Ninaamini kabisa ubora wa kiongozi hupungua baada ya muda Fulani, kwangu miaka 10 ni kipimo Bora kabisa, siwajibiki kwenye muda unaoamini ww Wala kukukatalia popote. Uzuri Nina mifano ya ninachoamini. Huyo Mbowe ni mmoja ya case study yangu ya kiongozi kukaa zaidi ya miaka kumi kwenye nafasi Moja ya kuteuliwa.
Kumfuata kiongozi mstaafu akupe ushauri, sio kumtaka arudi kuongoza. Kuna tofauti kubwa ya kuomba ushauri kwa mstaafu, na kuongoza. Ni kipi hakieleweki hapo?!
Mkuu ninasisitiza tena, ninachoamini hakimshurutishi yoyote kukiamini hata nikibaki mwenyewe kwenye hili ninaloamini. Kwangu Mimi miaka 10 ni muda tosha kabisa kwa kiongozi kukaa kwenye nafasi Moja ya kuchaguliwa hii ni bila kujali ww unaamini kwa muda gani, ama unatumia vigezo gani vingine. Wangalau miaka 15 kwa shingo upande. Baada ya hapo hata nishikiwe bastola siwezi kukubali hali hiyo. Sioni unapata wapi shida kwa jambo ambalo naamini mimi, wakati huo huo Sina tatizo na unaloamini ww, shida Iko wapi hapa?!