Mbwana Samatta ilikuwaje ukashindwa kumhamishia baba yako ‘ushuani’ ukakubali afie Mbagala?

Nakuelewa ndio maana nikacheka
Wenyewe wanasema uache uwanja
Ila kila life style Lina watu wake
Naishi ndani ya geti ,nyumba yangu ila natamani sana kwenda kupanga karibu na kibanda umiza ,au niende mitaa kama makorora huko kwneye vurugu...Mimi siwezi kuishi hizo sehemu hata siku moja ,kama osterbay ,Mbweni .

Siwezi kabisa .
 
#TikiKwaSamia

Kufungua milango ya uwekezaji kwa sekta binafsi kulikofanywa na Serikali kuwaleta na kuvutia zaidi wawekezaji binafsi katika sekta ya bandari kumeleta na inatarajiwa kuleta zaidi matokeo chanya nchini, pamoja na watumiaji wa bandari za Tanzania.
 
Tulimleta mama mdogo mjini kutoka kijijini, alipokaa mwezi mmoja akasema anataka kurudi kijijini maisha ya town hayataki.
Bibi yangu upande wa Baba alivyokuwa mzee sana alikuja Oysterbay Dar kwa baba yangu kutoka Mwanza kwa ajili ya kuwa karibu na huduma za matibabu.

Sasa yeye yale mazingira ya Oysterbay alikuwa hajayazoea kabisa.

Akawa anamlalamikia mwanawe (Baba yangu) arudishwe Mwanza, kwa sababu kule ndiyo kuna ndugu zake wengi, rafiki zake etc.

Basi baba yangu alipata tabu sana kumuelewesha kuwa huku ndiyo kuna matibabu mazuri, huduma za kuangaliwa vizuri etc.

Yule Bibi kuna siku alikuwa anatoka mwenyewe nyumbani anafungua geti anaanza kutembea, eti anataka kurudi kwa mguu kutoka Oysterbay Dar mpaka Mwanza. Alikuwa mzee sana.

Basi tulipata kazi kubwa sana kumlinda kila wakati asiwe peke yake na kuondoka nyumbani.

Wazee wengine wakishazoea sehemu zao ukiwaondoa unawakatia network zao wenyewe wanaona unawazingua tu.
 
Hao wa Mbagala ndio wanao fariki tu na wa Upanga hawafariki?
Mkuu uswahilini wanaofariki ni wengi tena kwakusoa laki moja ya matibabu, Kuna jamaa alifariki kwa kukosa laki moja na nusu ya upasuaji wa mgongo huyo jamaa alikua anafanya kazi ya kubeba mizigo bandarini. Nilivyosikia hivyo niliuzunika sana. Kusikia kijana amefariki kwa kukosa laki moja ya matibabu, Uswahili familia zina maisha magumu na wanarogana sana, sehemu za Waswahili siyo sehemu za kuishi kama wewe siyo mswahili maana Kurogana kwingi sana.
 
Unaliacha tu kama makumbushi unamuhamusha tu kwa kumshawishi
Huko Masaki atacheza bao na nani? Kijiwe cha kahawa atakipata wapi? Kuna maisha ya uswahilini huwezi kuyapata huko Masaki, hasa kwa mtu aliyezaliwa na kukulia uswahilini.
 
Kumbuka pia Mshua alikuwa Afande,,sasa nadhani unajua kauli za "Ndiyo Afande" zinavyokuwaga zinasimamiwa kikamilifu.Ni kama unampigia mbuzi gitaa kwenye misimamo
 
Mtu mwenye cheo cha CP wa polisi alikuwa na uwezo wa kufanya makubwa bila msaada wa mwanae
 
Kama huna bwana jipige kufua mara tatu af sema asante mungu
 
Mkuu,

Kuna watu wameshazoea mazingira yao ukiwahamisha uwapeleke wewe unapoona pazuri wao wanaona tabu.

In any case hayo ni maamuzi ya familia wewe nani uipangie pa kuishi?

Pole kwa wafiwa.
Nakumbuka uliwahi kuweka kisa humu cha mbibi alietoka Mwanza vijijini kwenda kutibiwa Dar, aliboreka kukaa sehemu ya kishua kila siku anataka kurudi kwao huko kijijini 😂

Mtu akizoea mazingira ni ngumu sana kumuhamisha, kuna watu washazoea uswahilini, yale maisha kwao ndio yanawapa utulivu,
 
Unajua mtu ukishaishi sehemu kwa miaka mingi hiyo sehemu kuhama ni ngumu utakuka uliza watoto mpaka wamekua watu wazima ukiambiwa uhame moyo unakataa, yani ata kwawatumishi wa umma utakuta mtumushi kaishi kwenye nyumba ya serikali tokea kija mpaka uzee wa kustaafu umefika siku akiambiwa aondoke kwenye nyumba hanakosa furaha.
 
Watu wanasema eti kukaa ndani ya Fensi ni upweke kumbe ni ugumu wa maisha ndio unawafanya hivyo hivi mtu uwe na uhakika wa Kila kitu upweke unatoka wapi kama stori si unatoka kwenye Fensi unaenda kupiga hizo stori
Kweli Uswahili ni fujo tupu umekaa umelala chimbani watu wanakujq kukaa nje ya dirisha lako wanapiga stori na wamama wanachota maji na wengine wanapika vitumbua. Ukijaribu kwenda kukaa sebuleni napo nje fujo watoto wana piga kelele mara unasika kigodoro kinapita, mara jirani kakodi mziki maspeaker makubwa mziki unapigwa.
 

Shukurani kukumbuka.

Yeah, huyo ndiye huyohuyo marehemu bibi yangu bwana.

Yani alikuwa anahudumiwa kila kitu friji open Oysterbay lakini mwenyewe anataka kurudi Mwanza akae na watu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…