Ufisadi ni ufisadi tu, Wizi ni wizi tu na Rushwa ni rushwa tu. Hakuna fisadi mkubwa wala mdogo, Hakuna mwizi mkubwa wala mdogo, vile vile hakuna mla rushwa mkubwa wala mdogo. Kama ni ufisadi wote waitwe mafisadi, kama ni wezi wote waitwe wezi na kama ni wala rushwa wote waitwe wala rushwa.
Kipimo kile kile kinachotumika kuwapima wanachama wa CCM, ndiyo pia kitumike kumpima na Heche. Kama kweli tunapinga ufisadi hatupaswi kuwa na double standards. Bwana Yesu alitufundisha "Kwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa" Mathayo 7:2