Maswali yangu kwa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kuhusu Tamko la Mkataba wa Bandari

Sisi wananchi tulio wengi, tena hata tulio kwenye imani ya Kiislam, tumefurahishwa sana na tamko la TEC. Hayo ndiyo mawazo yetu Watanzania wengi. Mkataba ule haufai.
 
ccm inapenda kuzalisha watu wajinga ili iwatumie kubaki madarakani. Mtaji wa ccm ni watu wapumbavu
 
haya umeyatoa msikitini,
 
Slaa ameshamaliza kazi iliyompeleka mahabusu lazima aachiwe, wajinga ndio waliwao
 
Hawawezi kujibu hata hoja moja, ni udini tu umewajaa,
Sasa na sie tunasema dp waje anaepinga akatafte inchi aishi au damu na imwagike mshindi aendeshe maisha mbereeeee
 
Swali la kwanza unao uhakika kuwa tulipiga kura huru na wananchi wakaukataa mfumo huo? Kama waliukataa iweje kura za Mrema(TLP) dhidi ya Mkapa(CCM) zilivunja rekodi kiasi uchaguzi ukafutwa na kuanza kuurudia kwa vipandevipande! Nyerere alisema hayo ili ajisafishe na baadae tuliona CCM ilikaria kufa shukurani kwa jeshi la polisi liliiokoa kwa kuwadhibiti wananchi dhidi ya CCM.
 
Mtazamo wangu, sasa hivi wezi na majambazi wanalitumia kanisa.

Wameshikwa pabaya.
 
Wanajificha?yet umesema ni diasporas hueleweki.
Sasa Diasporas hawana majina au? yes wamejificha na kutumia watu nchini kuleta uchochezi na inajulikana wengi wana Pass za nje na hili linawakera sana maana wanataka ya nje na ya ndani. Diasporas wako wengi na wengine hawana habari na haya mambo ila hicho kikundi kidogo ni kina nani na nani ana funds hizi movement za chochoko nyuma yao. Lakini watajulikana tu ni muda tu.
 
Mtazamo wangu, sasa hivi wezi na majambazi wanalitumia kanisa.

Wameshikwa pabaya.
Unadhani wameanza leo? Kwenye list ya waliopewaga za escrow na Rugemalila umewasahau? Kulikuwa na Maaskofu wawili wa hili kanisa pamoja na huyu Mama Tibaijuka. Its not a coincidence!!
 
Hoja 8 muhimu za TEC
14. Ibara zifuatazo za Mkataba huu zina matatizo yatakayosababisha nchi kutofikia uhuru wa kiuchumi (economic independence):

14.1. Ibara ya 2 (1): inayohusu lengo la Mkataba huu ambalo ni kuweka utaratibu unaoibana Tanzania kisheria katika kuendeleza, kuboresha na kuendesha bandari zote za bahari na maziwa, maeneo maalum ya uwekezaji, maeneo ya usafirishaji wa mizigo, na maeneo mengine ya kiuchumi.

14.2. Ibaraya 4: inayohusu wigo wa Mahusiano na Utekelezaji unaoitaka Serikali ya Tanzania kuwajibika kuijulisha Dubai kila fursa ya uwekezaji inapojitokeza.Hiiinakinzana na baadhi ya sheria za nchi yetu, kwa mfanosheria ya ushindani na ile ya manunuzi.

14.3. Ibaraya 5: ambapo DPWorldimepewa haki ya kuendeleza, kusimamia na kuendesha miradi pekee yake, wakati Tanzania inabaki na wajibu wa kumwezesha kufurahia haki hiyo.

14.4. Ibaraya 6:inayoitaka Tanzania kuwajibika kuipatia DP World vibali na vivutio vya kutekeleza miradi yake kama Serikali. Hii inapingana na baadhi ya sheria za kiutaratibu.

14.5. Ibaraya 7: inayoitaka Serikali kuwajibika kutoa mamlaka yanayotakiwa na mwekezaji bila ucheleweshaji.

14.6. Ibaraya 8: Haki ya kutumia ardhi ambapo Mkataba unasababisha uvunjifu wa sheria za ardhi na sheria zinazohusu masuala ya ardhi.

14.7. Ibaraya 10: Usiri wa Mkataba ambapo Mkataba unazuia mamlaka nyingine kama TAKUKURU /BUNGE kufuatilia mikataba.

14.8. Ibara za 23 na 24: zenye ugumu wa kujitoa kwenye Mkataba
 
Mie mmoja wao kivipi?
Aliye mzima hawezi kuwaita maaskofu kuwa wapuuzi na wajinga. Ndiyo maana siamini wewe uliyewaita maaskofu wapuuzi na wajinga, utakuwa mzima.

Kama ni tatizo la afya ya akili, ni bahati mbaya sana, siyo kosa lako la kujitakia. Unastahilo kuonewa huruma, na walio karibu nawe wakusaidie, japo magonjwa ya akili ni vigumu sana kupona kwa 100%.
 
Unadhani wameanza leo? Kwenye list ya waliopewaga za escrow na Rugemalila umewasahau? Kulikuwa na Maaskofu wawili wa hili kanisa pamoja na huyu Mama Tibaijuka. Its not a coincidence!!
Yote sawa, lkn vipi hizi Hoja zao 8
14. Ibara zifuatazo za Mkataba huu zina matatizo yatakayosababisha nchi kutofikia uhuru wa kiuchumi (economic independence):

14.1. Ibara ya 2 (1): inayohusu lengo la Mkataba huu ambalo ni kuweka utaratibu unaoibana Tanzania kisheria katika kuendeleza, kuboresha na kuendesha bandari zote za bahari na maziwa, maeneo maalum ya uwekezaji, maeneo ya usafirishaji wa mizigo, na maeneo mengine ya kiuchumi.

14.2. Ibaraya 4: inayohusu wigo wa Mahusiano na Utekelezaji unaoitaka Serikali ya Tanzania kuwajibika kuijulisha Dubai kila fursa ya uwekezaji inapojitokeza.Hiiinakinzana na baadhi ya sheria za nchi yetu, kwa mfanosheria ya ushindani na ile ya manunuzi.

14.3. Ibaraya 5: ambapo DPWorldimepewa haki ya kuendeleza, kusimamia na kuendesha miradi pekee yake, wakati Tanzania inabaki na wajibu wa kumwezesha kufurahia haki hiyo.

14.4. Ibaraya 6:inayoitaka Tanzania kuwajibika kuipatia DP World vibali na vivutio vya kutekeleza miradi yake kama Serikali. Hii inapingana na baadhi ya sheria za kiutaratibu.

14.5. Ibaraya 7: inayoitaka Serikali kuwajibika kutoa mamlaka yanayotakiwa na mwekezaji bila ucheleweshaji.

14.6. Ibaraya 8: Haki ya kutumia ardhi ambapo Mkataba unasababisha uvunjifu wa sheria za ardhi na sheria zinazohusu masuala ya ardhi.

14.7. Ibaraya 10: Usiri wa Mkataba ambapo Mkataba unazuia mamlaka nyingine kama TAKUKURU /BUNGE kufuatilia mikataba.

14.8. Ibara za 23 na 24: zenye ugumu wa kujitoa kwenye Mkataba
 
Hakuna hoja hapa.

Sasa mimi kukujulisha wewe fursa zilizopo kuna shida gani? Kama kipengele kingeandikwa nitawajibika kukupq fursa hapo ndo kuna shida. Kumjulisha mtu fursa zilizopo shida iko wapi? Na sheria ipi imevunjwa hapo? Sheria ya manunuzi haiongelei kama mtu akijulishwa fursa zilizopo basi taratibu za manunuzi zimevunjwa!

Hiyo 2(1) inaweka utaratibu unaoibana vipi serikali? Maana hakuna kitu kinachoibana Serikali kwenye icho kipengele

Ibara ya 6 haipingani na Sheria yeyote! Wangeitaja iyo sheria wangekuwa na hoja

Ibara ya 7 ina shida gani? Maana hivyo ndo dunia inavyoenda. Wanataka wawekezaji wacheleweshewe vibali? Hawa jamaa hamnazo kabisaaa!! Na nahisi pia wanachangia sana kuhamasisha ukiritimba kwenye serikali yetu.

Haki ya Kutumia ardhi ina shida gani?? Kama wangepewa exclusive right of ownership( haki ya umiliki) hapo at least wangekuwa na hoja! Sasa haki ya kutumia inashida gani? Hawa jamaa sio wazima kwa kweli
 
Kwani mjinga tusi? Mpuuzi nalo ni tusi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…