Lisu ni mwanaharakati zaidi kuliko mwanasiasa.
 
Lisu ni mwanaharakati zaidi kuliko mwanasiasa.
Mwanasiasa ni yule anayekubali kufanyiwa uhuni na kutulia, ila mwanaharakati ni mwanasiasa mwenye misimamo mikali ama? Hebu nipe tafsiri ya mwanasiasa na mwanaharakati ili nione tofauti yake, isije ikawa ww ni wale bendera fuata upepo kwa maneno hayo.

Kumbuka Nyerere aliitwa mwanaharakati na wakoloni, same kwa Mandela wakati wa kupambana ubaguzi wa rangi. Huenda na ww umetekwa na propaganda hiyo hiyo.
 

Hii ngoma inataka kwenda all out war. Nguvu zote ziwe consolidated. Hakuna kupoa.



Kwenye ukombozi hakuna kupoa na haitakuwa rahisi.

Tuikatae mifarakano.

Kina Mwabukusi, Slaa, na wote walilodhamiria kutaka katiba mpya Sasa na kumwondosha CCM pasi na kuchelewa tena, wote hao ni wenzetu.
 
Mbowe akiwa mwenyekiti wa Chadema maisha yake yote sidhani kama kuna athari yoyote kwa taifa. Tatizo ninaloona mimi ni madhara ya utawala wa ccm na tanu kwa miaka 60 katika nchi hii.
 
Mbowe akiwa mwenyekiti wa Chadema maisha yake yote sidhani kama kuna athari yoyote kwa taifa. Tatizo ninaloona mimi ni madhara ya utawala wa ccm na tanu kwa miaka 60 katika nchi hii.
Maoni yako yanaheshimika na kuthaminiwa.
 

..mimi naona Mbowe na Lissu wanafanya vizuri kama Mwenyekiti na Makamu wake.

..Chadema kuna uhuru wa mawazo na sio chama ambacho kinakwenda kwa kufuata haiba ya Mwenyekiti.
 
Mkuu kimsboy, karibu uangalie hili ni bandiko la lini CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
That was 13 years ago!.
P
 
Kwanza kabisa mkuu 'Proved', hayo ya akina Pascali nadhaniu nilishakueleza bayana, linapokuja jambo lolote na rejea ya jina hilo, usinihusishe na jambo hilo kabisa; kwa sababu hakuna lolote ninaloheshimu toka kwa mtu wa aina hiyo.
Baada ya kuyasema hayo, nikueleze kuhusu CHADEMA. Kama safari hii watakubali tena upuuzi wa CCM, ni bora wafungashe tu vilago na kuondoka kabisa kwenye shughuli za siasa za Tanzania.

CCM wakati wote sasa wanapanga uharibifu tu na kukiuka taratibu zote na sheria ili wabakie madarakani.

Ni wajibu wa watu kukataa upuuzi huo kwa njia zote ziwezekanazo.
Wanayofanya CCM sasa hivi ni kuonyesha kiburi na kudhani hakuna lolote linaloweza kufanyika dhidi yao.

Kuwa na 'Dola' na kuitumia dola hiyo kufanya uhalifu kuna mwisho wake. Itafika wakati vyombo hivyo na wananchi watakataa upumbavu huo.
Wakati huo umewadia. CHADEMA ni muhimu wawaongoze wananchi kukataa ushenzi huu.
 
..mimi naona Mbowe na Lissu wanafanya vizuri kama Mwenyekiti na Makamu wake.

..Chadema kuna uhuru wa mawazo na sio chama ambacho kinakwenda kwa kufuata haiba ya Mwenyekiti.
Mradi tu Mbowe asiingilie juhudi za chama kukataa uhujumu unaofanywa na CCM.
Mbowe amebadilika. Kama kuna asali alionjeshwa na baadae akataka kuitema, naona sumu iliyokuwemo kwenye asali ile haikumwacha salama hata kidogo.

Ni sawa na ile Corona iliyomwathiri Philipo Mpango. hajawahi kurudia hali yake ya kawaida baada ya gonjwa lile.
 

Tofauti za wanasiasa na wanarakati ziko hapa:

Tuzitambue tofauti za vyama vya upinzani (ACT, CHADEMA, CUF, nk) na Wanaharakati

Kuna:
1. Mwanaharakati (usu)- kama kina Maria
2. Mwanaharakati mwanasiasa - kina Lissu, Seif, Mtikila, Mandela, Malema, nk
3. Mwanasiasa (usu) - Cheyo, Lipumba nk
 
Bila Mbowe nchi ingekuwa kwenye mgogoro mkubwa sn
Mkuu 'Benja', wewe huoni nchi ipo kwenye mgogoro mkubwa zaidi ya unavyofkiria wewe?
Mgogoro unaozidi Chama kuhodhi uongozi kwa nguvu, huo siyo mgogoro mkubwa?

Unataka kuona mgogoro wa namna gani hasa ndipo utambue kuwa kuna mgogoro. Hadi damu itiririke mitaani?
 
..mimi naona Mbowe na Lissu wanafanya vizuri kama Mwenyekiti na Makamu wake.

..Chadema kuna uhuru wa mawazo na sio chama ambacho kinakwenda kwa kufuata haiba ya Mwenyekiti.

Demokrasia ingeachwa ichukue mkondo wake kwa nafasi zote chamani kupitia primaries kama ilivyo kwenye chaguzi kote kuliko staarabika.

Yaweza kuwa wapo wengi wenye kufaa na hata pengine bila nafasi ipi kubinafsishwa kwa mtu au watu. Lolote linawezekana.

Tusijifungamanishe na watu na kudai kijuu juu tu kwa kujifurahisha kuwa kuna demokrasia vyamani. Ikibidi tupate independent au external assessors kututathmini.

Wanapiga hatua sana wanaoikumbatia demokrasia. Agenda zinapaswa kuwa za wengi. SI za mtu. Hapa ndipo tunapofeli vyamani na hata kama Taifa.
 
Hapana mkuu, kuna hekima na busara ni kitu kikubwa sn, Mbowe ni mvumilivu sn tofauti na watu wengine
 
Hapana mkuu, kuna hekima na busara ni kitu kikubwa sn, Mbowe ni mvumilivu sn tofauti na watu wengine
Mbowe alishajijengea heshima ya kipekee sana alipoivusha CHADEMA wakati wa misukosuko ya kutisha sana na kuweka usalama wa maisha yake rehani.

Akirudi nyuma kwa namna nyingine yoyote, baada ya kujitambulisha vile, atajivunjia heshima yote aliyojijengea katika jamii.

Kazi anayotakiwa kuisimamia na viongozi wenzake, ni kuhakikisha CCM, katika sura nyingine yoyote inayojionyesha nayo haibaki madarakani.
Natumaini utanielewa nilicho andika hapa.
 
Ana hela huyo Lisu? Mbona alikuwa nccr Kwa nini haikuwa vizuri?

Kama anajiamini atoke akaanzishe chama chake tuone
 
Lisu akiwa Mwenyekiti hicho kutakuwa sio chama Bali genge la wanaharakati ambao wataishia kuwa busy na kesi badala y kufanya siasa.

Pili vile anajiona mjuaji basi itakuwa ni ugomvi Mwanzo mwisho.

Mwenyekiti anatakiwa kuwa mtu dizaini ya Zito,Mnyika,na watu wengine modarate sio hao wanaharakati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…