Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Mshana acha uongoo kizazi cha saivi siyo kma kile chenu ambacho ndoa ilikuwa jambo LA muhimu na msingi kama hoja zako hazijatofautisha kizazi na kizazi basi hazina mashiko vijana siyo waoga wala hawana matatizo ya kiakili wala kimaumbile ila Yale wanayoyaona na kuyashuudia
Sawa Aiba
 
Lengo la ndoa ni kujenga familia bora kiroho na kimwili, familia ndio ujenga taifa bora.Duniani pote huwezi ukawa muhuni ukapewa uongozi haipo hio.
Viongozi wote wameoa
Hoja dhaifu mno, tangu lini kuoa/kutooa kikawa kipimo cha uhuni!? Ukichunguza utagundua wanandoa ndo wahuni wabobezi na yote ni sababu walichokutana nacho ndani ya ndoa ni tofauti na walichotarajia! Ndoa zimejaa migogoro, usaliti chuki na majuto.
#KATAANDOA
 
Imani ni nini na dini ni nini
Imani ni hali ya mtu kuamini kwenye kitu fulani pasipo sheria/Amri.

Dini ni imani zilizo wekewa sheria ili zifuatwe na watu wengine pasipo kuhoji chochote. You just believe, No questioning that's Religion.
 
Lengo la ndoa ni kujenga familia bora kiroho na kimwili, familia ndio ujenga taifa bora.Duniani pote huwezi ukawa muhuni ukapewa uongozi haipo hio.
Viongozi wote wameoa
Sisi Wakristo kiongozi wetu (Yesu Kristo) hakuwahi kuoa. Nipe mifano ya hao viongozi waliooa wenye busara, hekima na uongozi bora zaidi ya Yesu.
 
Nina marafiki wengi waliooa, naona na kusikia majuto yao. Nimesuluhisha sana migogoro ya ndoa na kujifunza mengi kupitia migogoro hiyo. Pamoja na yote ninekuwekea mifano michache ya watu maarufu wanaohangaika na ndoa zao kipindi hiki (Dr. Mwaka, Manara) na wewe nipe mifano ya watu wanaojuta kutooa.
Nje ya ndoa kuna uhuru, Sex (ngono) pia inapatikana kama kawaida, watoto unapata bila ndoa na zaidi unaepuka stress zisizo na ulazima.
Ndoa ni kichaka cha wanawake kuwanyonya na kuwavuruga wanaume.
#KATAANDOA
Uko sahihi kabisa, lakini hayo hayajaanza leo au jana yalikuwepo toka enzi.
Kabla sijaingia kwenye hiyo taasisi nami baadhi ya marafiki nilisuluhisha sana mpaka nikawa napata hofu lakini maisha ni kuwa optimistic tu, zaidi ya miaka 15 ya ndoa sijawahi kujuta kabisa nafurahia maisha.

Siyo lazima yaliyotokea kwa mtu yatokee kwako kila mtu ana destiny yake.
 
Key points ni kwamba KILA mmoja anaoa kwa sababu zisizofanana na mwingine.
Wengi kwa ajili ya
1.ngono
2.heshuma
3.Kuzaa watoto wote na mama mmoja
4.Mlinzi wa mali
5.Mlinzi wa nyumba yako
6.Katibu au msaidizi wa mambo yako
7
Hizi tofauti ndizo ufanya tuwe tofauti juu ya mitazamo ya ndoa.
Vyote hivyo unaweza vipata ukiishi na mwanamke bila ndoa yani kavu kavu.
 
Akili yako imedumaa! Unahisi kuoa/kuoelewa ndo kila kitu katika maisha!!?? Hiyo sex hata bila ndoa inapatikana tena kirahisi mno. Kwa taarifa yako hata mashoga wana ndoa zao kama nyinyi.
Ndoa si kwasababu ya sex,ndoa ni kwasababu ya kujenga familia iliyo bora
Dini hairuhusu kuishi na mwanamke bila ndoa

Ndoa ni kutii maamrisho ya Mungu.
 
Ndo muurudishe huo mfumo dume..mnashindwaje kuwacontrol wanawake zenu? Hao wanaowaambia wanasumbuliwa na wake zao kuna mahala wameharibu toka mwanzo thats why wameshindwa kucontrol na kuwa na power over them...mwanaume ni kichwa na hivyo inapaswa kuwa..
Tatizo ni sheria ya ndoa, ukitaka kutumia mfumo dume basi jiandae kupambana na sheria ya ndoa inayompa haki zote mwanamke! Dr. Mwaka amejaribu ku-apply kidogo mfumo dume kwenye sakata lake, nadhani unaona anavyosakamwa!
Ndoa ni kichaka cha mwanamke kumuendesha mwanaume...#KATAANDOA
 
Hali inazidi kuwa mbaya kwa vijana wetu hasa hawa wa kiume wanahamasishana kila kona na kampeni yao yenye hashtag #KATAA NDOA

Sababu wanazotoa zinachekesha mno na kwakweli hazina mashiko.. Kubwa ikiwa ni kuogopa kusalitiwa lakini pia kuna la uchoyo na kukwepa majukumu ila haya hawayasemi kwa uwazi

Hili jambo ni kama fasheni yenye mass hallucination ndani yake! Itapita lakini inaweza kuacha madhara kwa wengine hivyo hatuwezi kukaa kimya

Haya ndio makundi yao

1. Wasiojiamini..
Hawaamini kama wanaweza kutunza mke kutokana na story za vijiweni
Hawaajiamini kama wanaweza kumridhisha mwanamke kitandani
Hawajiamini kama wanaweza kutulia kwenye ndoa bila kuwa na vimada
Hawajiamini kwamba watapendwa na hawawezi kusalitiwa!


2. Wenye kasoro za kimaumbile
Wanaojihisi ni vibamia
Wanaojihisi hawawezi kumpa mwanamke ujauzito
Wasiotahiriwa
Wagumba kwa ithibati

3. Waathirika kisaikolojia
Kutokana na makuzi mabaya
Kutokana na malezi mabovu
Waliolelewa na walezi katili
Walioathirika na punyeto
Walioumizwa kimapenzi
Waliosalitiwa

4. Wasela na wakaa geto
Maisha hayajasimama
Wanaishi kwa kuungaunga
Wasiopenda majukumu

5. Wenye kasoro za kijinsia
Mashoga wa kujificha (mchicha mwiba)
Madomo zege
Wenye ulemavu uliojificha

6. Wapenda kitonga, dezo
Wanaolelewa na wake za watu
Wanaotunzwa na mashangazi
Wanaopenda vya bure toka kwa yeyote
Wapenda shortcut
Wavivu wasipenda kujishughulisha
Wapenda starehe

7. Bendera fuata upepo
Wanashadadia tu kwasababu fulani kasema
Wanafuata mkumbo kwakuwa fulani yumo
Wanadhani ndio usasa na ndio ujanja

Washauri wao wakuu
Walioshindwa kuhimili changamoto za ndoa
Walioachwa, waliopigwa kibuti
Walioharibu kwenye ndoa zao
Wapotoshaji

Nisiandike sana ngoja niweke kituo hapa
5.
 
Back
Top Bottom