Mbowe, he should go!. Ajiuzulu uenyekiti, ampishe more able person kama Dr. Slaa kwenye usukani wa chama, Katibu Mkuu mpeni Zitto strategically, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, na kulivua lile koti la ukanda na ukabila ili walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura 2015 kwa kujionyesha Chadema ni chama cha wote, dini zote na kanda zote.

Kupumzishwa kwa Freeman Mbowe sio kuwa hafai no, anafaa sana lakini kwa background yake na nature ya kazi zake, as a businessman, hapo alipoifikisha Chadema amaishafanya kazi kubwa na kufikia mwisho wa uwezo wake. Kwa background yake ya a former DJ na sasa ni mfanyabiashara, focus ya wafanyabiashara kote dunia nzima ni maximisation of profits, hivyo Mbowe atahitaji ruzuku ya Chadema itumike kuivest kwenye assets, kwenye vitu vya kuonekanika yaani assets kama magari, mavazi, etc

Ili Chadema kiweze kushika nchi 2015, it has to invest on people na sio ku invest kwenye vitu. Chadema must invest kwenye mass mobilisation na sio kutegemea mikutano ya hadhara na maandamano. Chadema needs to have able people kuiwezesha kushika dola five years to come kwa kutumia reaching out mechanism kuwafikia the mases kwa kumiliki media yake yenyewe. Chadema lazima ifanye recruitment ya loyal able people, watakaokuja kuendesha serikali ya Chadema. Mbowe hawezi kukubali ruzuku ya Chadema itumike to invest on people, kwasabu it's a loss making venture kwa mfanyabiashara na kuivest kwenye mass media sio profitable investment kwa business man ambaye ni in for profits making!. Dr.Slaa na Zitto sio wafanyabiashara hawa ni ma technocrats. Chama kishikwe na wanasiasa watendaji ma technocrats na sio wanasiasa wafanyabiashara!. Chadema iwekeze kwenye watu na kupanua mtandao wake hadi vijijini, ili kwenda kuiongoa CCM kuanzia kule chini kabisa kwenye mizizi yake ambako ni kule kwenye mashina. Chadema imiliki media yake yenyeshe for mass mobilization na sio kutegemea mikutano na maandamano, huko ni kuendeleza uanaharakati, Chadema inatakiwa kukaa mkao wa kutawala, ikitangaza kitu, kinafika Tanzania nzima!

Paskali
That was 13 years ago!.
P
 
Kina Pascal Mayalla wanasema siasa za confrontational politics zimewaumiza zaidi Chadema kuliko kuwasaidia kwani dola ilitumia mwanya huo kuwakandamiza.

Hivyo 'radical elements' kama kina Heche wataipata Chadema wakati mgumu kutoka vyombo vya dola, bora kina Mbowe anagalu wanaumwa ila Kuna mida wanapulizwa na kupakwa spirit.

JokaKuu zitto junior Kalamu brazaj
Kwanza kabisa mkuu 'Proved', hayo ya akina Pascali nadhaniu nilishakueleza bayana, linapokuja jambo lolote na rejea ya jina hilo, usinihusishe na jambo hilo kabisa; kwa sababu hakuna lolote ninaloheshimu toka kwa mtu wa aina hiyo.
Baada ya kuyasema hayo, nikueleze kuhusu CHADEMA. Kama safari hii watakubali tena upuuzi wa CCM, ni bora wafungashe tu vilago na kuondoka kabisa kwenye shughuli za siasa za Tanzania.

CCM wakati wote sasa wanapanga uharibifu tu na kukiuka taratibu zote na sheria ili wabakie madarakani.

Ni wajibu wa watu kukataa upuuzi huo kwa njia zote ziwezekanazo.
Wanayofanya CCM sasa hivi ni kuonyesha kiburi na kudhani hakuna lolote linaloweza kufanyika dhidi yao.

Kuwa na 'Dola' na kuitumia dola hiyo kufanya uhalifu kuna mwisho wake. Itafika wakati vyombo hivyo na wananchi watakataa upumbavu huo.
Wakati huo umewadia. CHADEMA ni muhimu wawaongoze wananchi kukataa ushenzi huu.
 
..mimi naona Mbowe na Lissu wanafanya vizuri kama Mwenyekiti na Makamu wake.

..Chadema kuna uhuru wa mawazo na sio chama ambacho kinakwenda kwa kufuata haiba ya Mwenyekiti.
Mradi tu Mbowe asiingilie juhudi za chama kukataa uhujumu unaofanywa na CCM.
Mbowe amebadilika. Kama kuna asali alionjeshwa na baadae akataka kuitema, naona sumu iliyokuwemo kwenye asali ile haikumwacha salama hata kidogo.

Ni sawa na ile Corona iliyomwathiri Philipo Mpango. hajawahi kurudia hali yake ya kawaida baada ya gonjwa lile.
 
Mwanasiasa ni yule anayekubali kufanyiwa uhuni na kutulia, ila mwanaharakati ni mwanasiasa mwenye misimamo mikali ama? Hebu nipe tafsiri ya mwanasiasa na mwanaharakati ili nione tofauti yake, isije ikawa ww ni wale bendera fuata upepo kwa maneno hayo.

Kumbuka Nyerere aliitwa mwanaharakati na wakoloni, same kwa Mandela wakati wa kupambana ubaguzi wa rangi. Huenda na ww umetekwa na propaganda hiyo hiyo.

Tofauti za wanasiasa na wanarakati ziko hapa:

Tuzitambue tofauti za vyama vya upinzani (ACT, CHADEMA, CUF, nk) na Wanaharakati

Kuna:
1. Mwanaharakati (usu)- kama kina Maria
2. Mwanaharakati mwanasiasa - kina Lissu, Seif, Mtikila, Mandela, Malema, nk
3. Mwanasiasa (usu) - Cheyo, Lipumba nk
 
Bila Mbowe nchi ingekuwa kwenye mgogoro mkubwa sn
Mkuu 'Benja', wewe huoni nchi ipo kwenye mgogoro mkubwa zaidi ya unavyofkiria wewe?
Mgogoro unaozidi Chama kuhodhi uongozi kwa nguvu, huo siyo mgogoro mkubwa?

Unataka kuona mgogoro wa namna gani hasa ndipo utambue kuwa kuna mgogoro. Hadi damu itiririke mitaani?
 
..mimi naona Mbowe na Lissu wanafanya vizuri kama Mwenyekiti na Makamu wake.

..Chadema kuna uhuru wa mawazo na sio chama ambacho kinakwenda kwa kufuata haiba ya Mwenyekiti.

Demokrasia ingeachwa ichukue mkondo wake kwa nafasi zote chamani kupitia primaries kama ilivyo kwenye chaguzi kote kuliko staarabika.

Yaweza kuwa wapo wengi wenye kufaa na hata pengine bila nafasi ipi kubinafsishwa kwa mtu au watu. Lolote linawezekana.

Tusijifungamanishe na watu na kudai kijuu juu tu kwa kujifurahisha kuwa kuna demokrasia vyamani. Ikibidi tupate independent au external assessors kututathmini.

Wanapiga hatua sana wanaoikumbatia demokrasia. Agenda zinapaswa kuwa za wengi. SI za mtu. Hapa ndipo tunapofeli vyamani na hata kama Taifa.
 
Mkuu 'Benja', wewe huoni nchi ipo kwenye mgogoro mkubwa zaidi ya unavyofkiria wewe?
Mgogoro unaozidi Chama kuhodhi uongozi kwa nguvu, huo siyo mgogoro mkubwa?

Unataka kuona mgogoro wa namna gani hasa ndipo utambue kuwa kuna mgogoro. Hadi damu itiririke mitaani?
Hapana mkuu, kuna hekima na busara ni kitu kikubwa sn, Mbowe ni mvumilivu sn tofauti na watu wengine
 
Hapana mkuu, kuna hekima na busara ni kitu kikubwa sn, Mbowe ni mvumilivu sn tofauti na watu wengine
Mbowe alishajijengea heshima ya kipekee sana alipoivusha CHADEMA wakati wa misukosuko ya kutisha sana na kuweka usalama wa maisha yake rehani.

Akirudi nyuma kwa namna nyingine yoyote, baada ya kujitambulisha vile, atajivunjia heshima yote aliyojijengea katika jamii.

Kazi anayotakiwa kuisimamia na viongozi wenzake, ni kuhakikisha CCM, katika sura nyingine yoyote inayojionyesha nayo haibaki madarakani.
Natumaini utanielewa nilicho andika hapa.
 
Binafsi naona Mbowe angeachia kijiti cha uenyekiti wa Chama ampe Lissu au Heche John

Nasema haya kwasababu Chadema kwa sasa na upinzani unahitaji mtu mwenye maamuzi magumu, misimamo mikali na ambaye hajapoa sana

Simchukii Mbowe hata kidogo wala siangalii ukabila wala dini, ingekua natizama hayo basi ningemfavor mbowe kwasababu labda tunatoka kijiji kimoja. Mimi sio mkabila kama mwendazake au mdini kama Gwajima.

Nachotazama ni utendaji, sasahiv upinzani wanahitaji apatikane mtu mwenye misimamo mikali sana sio mtu mpole mpole kama Mbowe.

Chama kinahitaji watu kama Lissu au wengineo ndo waongoze Chama sio Mbowe

Mbowe sasa imetosha!! Mkabidhi mtu mwingine kijiti sasa!
Ana hela huyo Lisu? Mbona alikuwa nccr Kwa nini haikuwa vizuri?

Kama anajiamini atoke akaanzishe chama chake tuone
 
Pamoja na kwamba mimi siyo shabiki wa chadema tangu niondoke huko, nakubaliana na wewe kwa mbowe kuondoka na kupisha mtu mwingine. Lakini sikubaliani na pendekezo lako la kutaka amwachie lisu uenyekiti. Kumwachia lisu ni kutaka kukiua chama. Lisu hawezi kuongoza taasisi kama chama, anaweza kuongoza genge la wahuni wahuni tu wavuta bangi ambao wanaweza kufuata misimamo yake ya kichizi bila kushughulisha mbongo zao. Akiwaambia kwenda barabarani wanaenda tu bila kuhesabu gharama wala consequences.
Lisu akiwa Mwenyekiti hicho kutakuwa sio chama Bali genge la wanaharakati ambao wataishia kuwa busy na kesi badala y kufanya siasa.

Pili vile anajiona mjuaji basi itakuwa ni ugomvi Mwanzo mwisho.

Mwenyekiti anatakiwa kuwa mtu dizaini ya Zito,Mnyika,na watu wengine modarate sio hao wanaharakati
 
Back
Top Bottom