Pole mwanangu dahh!!! Na yeye alikuwepo wakati unaambiwa hayo yote?? Ilikuaje mpaka akaamua kukushtaki kwao badala ya kwenu?
Mwanangu hapo tembea tu, achana na hiyo kitu au endelea lakini pull off.
Hao wakishua, au kama alivyowaita, “get kali”, watoto wa Daddy this, Daddy that… Daddy hivi, Daddy vile...mimi sishangai sana alivyoshitaki kwao, a.k.a. kwa Daddy. 😅
Issue ambayo kwa kawaida inaweza kuonekana ndogo na ya kuvumilika kiuswazi au kiutawala, kwao inaweza kuwa kubwa sana. Kwa hiyo usishangae sana kwa nini amefikia hatua ya kushitaki.
Unaweza kusikia, ukameza tu na kuishia kucheka. 😂 Lakini unajua nini, kwa mleta mada? Vumilia tu. Remain strong, like nothing happened. Tunaelewa kabisa jinsi inavyouma, lakini usiruhusu hilo likuvunje moyo.
Endelea kujipambania mpaka ufikie lile lengo lako kubwa na mafanikio makubwa ya kiuchumi. Kwa sababu kwenye maisha, mafanikio ya kiuchumi hayana kikomo.
Wakati huo huo, jiandae moyoni kwa lolote. Maisha yana options nyingi sana. Usijibane sana kwenye option moja tu, kwa sababu huyo mtu huenda asiache kuwa na hicho kiburi anachopewa na mazingira na wazazi wake.
Kwa hiyo, kuendelea kumtegemea yeye abadilikе kunaweza kuwa ni kujichosha nafsi yako na kujiongezea maumivu moyoni. Focus on yourself, build yourself, and keep moving.
Zaidi ya yote, nakutakia mapambano mema. You’re gonna win this battle. Kwa sababu mentality ya battle yako umeshaielewa 💪