Tetesi: Mange Kimambi: Ujambazi wa rasilimali za Tanzania unaendelea kwa kasi

Tetesi: Mange Kimambi: Ujambazi wa rasilimali za Tanzania unaendelea kwa kasi

Bora wapewa waarabu hizo Taasisi zinazosimamia zinalipa mishahara midogo na wala wafanyakazi hanufaiki ,DP world ilivyopewa gati lile imelipa wafanyakazi mishahara mara mbili ya awali ...Mamlaka inayosisimamia hapo KIA inalipa watu mishahara midogo na ilibaki wanakula viongozi ,kiwanja kidogo ila unakuta mlolongo wa viongozi wote wanaiba.
 
Huyo dada wa huko California baada ya ule ujinga wa tarehe 29 October wengi wetu tumemjua vizuri na kwa ukaribu kichwa chake kinafanya kazi vipi.

Mtanzania wa kawaida mwenye akili timamu anaelewa kwamba Bandari haijauzwa kwa mtu yoyote imekodishwa kwa DP World sawa na ambavyo TICTS ilikodishwa kwa miaka 30 na baadae serikali ikaichukua bandari yake baada ya TICTS kushindwa kutimiza baadhi ya vigezo vya mikataba.

Unapotengeneza fitina za mitandaoni madhara yake huwakuta wanaohusika na wasiohusika, taharuki ya moja kwa moja huikuta jamii nzima. Huyo dada hawezi kuelewa ubaya wa anachokifanya kwa sababu yeye yupo huko USA.
Ulishaona Mkataba wa TICS na DP World? Unaweza kulinganisha?
Tatizo likiuwa mkataba siyo nani anakodishwa.

Halafu kumvika lawama huyu mwanamke mdogo ambaye yupo LA ni upuuzi. Suala la msingi mmeacha, utekaji, upotezaji, uongo uongo wa polisi. Accummulation of all such evils, mnaenda ati kumsingizia yule mama hata wala hana kitu, she is just suviving in the US of America. Haaaa.

Unakuja hapa unajisahaulisha kuwa mmeteka watu, mmeua na hata mmevuruga amani ya nchi, angalia ule uchaguzi, ati 98% kura and 31 million of 87 participation!

Acheni upuuzi
 
Hao si magaidi ndugu yangu.. According to you Mgalatia😅
Wewe unapata picha gani mkuu, baada ya attempt kadhaa kufanyaka na wanaotakiwa kusikia hawasikii na wenye matakwa yao ya msingi bado hawaelewi, alafu mwendo ndio kama huu! Unadhani wataendelea kutumia njia za maongezi kama ilivyo awali na hali ndio kama hivi
 
Swali:

JE, KUNA MTU ALIHITAJI KUAMBIWA NA MANGE KIMAMBI KUWA UFISADI NI MKUBWA TZ??

Kama wewe mpaka leo hujaona uhusiano kati ya ugumu ulionao kimaisha na huu ujambazi wa CCM basi game lako tight sana!

Ndiyo maana utapeli wa harakati una mafanikio makubwa sana hapa nchini. Mngekuwa serious kwenye kudai haki kusingekuwa na NGO za harakati nyingi kama ilivyo sasa.

Anyway, endeleeni kuwanufaisha matapeli wenu huku mkijadili siri za mikakati ya kuing'oa CCM hadharani kwenye LIVE na SPACE zao.

Nchi hii inastahili TUZO ya dunia ya Unyonge uliopitiliza!

Watu watatekwaje mbele ya umati mchana kweupe halafu mkajidai mnapambania mabadiliko?!

Tunachoshana sana! Wapinzani wamechoka kujitoa mhanga bila support. Sasa tumebaki na Wanaharakati wa NGO wanaolipwa kupaza sauti bila kukiri kuwa wanalipwa!
 
KWA MAZINGIRA YA SASA GEN Z WAKITANGAZA MAANDAMANO HATA KAMA HAWATAFANYA, VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA LAZIMA VIWEKE LOCK -DOWN.

KUWEKA LOCK-DOWN MAANA YAKE NI KUKWAMISHA SHUGHULI NYINGI ZA KIUCHUMI; UTALII UNADORORA ZAIDI, BANDARI KUNASIMAMA, USAFIRI WA ANGANI NA ARDHINI UNADORORA ZAIDI NA MAPATO YA SERIKALI YANAPUNGUA.
 
Tatizo lako wewe mtu huwa husome ukaelewa.
We ukiona tu jina langu unakurupuka.

Nimeuliza hapo juu. Km Tanzania imeficha habari ya kuuza KIA kwa hofu ya kuwachafua watanzania Je na OMAN PIA WAMEFICHA kwa kumuogopa nani?

We unajua maana ya Nchi kuingia mkataba na NCHI ingine wa kuendesha vyombo vya usafiri qa ANGA na MAJI? au unadhani hio ni kama biashara ya Korosho za mtwara?

Mikataba ya namna hio ni extremely serious .
Nchi ikifanya mchezo inaweza kumalizika kabisa kwa muda mfupi mno.

Sasa Mkataba serious namna hio Tanzania ifiche na OMAN ufiche ?
leo tuupate kwa mange kimavi na copy ya BRELA?
Come on!
Huenda huna elimu hizi lkn jaribu kufikiri basi kabla hujaandika humu. Unatia aibu mzee mzima.

Details za mkataba zinatoka kwa Mange kwa saab pande zote mbili zinataka mkataba ufichwe.

Serikali ikitaka siri inawezakumwambia jambazi mwenzie ambae wamemuuzia nchi kwamba LETS KEEP THIS SHIT OFF THE RADAR !!!!! Kwa madai na vigezo vya BUSINESS SECRETS.

Na si kweli
kwamba mwekezaji anataka uwazi.
Wawekezaji hushinikiza mkataba uwe "siri ya biashara."

Muwekezaji hawezi hata siku moja kutaka details za mkataba zianikwe.

Hata wewe ungeshinda tenda ya serikali ungetaka details zianikwe? Vipi kama ume bid kulipwa hela kubwa zaidi na huna qualifications kushinda wenzio na umepewa kimchongo ? Uanike mkataba ili iweje ??

Ndo maana mkataba wa mauzo ya bandari ulivujishwa na Watanzania. Sio Waarabu.

Especially mikataba contoversial. Ya kuuza njia kuu za uchumi.

DETAILS ZA MKATABA WA MCHONGO KWA NINI EITHER PARTY (YEYOTE KATI YAO) ATAKE ZIANIKWE ?????
 
Hauko sawa ktk kufikiria.
Unaona bora wote tuikimbie nchi yetu tuwaachie mafisadi wamalize rasilimali zote?
Utaweza kuhamisha na ndugu zako wote kwenye ukoo wenu?
Huko uendako na wao wangefanya hivyo kwa nchi yao, wewe ungekimbilia wapi?
Uoga na ubinafsi vitu vibaya sana kwa binadamu.
Angekuwa amewahi kuishi nchi yoyote tofauti na nchi yake asingethubutu kuandika ujinga huo. Anadhani kuishi nchi za watu ni rahisi.
 
KWA MAZINGIRA YA SASA GEN Z WAKITANGAZA MAANDAMANO HATA KAMA HAWATAFANYA, VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA LAZIMA VIWEKE LOCK -DOWN.

KUWEKA LOCK-DOWN MAANA YAKE NI KUKWAMISHA SHUGHULI NYINGI ZA KIUCHUMI; UTALII UNADORORA ZAIDI, BANDARI KUNASIMAMA, USAFIRI WA ANGANI NA ARDHINI UNADORORA ZAIDI NA MAPATO YA SERIKALI YANAPUNGUA.
 
Hizi ndio mbanga za kuwaza ..sio mtu anakuambia uandamane ..watu wanakula shares billions wataacha kukupiga risasi ya kichwa ukiingilia ama kutaka kuharibu mitikasi yao ...Bora ufanye mishe mambo yakitiki mzee unaamsha
Upo sahihi mkuu, lkn nyumbani ni nyumbani tuu, ukiona kuna vitu havipo sawa bado roho itakuuma
 
Back
Top Bottom