Yes, shida iko kwenye hapo kulazimishana mitazamo.. mie napenda saidia ndugu, ila asiesaidia simlaumu ndio akili yake inamwambia yuko sahihi.
Kuna samaki wamezoea kuogelea kwenye maji mpaka hawayajui haya ni maji, kwa sababu maisha yao yote wapo kwenye maji, hawajui kitu tofauti.
Hivyo hivyo, kuna watu wamezoea umasikini, wanaelea kwenye umasikini, mpaka hawaujui huu umasikini. Wanauona umasikini ule ni jambo la kawaida.
Wanaona jambo la kimasikini kabisa la kumfanya mtoto kitegauchumi cha kumjengea baba nyumba kama ni jambo la kawaida, ni jambo zuri, ni jambo la mapenzi, ni jambo la wajibu, tena kwa wote, si kwao tu.
Watu hawa mara nyingine nataka kuwalaumu.
Lakini mara nyingine najisemea, niwalaumu kwa nini?
Hawa ni watu waliozoea umasikini, ni kama samaki waliozoea maji, hawajui kitu kingine. Hawajui dunia isiyo na maji.
Ukimwambia samaki aliyezoea maji kuwa kuna jangwa la Sahara ni mchanga tu huko, hakuna maji huko, anaweza kuwa mgumu kukuelewa.
Yeye kazoea maji tu, dunia isiyo na maji hata kuifikiria hawezi.
Na hawa watu wako hivyo hivyo.
Wameshazoea umasikini wa wazazi kujengewa nyumba na watoto wao.
Ukiwaambia dunia ambayo mzazi anaweza kujenga nyumba kabla ya kuzaa, wanaona kama unaandika habari za science fiction wasiyoielewa kabisa.
Inakuwa ni kama habari ya kumsimulia samaki asiyejua dunia isiyo na maji dunia ya jangwani ambayo haina maji kabisaa.