Maswali yangu kwa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kuhusu Tamko la Mkataba wa Bandari

We we ni sehemu ndogo sana ya wanaoukubalia huu mkataba wa kihuni
Mimi nimefanya utafiti mitaani,vyuoni,walimu shule ya msingi na sekondari kote huko mkataba hawautaki.90% ya watanzania hawautaki
mimi mtaani sijawahi sikia mtu akiuongelea kwa mema huo mkataba hii inajumlisha hadi wale manyumba kumikumi ambao nishina la chama dola
 
Mbona wamechelewa hizo hoja zao ilikuwa wampe Spika ili zijadiliwe bungeni
 
Nyinyi endelea kukusanya hizo taarifa lakini ndio hivo tena tayari imeenda
 
We we ni sehemu ndogo sana ya wanaoukubalia huu mkataba wa kihuni
Mimi nimefanya utafiti mitaani,vyuoni,walimu shule ya msingi na sekondari kote huko mkataba hawautaki.90% ya watanzania hawautaki
Wewe endelea tu na hao utafiti wako lakini ndio hivo Bandari ndio tayari hiyo imeenda
 
Shida ni hao wabia wa Mkataba Dp world ni warabu waislamu
 
Kweli kazi tunayo watanzania. Kwa mwenendo wa mjadala kwenye Uzi huu unavyoendelea ni dhahiri vimelea vya udini vipo kwa baadhi ya watanzania.

Nafikiri ni bora tungejadili hoja zilizotolewa na wanaopinga mkataba huu kuliko kukazania tu kwamba wanaopinga wanapinga kwa sababu ni wakristo (wakatoliki). Eti kwamba wanaopinga ni wakristo kwa sababu waliosaini mkataba ni waislamu. Hapa tunapotea njia ndugu zangu. Sisi watanzania ni wamoja siku zote tusianze kugawanyika kwa udini. Familia nyingi zimechanganyika kwenye hizi dini. Dini ni imani ya kiroho tusiiifungamanishe na masuala muhimu ya kitaifa.

Itapendeza iwapo kila mmoja atajadili mkataba badala ya kuangaliana dini zetu. Huu ni ugonjwa mbaya mno. Kwa mwendo huu itafika mahali tutachochea vita ya kidini.

Mimi naona serikali ichukue busara ya kuufutilia mbali mkataba huu hata kama inaona unamanufaa. Manufaa yake si kitu iwapo mkataba utakuja kutugawa kidini. Bora tutafute njia nyingine ya kuendeleza bandari zetu. Hii hapana haina mwisho mzuri.

Hapa ni busara, busara na busara tu. Tuache mambo mengine.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Hivi inajielewa kweli? Yaaani mkataba una manufaa alafu Serikali iutupilie mbali?
 
Kanisa gani linahubiri huu upuuzi?usiwaone Catholics kama hao vichaa wanaoshabikia ujinga kuamini kwa sababu raisi wa upande wao hata akifanya baya asishauriwe.

Ktk huo waraka kama umeusoma kuna waliposema hawaitaki DP World?wao wameshauri hata hao waislam wenzako walioenda shule wameshauri baadhi ya vipengele virekebishwe ili wapewe contract ila wewe unakuja na blah blah blahs zako hapa sijui wanahubiri wanafanyaje,Kanisani zinahubiriwa habari za kuacha dhambi na kutendeana mema siyo vinginevyo.
 
Kwa hiyo unakubali turudi kwenye mfumo wa Chama kimoja maana wananchi wengi walitaka tubaki kwenye mfumo wa chama kimoja?
 
Kwa hiyo unakubali turudi kwenye mfumo wa Chama kimoja maana wananchi wengi walitaka tubaki kwenye mfumo wa chama kimoja?
Sijajua umetumia logical gani kutoka ktk post uliyoni-quote hadi ukaja na hoja hii hapo kwenye bold.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…