Mtu anaweza kutoa MAONI fulani kutokana na kutokujua( ignorance). Wananchi walitoa MAONI hayo Kwasababu walifikiri kuwa
(1)viongozi wote wa SERIKALI wana nia njema ( lakini uhalisia siyo hivyo).
(2) Kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya mfumo wa vyama vingi( ilikuwa inatangazwa kuwa vyama vingi vingeleta vita.)
(3) Propaganda za CCM za wakati huo( walikuwa wanatangaza kwenye majukwaa kuwa vyama vingi vitaleta vita)
(4) Kutowaambia wananchi faida za vyama vingi na HASARA ZAKE na FAIDA za chama kimoja na HASARA ZAKE( Hivyo baadhi ya wananchi walitoa MAONI wakiwa blindly.)
Katika muktadha huo J.K.NYERERE aliwasaidia wananchi kuruhusu mfumo wa vyama vingi Kwasababu aliona tishio la maslahi ya nchi katika mfumo wa chama kimoja.
NB
Vyama vingi yalikuwa masharti ya IMF na WORLD BANK kwa nchi masikini ili zipate mikopo na misaada(ya kifedha na kitaalamu). Hivyo kwa mujibu wa wakati husika ilikuwa haikwepeki baada ya kuanguka kwa USSR.