Hivi kugoma kula huwa ina impact sana hata nje anaona wanaitumiaga sana ulaya na kwingene kuna sheria za kimataifa haki ya kula mfungwa wanasheria nijuzeni
Ukigoma kula ni Hatari sio ndogo,MAGEREZA ni SERIKALI wanachokwepa ni MTU KUFIA MAGEREZA maana serikali ndio itaonekana imemu ua.
Dunia haiwezi kukuelewa mtu hana silaha umempokonya kila kitu halafun afe ndani mwako,HUELEWEKI HATA UONGEE KIZULU.
Kinachotokea ukigoma kula...
Askari wa zamu atakutisha kukupiga kula kula kula, ukigoma Watakutingisha kwa kukupiga kidogo wakutishe,Wakiona misimamo Mikali
Ataitwa ASKARI mwenye sifa ya ukorofi na ukali anae ogopwa,atakuja akutishe ULE...usipokula pamoja na vitisho vyake,
Wanajua hii issue iko serious,Wanaanza kuku pet pet na kukubembeleza...UKIGOMA BADO
ANAITWA BWANA JELA WA MAGEREZA (hawa wazee huwa wana busara kuliko YESU) Bwana jela ASKARI MKUU WA GEREZA HILO akija kwanza wafungwa wengi humpenda maana anafata sheria kuliko MAHAKAMA huyo hapindishi sheria anaijua sheria na anaisimamia SHERIA
huyo akija hata kama kuna mgomo wafungwa hulegeza kamba na huyo aki ahidi kitu kita timizwa,
BASI akija BWANA JELA atasema uletwe akusikilize mtakaa nae OFISINI nyie wawili tu, Utamweleza unachotaka (95%) ya mahitaji ya wafungwa/mahabusu yanayomfikia BWANA JELA huwa yanatatuliwa ndani ya masaa 12 sio 24 ni hapo kwa hapo hata kama ni simu kwa rais itapigwa hapo hapo ki ufupi shida ikimfikia yeye imeisha.
Kwa CASE ya LISSU bwana JELA anaweza asiitatue maana kama yuko serious sana basi BWANA JELA NAE ATAMUITA MKUBWA WAKE
Ki ufupi kuhusu Kula tuuu Lissu atakataaa huku nnje ila TEAM YA MAGEREZA UONGOZI WA JUU WAKIJA KWA PAMOJA WALE UTAKULA TUUUU maaana ni wazeee,wenye hekima kama za abrahamu wanaongea na wewe kama vile wana mamlaka ya kukuachia uende uraiani so kula tu LISSU atakula
ila katika Vitu vinawatisha MAGEREZA ni mahabusu/mfungwa kugoma KULA ni 1 ya kitu hawaruhusu hata kwa bahati mbaya.
lakini WEWE unae GOMA hakikisha una uwezo wa kugoma kweli huku case yako ikiendelea kuwa solved sio uwe kinjaa njaa.
Kwa hii LISSU anaweza shinikiza na akapata anachotaka kwa Strategy hiii..
SWALI : LISSU anaweza kushinda njaaa kweliiiii???? maana mlolongo huu ni mrefu na haya yote nilio yaaandika kwa mtu kama LISSU yatachukua siku 1 tu kukamilishwa na si zaidi ya masaa 24