Mbwembwe nyingi mitandaoni, lakini makazi ya Baba Mkoani Iringa pa kawaida Sana

📌wewe umethibitishaje km ndo baba ake mzazi?

📌je umefatilia historia yote hakuna sehemu amejengewa tofauti na hapo ulipoona wewe?

📌je unaamini kma pesa za huyo jamaa ako ni pesa za harali?

📌kama sio pesa za jasho harali je unafikili mzee angekubali kuishi ktk nyumba iliyojengwa kwa pesa zisizo harali?

📌je unajua km baaddhi ya wazee wanazo imani yakuwa hapaswi kuishi ktk nyumba nzuri maisha yake yote.?
🤔🤔🤔🤔☝️
 
Sasa kama hana uhakika kwamba huyo ni baba yake, si angejikausha tu asiseme amefiwa na baba na wala asiende msibani?

Bado hujaleta sababu za nikwanini mtoto asimjengee mzazi. Unajificha kwenye kichaka cha, "zipo sababu." Ni zipi hizo sababu?
..mkuu je una uhakika hiyo nyumba aliyokuwa anaishi baba yake ni mbaya kwa kiwango unachosema?.je baba yake aliwahi kulalamika mahali popote kuwa anaishi sehemu mbaya?..maana unaweza kuwa unafikiri makazi mazuri ni majumba makubwa ya ghorofa wakati sio preference ya kila mtu hasa wazee!..watu wengi wa vijijini hasa wazee wanapendelea kuishi mazingira waliyoyazoea na yasiyowafanya waonekane tofauti na wengine wa maeneo yao!..
 
Picha linaanza Kamera na video zinakataliwa,,je kwanini wafanye hivyo? Ni aibu,hata wao nafsi zinawasuta jamii ikijua aibu hiyo

Kuna watu wamesema sijui wazazi wangejenga kwanza kabla ya kuzaa,hivi kuna mtu ambaye hajui maisha ya kawaida ya Mtanzania,sote tunajua wazazi wetu walivyo pambana kutulea tena tukiwa wengi,halafu mngetegemea hapo hapo wajenge makazi mazuri?

Kuna watu mnaongea upuuzi sana,kwakuwa mmetokea kwenye familia ambazo zilipata privilege huko serikalini na wazazi wenu wakajenga nyumba nzuri mnajisahau na kuona wazazi wengine walipata bahati hizo pia

Ni upuuzi kutoa hoja kwamba eti hakuna haja ya kujenga kwenu kwakuwa hilo ni jukumu la wazazi wako,huo ujinga mmeutoa wapi,hivi upo town kweli unaishi vizur halafu wazazi wako wanaishi pabaya unajisikia fresh kabisa?


ACHENI UJINGA
 
Hakuna mahali mimi nimesema nyumba nzuri ni gorofa. Nyumba nzuri inaonekanaga tu mkuu.
 
Hakuna mahali mimi nimesema nyumba nzuri ni gorofa. Nyumba nzuri inaonekanaga tu mkuu.
..mkuu una maanisha nn kusema "nyumba nzuri inaonekanaga"?..kila nyumba ni nzuri endapo tu anayeishi ameridhika nayo..ukija na kigezo cha sijui "kuonekanaga" kuna mtu anaweza kusema hata nyumba unayoishi wewe ni mbaya haifai binadamu kuishi just because amewahi kuona & kuishi nyumba nzuri kuliko unayoishi..!.kukosoa makazi kwa vigezo vya muonekano wakati anayeishi hajawahi kuona shida ni kumkosea mwenye nyumba maana hata nyumba unayoishi wewe kuna watu wanaona haifai kabisa kuishi binadamu kitu ambacho hutapenda kusikia!
 
Mzee Kiranga umemaliza yote niliyotaka kusema. Ubarikiwe sana.
 
Ahaha..We jamaa😄😄
 
Ni lini utamiliki akili???
 
Alikuwa anatamba kwamba amejenga sana kwao?
 
Nani kasema kuwasaidia wazazi ni dhambi?

Mbona mgumu kuelewa mambo hivyo wewe?

Nikikuambia kuwa hilo ni suala la hiyari, suala la maamuzi ya mtu binafsi, suala ambalo hatutakiwi kumhukumu mtu kwa sababu hatujui mahusiano yalivyo ndani ya familia, hatujui hata kama huyo anayesemwa ni baba mtu ni baba mtu kweli, hapo wapi nimesema kujengea mzazi ni dhambi?

Hili si suala la kuniuliza mfano wangu, mimi ninaweza kuwa na falsafa tofauti na mtu anayejadiliwa, na hilo ni sawa tu.

Kwa nini unataka watu wote tuishi sawa?

Waacheni watu waishi wanavyotaka bila kuwahukumu kwa sababu hawana mitazamo sawa na nyie, na nhie muachwe na misimamo yenu.

Huelewi wapi?
 
Sasa kama hana uhakika kwamba huyo ni baba yake, si angejikausha tu asiseme amefiwa na baba na wala asiende msibani?

Bado hujaleta sababu za nikwanini mtoto asimjengee mzazi. Unajificha kwenye kichaka cha, "zipo sababu." Ni zipi hizo sababu?
Hayo ni mambo yao ya familia, mmewavamia watu katika mambo yao ya familia, bila savoir faire.

Unajua savoir faire ni nini wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…