Mchengerwa: Yeyote atakayejaribu kuichezea Serikali hatutamuacha salama

Porojo za nini? Sisi tunataka hoja zijibiwe!

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Sema Baba sema wakusikie,Mama mkwe anachezewa vibaya sema.
 
Waliozaliwa miaka ya 70s katikatika bado wanajiita vijana. Hao wanaweza kusema waliushuhudia utawala wa mwalimu Nyerere maana mpaka anaacha walikuwa na miaka zaidi ya 10 ambao kwa mfano kama alizaliwa 1975 mpaka mwalimu anaacha madaraka walikuwa na miaka 10!
"Sisi vijana tulioshuhudia utawala wa baba wa taifa"!

Hivi kuna yoyote aliyeshuhudia utawala wa Nyerere na bado akabaki kuwa kijana hadi leo?
 
Katiba ya Wananchi sio ya CHADEMA msituletee mambo ya Simba na Yanga hata kwenye mambo muhimu kama haya
 
Kuoa mtoto wa rais wa mchongo anajiona kubwa ni zaidi ya makamu wa rais na waziri mkuu. Huyu na Mwigulu ndio washauri wa wakuu wa bi tozo
 
Wewe una akili ndogo sana, kwa ujinga wako unaona katiba ingeinufaisha Chadema! Haujui kuwa siasa ina kiwango kidogo sana kwenye katiba huku asilimia kubwa inahusu maisha yangu na yako ys kila siku, wewe ni kati ya wale wanaoona fahari kuitwa watumwa.
 
sasa huyu ndiye anayeharibu amani sasa. anamtishia nani? yeye ndiye mmiliki wa nchi hii, nchi hii ni mali ya familia yake? anaposema hatawaacha watu salama na wao wakisema hawatawaacha maccm salama patatosha? huo ndio utawala wa sheria, kwamba hautawaacha watu salama yaani utawadhuru badala ya kuwapeleka kwenye vyombo vya kisheria? anafikiri kwa kauli hii watu wanamuogopa? kwani ni mara ya kwanza watu kutoachwa salama? watu walipotea na kuumizwa kipindi cha magu na bado waliendelea kusema ukweli anafikiri watu watamwogopa yeye?
 
Huwa ninamheshimu sana, sikujua nate amekuwa na akili za mkwewe
 
Yuko kwake,alitimiza wajibu wake na huyu atatimiza huo wajibu kisha kijiti kwa mwingine.

Uongozi ni dhamani huwezi Kaa kimya watu waharibu Nchi kisa eti kesho hutokuwa Kiongozi tena, upuuzi
Kwahiyo kumbe ni mkwala tu wa kawaida ili asionekane kakaa kimya.
 
Watu wakirudisha kadi za kijani CCM wanafikiri serikali inaelekea kupinduliwa. Japo huyu sijamwelewa ama mada ya ugaidi?
 
Huenda katumwa na mama mkwe, sisi hatujui bhana....
 
Tatizo akiongea inaonekana kana kwamba anasukumwa na maslahi yake binafsi ya kifamilia badala ya yale ya wengi Yaani Umma wa watanzania.

Ako na conflict of interest.

Uhalali wake wa kunena unakuwa impaired sababu hayuko huru yuko biased .?!
Hilo swali ndio jibu lenyewe$
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…