Mbezi beach, Dar: Jimson Kibiki, apigwa risasi na Majambazi wakati akitoka benki kuchukua hela, wamnyang'anya Mil 4

Mmegawana sh ngapi ngapi za mliempiga risasi?
 
Unafikiri huo uliisha. Tatizo ilikuwa nani atathubutu kuripoti?
We babu hata kama unamchukia Mwendazake, kuna vitu haviihitaji ubishi, eti walikuwa hawaripoti. Waulize watu wa Kigoma hasa Kibondo watakwambia ukweli, Sasa walikuwa wanaweza kuishi kwa amani kabla ya huyu Mzee kupita siku Bila duka, nyumba au gari kuvamiwa au kutekwa na majambazi ilikuwa ni Jambo la ajabu. Lakini within these four yrs mambo yalitulia kabisa.
 
wewe mndengereko unajua mgawanyo wa majukumu au umeongea tu pumba hapa.JWTZ hawezi kuingilia kazi za polisi.Hapo kikubwa tuwape rai polisi wetu waendelee na ile mbinu yao 'catch to kill'
Zama hizi kwa ujinga wa polisi wetu tuache kbs kuishi kwa kuangalia majukumu. Polisi wetu ni wezi sana.
 
Pale mlimani city ndio pana hatari kubwa sana.

Ukienda bank za pale bankers wanakuchoresha kwa wahuni

Unafuatwa na boda boda hivi mchana kweupe,,, hawavai mask usoni wala nini..

Utashangaa wanakuambia the exact amount uliyotoa bank (mfano ulitoa 10m bank), njemba zinakuambia tupe ile 10m uliyotoa hapo

Sasa utajiuliza wamejuaje kama ulitoa 10m bank??

Kuna haja ya kuchunguza hawa bankers wanao uza roho za watu kwa majambazi!

kwa namna moja au nyingine ni lazma wanapata maslahi kutokana na ujambazi huo.
 
Daaah kweli mkuu,kauli zake zilikuwa hazIna masihara, nakumbuka aliwahi kuongea mara moja tu kuhusu utekaji wa magari pori la nyakanazi (watumiaji wa barabara hiyo wanapajua)watu walikuwa wanatekwa sana,wanavuliwa nguo zote wanaanza kuimbishwa "mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe"jamaa alisema raia wanaishi kwa hofu ndani ya nchi yao wenyewe wakati polisi wapo Jw wapo inakuwaje eneo linajulikana kuna majambazi wanatamba tu hawakamatwi,hataki huo ujinga!!ikafanyika operation watekaji wakapotea,sasa kwa hali inavyoendelea watu wanapita kwa hofu kwenye lile pori!!!! MAMA NI KIONGOZI MZURI LAKINI AKAZE SAUTI.
 
Hapo raisi hatuna
 
Wewe na mapraivet wenzako wa JW ndo wezi.
Matukio mengi tu askari wachache msio na maadili mnaliaibisha jeshi letu la wananchi. Kesi kibao zimesolviwa kimya kimya kati ya viongozi wa polisi na Jw, pengine hulijui hilo.
Muache ujambazi.
 
JWTZ sio kazi yao kudeal na uhalifu, hiyo ni kazi ya Polisi.
 
Hatujui mkuu saivi kila mtu ashike hamsini zake.
 
Naishi mtaa mmoja ambao wajeda wengi wamejiwekeza kwa kujenga na kuishi, mwizi akikamatwa suala ni moja tu kukatwa robotatu ya vidole vyake vya mikono na miguu na visigino hii ninkwa wezi na wadokozi.

Majambazi huwa hawakatwi vidole wala visigino ni kukatwa roho moja kwa moja.

Wambura hebu onesha ile heshima mama alikupa siku ile akitoa onyo kwa wanaojaribu kujiibua kwenye wiziwizi.

Kwa sasa suala la wizi halipo tena.
 
Sawa, suppose mtoa hela aliwaambia washikaji atakwenda kutoa bilioni moja benki, je aliwaambia ni benki gani? Huu mchongo ni wa wafanyakazi wa benki wenyewe, unaitwa inside job na usikute hata bunduki waliazima toka jeshini au polisi.
vyote vinawezekana
 
IGP ni Yule Yule, tunamwona ni Yule yule
 
Mfano wanaonunua mazao wakulima wa vijijini hawataki mpesa wala acc hawana,inabidi uende n cash hapo ndio pagumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…