Mbezi beach, Dar: Jimson Kibiki, apigwa risasi na Majambazi wakati akitoka benki kuchukua hela, wamnyang'anya Mil 4

Mbezi beach, Dar: Jimson Kibiki, apigwa risasi na Majambazi wakati akitoka benki kuchukua hela, wamnyang'anya Mil 4

Acha tu
Kumbe unamfaham nuru?
Sasa mama yake jimmy je?mama anaomboleza yule jamani ukiwa pale msibani hata kama humjui marehem utalia tu ukimsikiliza mama anavyoomboleza!
Kwani huyu Jimmy ni mtu wa wapi? Au asili yao wapi yaan?
 
Nakumbuka mzee Chuma amri ilikuwa ni moja no kuchekeana kamata jambazi piga risasi.
Ukifata sheria ni umkamate umpeleke mahakamani.
 
Kidogo inaanza kutia wasiwasi.

Ni kama mama hakuwemo kwenye serikali iliyokuwa imeyadhibiti haya mambo, na sasa ni kama anatafuta njia zake mpya kabisa kwa kila kitu, jambo ambalo inaonekana inamchukua muda mrefu na kutoa mwanya kwa watu kujifanyia yao.

Hivi polisi nao wamebadili utendaji kazi wao uliokuwa umedhibiti uhalifu wa aina

Samia atalinganishwa na mtangulizi wake katika baadhi ya mambo, na ataonekana hatoshi kabisa!
Kwani kipindi cha Magufuli hakuna mtu sliyepigwa risasi katika ujambazi?
 
Kama nawaona hao watoto wakimuuliza mama yao, baba yuko wapi mbona harudi nyumbani.

Huyo mdada asipopata ushauri nasaha na uangalizi wa karibu anaweza akafanya mambo ya ajabu kwa msongo wa mawazo, au akachanganyikiwa.

Mungu awasaidie na awaongoze.
 
Pumzika Kwa Amani Kaka,Damu Yako Haijamwagika Bure!
Mungu Aishie na Kutawala Atalipa Kisasi Chako.

Familia Hii Namuomba Mungu Aitie Nguvu na Kuifariji Katika Kipindi Hiki Kigumu Kwao.

Wito Wangu Kwa Serikali,Komesheni Hali Hii ya Wizi,Inatia Doa Serikali Iliyosema/Kuapa Kulinda Nchi,Raia Na Mali Zao.
 
Nachukia sana majambazi! Natamani popote walipo wakijulikana wapigwe risasi kabisa hakuna kupelekana mahakamani! Kama mtu anatoa uhai wa mwingine ya nn kumwacha hai!

Natamani IGP atoe amri kabisa kwa askari polisi, palipo na majambazi piga risasi ua kabisa!

Nashindwa kuelewa IGP alikuwa huyu huyu kwann kabla ya samia majambazi hayakuwepo na sasa hv wanakuwepo! Askari ni hawa hawa!

Au kuna hujuma mahali za maaskari? Uongozi wa jeshi la polisi waliangalie hili linawapa doa!
 
Back
Top Bottom