Mary Chatanda: Freeman Mbowe amekosa shukrani kwa Rais Samia pamoja na kumtoa gerezani. Huenda ameathirika kisaikolojia

Mary Chatanda: Freeman Mbowe amekosa shukrani kwa Rais Samia pamoja na kumtoa gerezani. Huenda ameathirika kisaikolojia

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa Mary Chatanda amemshukia vikali Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe kwa kile alichokieleza kuwa amekosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alimtoa gerezani alikokaa kwa muda mrefu tangu kipindi cha utawala wa serikali ya awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Dkt.John Pombe Magufuli

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara Mkoani Lindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara zake kwenye mikoa ya Kusini mwa Tanzania Chatanda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM amesema, hivi karibuni Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amekuwa akimtukana Rais Samia kwa kueleza kuwa ameuza nchi jambo ambalo halina usahihi na linachonganisha Wananchi, hivyo kutoa wito kwa Wananchi hao kuwapuuza na kutowasikiliza pale watakapoitisha mikutano yao

"...anazungumza, anamtukata, anasema ameuza nchi, kwani sisi tumeuzwa hapa tulipokaa?, Kuna mtu anayesema kuwa nimeshawanunua ninyi ni watu wangu?, Wakija msiwasikilize.., anasema anaenda kujiandaa mikutano 70..."

Ameendelea kueleza kuwa kinachotokea kwa Mbowe sasa inawezekana ameathirika kisaikolojia baada ya kuwa jela kwa muda mrefu hivyo alipaswa kutulia kwakuwa jela kuna mambo mengi.

Chanzo: Jambo TV
Jela kuna mambo mengi......

Mbowe hana shukran.....
 
Ile kesi ya ugaidi ,sama na mh.Rais SSH.....Mbowe angekuwa ndani hadi leo.....
 
Mkorogo unaharibu sana akili za wanawake wengi wa kitanzania.
Mkanye mkeo/binti yako miaka si mingi mazombi watakuwa wengi kuliko maelezo.
Wenye masikio na wasikie.
 
Kesi ya ugaidi....

Ingemmaliza mh.Mbowe.....

Amshukuru sana mh.Rais SSH...

Mbowe hana shukran...
 
Shukrani gani wakati huyo samia wenu anauza bandari? Kum*m*ke watu wengine sijui wanatumia Makal*o kufikir?
Wewe mwenyewe unayatumia hayo kufikiri na ndio maana umedanganyika na kuicheza ngoma ya wanasiasa....ishu ya bandari ni ya kitaalamu....
 
Unaelewa trillion 26 au unaongea tu?
Unayeelewa ni wewe....

Sasa pamoja na mapungufu na matobo yote yanayojulikana pale bandarini tunapata hizo trilioni 7 sasa sijui ugumu utatoka wapi kuzipata hizo 26 ?!! [emoji1787][emoji1787]

Tunakwenda shule kusomea upumbavu ?!! [emoji1787]
 
Sio kwa vipengele defective kama vya IGA ile ukaona trilioni 26 ni kitu!
Vinginevyo wewe unaungana na vipaza wenzio walioko Dodoma wakijiita wabunge.
 
Sio kwa vipengele defective kama vya IGA ile ukaona trilioni 26 ni kitu!
Vinginevyo wewe unaungana na vipaza wenzio walioko Dodoma wakijiita wabunge.
Weka kipengele kimoja defective cha IGA....

Hivi hufuatilii waziri alichokisema.....bado vipengele ni vingi na hatua ni nyingi za makubaliano.....
 
Hapana "mwana"

Mimi ni kijana tu huku kwa Sondombwa nina goli langu la "kahawa na tangawizi"....tumesoma na tunalijenga taifa letu popote tulipo [emoji120]
Ndugu yangu jifunze kusoma. Mkataba ulikuwa humu umejadhiliwa kipengele hadi kipengele. Halafu leo unasema ni wa kitaalamu. Utaalam gani kwenye mkataba wa hovyo kama ule?
 
Ndugu yangu jifunze kusoma. Mkataba ulikuwa humu umejadhiliwa kipengele hadi kipengele. Halafu leo unasema ni wa kitaalamu. Utaalam gani kwenye mkataba wa hovyo kama ule?
Nimeufuatilia binafsi sijaona ukosefu wa utaalamu ndani yake....
 
Back
Top Bottom