Maswali yangu kwa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kuhusu Tamko la Mkataba wa Bandari

Mkuu Baraza la Maaskofu lilikemea vitendo vya kutekana na kuua kipindi cha Magufuli, tena kuna askofu mmoja yeye ndo alisema kabisa kuwa Serikali kufunga mikutano ya kisiasa sio haki cos kazi ya vyama hivyo ni siasa sasa kama wanafunga wanataka vyama vifange nini?

Nakukumbusha! Unajua kwanini Askofu Niwemugizi anyang'anywe Passport yake?

Mikataba aliyovunja Magufuli ilikuwa ya unyonyaji ambayo ndiyo kama huu wa DP World kias wewe ulipewa dhamana pale unasema bora tuvunje kama kulipa tulipe kuliko kuwaachia mpaka shughuli za Bandari zitakapokwisha.

Nakukumbusha! Baada ya kuana haya Magufuli alileta sheria kuwa mikataba yote itakayoungiwa na Serikali inayohusu Rasimali za Taifa basi lazima ije Bungeni iidhinishwe, kwanini aliweka hivi? Ili watanzania wajue viongozi wao wanasaini vitu gani, kama kupinga wapinge na kama kuunga mkono waunge mkono.

Leo hii Samia anapeleka muswada Bungen kutaka kifungu hicho kitolewe na kiseme kuwa baraza la mawaziri likishapitisha jambo kuhusu mikataba ga Rasimali za Taifa iwe ndiyo mwisho.


Kumbuka Mikutano ya Baraza la Mawaziri ni siri, wewe huwezi jua wala huna mamlaka ya kuhoji maamuzi yeyote yaliyofanywa na Baraza la Mawaziri ata Mahakamani.

Nakukumbusha tena kuwa Katiba yetu Ibara 27 (1) (2) inasema kila mtanzania ana wajibu wa kulinda na kutunza Rasimali za nchi, Katiba haikuipa jukumu ili Baraza la Mawaziri wala Bunge wala Mahakama! Ila wananchi wote! Ila leo watu wanataka kuingia mikataba kisiri wananchi wasijue? Tunaenda mbele au tunarudu nyuma?
 

Ulitaka utawala wa Kizungu wa KiRoma urudi ??
 
Tics walipewa Bandari kipindi cha nani? Waliwahi kutoa waraka?

Wakati Magufuli anawaongezea Tics miaka 4 pale bandarini mwaka uliwahi kuona wakitoa waraka?
Sasa wewe ndo hujui! Tics pale Bandarin alikuwa na Gati 2 tu! Na TICS alishindanishwa kwa mujibu wa sheria yetu ya manunuzi hakupatikana kama alivyopatikana DP World.

Kuhusu Magufuli kuwaongezea miaka 4 Tics labda kama huna habari kamili ila huyo Magufuli ndiyo alibadilisha mkataba wa tics ukawa wa vipindi vya miaka mi5 kama hawatakidhi viwango tuvitavyo basi waondoke watupishe! Bila hivo Tics angekuwepo mpaka leo.

Mwisho kabisa nakuuliza? Unajua Kwanini Dp World imetumia mgongo wa IGA?
 
Mkuu mbona unakuwa mgumu kuelewa, hakuna anayepinga uwekezaji tatizo ni vipengele Embu tupe mkataba wa Southampton.
 
Mikataba kama ya kinyonyaji hakuna njia za kisheria za kufuata ili kuachana nayo bila kuisababishia nchi hasara? Kama wanaweza kuchambua mkataba wa Bandari hawakuweza kuchambua taratibu sahihi za kufuata kipindi icho ili nchi isifirisiwe?

Tundu Lissu alipigwa risasi mwezi mwaka 2017. Ukiwahi kuona tamko lao kulaani lile tukio mwaka 2017?


 
Mkataba ni mbovu acha zako. Hata mahakama imeonyesha reservation za msingi sana ila la ajabu wakatupilia mbali shitaka. Kwa namna nyingine walikubali hoja zile za kimsingi za walalamikaji karibu zote. Kwanza ni hili la kulazimu kubadili sheria ili zikubaliane na mkataba inaonyesha wazi mkataba umefungwa kinyuma cha sheria za nchi. Kwamba waislaam wao wakija na azimio kukubali mkataba ni mojawapo ya sababu kuutupilia mbali mkataba maana unaleta mgawanyiko hatari kwenye jamii yetu.
 
Hoja yao kuwa Bandari tuiendeshe sisi hawakuiona wakati TICS anapewa pale Bandarini?
 
Mkataba mbovu kivipi? Kama mtu hajui kutafsiri vifungu asilazimishe ukilaza wake kwa wengine!
 
Mkuu mbona unakuwa mgumu kuelewa, hakuna anayepinga uwekezaji tatizo ni vipengele Embu tupe mkataba wa Southampton.
Vioengele vipi vina shida?

Serikali ilisemaje kuhusu hoja mbalimbali za vipengele?
 
Ko
Ko ulitamani kuona wanaunga mkono hoja?? Wao wameweka hoja zao za msingi ko heshimu maoni yao
Watu wa dini wasijihusishe na shughuli za Serikali. Si wakristo wenzangu si waislamu
 
Kwa nini hawakuibua hoja ya Bandari tuiendeshe wenyewe wakati magufuli anawapa iyo miaka 5 ?
 
Hao wapinga Kristo wakae kwa kutulia



Bwana Yesu alisema: Lakini mimi nawaambia msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. (Mathayo 5:39-40).

Hivyo Wakristo wale ambao wanagombana niWapinga Kristo


Yesu pia alikataza kuitwa Kristo:

Ndipo alipowakataza wanafunzi wake wasimwambie mtu yeyote kwamba yeye ndiye Kristo. (Mathayo 16:20).

Hivyo Wakristo ambao wanatangaza kwamba Yesu ndiye Kristo ni Wapinga Kristo.

Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu. (Mathayo 10:35, Luka 14:26, 12:51, 5:2)

Hivyo Wakristo ambao wanapenda amani wala hawafitini watu hao ni wapinga kristo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…