Maswali yangu kwa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kuhusu Tamko la Mkataba wa Bandari

Maswali yangu kwa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kuhusu Tamko la Mkataba wa Bandari

Shida ni nini? Wakiacha hao waarau bandari si yetu tunabaki nayo?

Au kwa kwa nini wasipewe bandari za Zanzibar kama sisi bara hatutaki?
 
Mfano Mimi mwenyewe naukubali huu mkataba Sasa iweje TEC wafanye technical error ya nna hii?
Sio ww tu unaeukubali hata akina Lord denning Faizafoxy covax HIMARS choiceVariable Lucas mwashamba wanausapoti mkataba huo wenye mapungufu san kweny some articles. Lkn kwakua mmeamua kuitelekeza Nchi kwa matumbo yenu na familia zenu, sa acha tuone je mkate wenu wa kila utayeyuka wa kupush agenda ya DP world ama la!!
 
Mimi siukubali hata kidogo.Ingekuwa amri yangu wote walioshiriki kuandaa,kuushabikia,kuingia makubaliano na kuupitisha ningewanyonga siku ya I Ijumaa mchana.

Sijui kama wewe ungepona.
Hali kadhalika na mimi kwahio technically wapo sawa wamesema wananchi na sio kila mwananchi na last time i checked mimi ni Mwananchi
 
Watu wanaosapoti ule mkataba vilevile ulivyo wanapatikana jamii forums tu na mitandao ambayo watu hawajulikani majina yao halisi. Tangu hili sakata lianze sijawahi kukutana na ndugu, jamaa au rafiki anaye sapoti huu mkataba. Kila sehemu ninapoenda watu wote wanakandia sana. Hata mleta mada vijiweni au maofisini hawezi kuutetea. Ni kichaa peke yake atakubaliana na vile vipengele vinginevyo kama mtu ana maslahi binafsi au kashalamba ela za DP WORLD 🌎.
Ogopa watu waliojificha ambao hawapayuki mitaani,
 
Hali kadhalika na mimi kwahio technically wapo sawa wamesema wananchi na sio kila mwananchi na last time i checked mimi ni Mwananchi
TEC wanawazumzia wananchi wenye akili,wajinga wajinga kama wewe no.
 
TEC hawajawahi kukosea. Wale ni jopo la wasomi na wanajua nini wanasema.
Hakuna usomi wowote. Fatilia performance zao. Mfano Kuna fr mmoja namjua nimesoma naye seminary ana Zero ya pcm alipata point 19. Lakini ni father mpaka leo
 
Mfano Mimi mwenyewe naukubali huu mkataba Sasa iweje TEC wafanye technical error ya nna hii?
Hoja 8 muhimu za TEC

14. Ibara zifuatazo za Mkataba huu zina matatizo yatakayosababisha nchi kutofikia uhuru wa kiuchumi (economic independence):

14.1. Ibara ya 2 (1): inayohusu lengo la Mkataba huu ambalo ni kuweka utaratibu unaoibana Tanzania kisheria katika kuendeleza, kuboresha na kuendesha bandari zote za bahari na maziwa, maeneo maalum ya uwekezaji, maeneo ya usafirishaji wa mizigo, na maeneo mengine ya kiuchumi.

14.2. Ibaraya 4: inayohusu wigo wa Mahusiano na Utekelezaji unaoitaka Serikali ya Tanzania kuwajibika kuijulisha Dubai kila fursa ya uwekezaji inapojitokeza.Hiiinakinzana na baadhi ya sheria za nchi yetu, kwa mfanosheria ya ushindani na ile ya manunuzi.

14.3. Ibaraya 5: ambapo DPWorldimepewa haki ya kuendeleza, kusimamia na kuendesha miradi pekee yake, wakati Tanzania inabaki na wajibu wa kumwezesha kufurahia haki hiyo.

14.4. Ibaraya 6:inayoitaka Tanzania kuwajibika kuipatia DP World vibali na vivutio vya kutekeleza miradi yake kama Serikali. Hii inapingana na baadhi ya sheria za kiutaratibu.

14.5. Ibaraya 7: inayoitaka Serikali kuwajibika kutoa mamlaka yanayotakiwa na mwekezaji bila ucheleweshaji.

14.6. Ibaraya 8: Haki ya kutumia ardhi ambapo Mkataba unasababisha uvunjifu wa sheria za ardhi na sheria zinazohusu masuala ya ardhi.

14.7. Ibaraya 10: Usiri wa Mkataba ambapo Mkataba unazuia mamlaka nyingine kama TAKUKURU /BUNGE kufuatilia mikataba.

14.8. Ibara za 23 na 24: zenye ugumu wa kujitoa kwenye Mkataba
 
Hakuna usomi wowote. Fatilia performance zao. Mfano Kuna fr mmoja namjua nimesoma naye seminary ana Zero ya pcm alipata point 19. Lakini ni father mpaka leo
Ukiwa na ufaulu wa division III kushuka chini hawakuchukui... Unless ukasome kwanza diploma. Hiyo zero itakuwa ni yako.
 
Mfano Mimi mwenyewe naukubali huu mkataba Sasa iweje TEC wafanye technical error ya nna hii?
Tulia alisema Wana mbeya wanaukubari mwabukusi na watu waliokua wanajaa mahakamani kumsapoti ni wawapi?
 
Back
Top Bottom