Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msianze kuhangaika tunazungumzia kuvunjwa kwa mkataba na ni nani alihusika kuuvunja ndiyo msingi wa mjadala.

Tundu Lisu "Kibaraka wa wazungu" amesema aliehusika kuvunja mkataba ni raisi John Magufuli wakati akiwa ni waziri wa ujenzi na ushahidi wote upo umehifadhiwa.

Ila mkataba ulivunjwa mwaka 2009 na serikali huku Dr Kawambwa akiwa waziri husika.

Ukianza kuzungumzia mwaka 2010 rufaa ilipokatwa unakuwa unaanza kupotosha umma.

Yaani unaonekana unababaika.

Haya mambo hayataki pupa bali ni mwendo mdundo.
Du bado kunawatu wanashupaa tu kutetea ujinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni dhahiri ya kwamba huyo mtu TL anatumika na makampuni yanayonufaika sana kwa wizi warasilimali zetu, na baadhi ya watumishi wa umma na baadhi ya wana ccm kuichafua,kuipinga na kuidhoofisha SERIKALI YA SASA YA CCM. Nina ushahidi wa kutosha juu hujuma hii. Ambaye ataona nimevunja haki yake anipeleke mahakamani.
TL anafanya kazi hii kwa malipo,siyo bure. CCM wanawafahamu hao WASALITI. Iwaanike hadharani na kuwatimu. We cant let things go wrogly like that.Watumishi wa umma wanaofanya kazi ya kutoa taarifa za serikali watafutwe na kutumbuliwa kwa wakati.
Kumbe kuna wasaliti wanaotoa taarifa za serikali? Na ndo wanaompatia TL? Kumbe taarifa alizotoa TL ni sahihi kwa sababu amepatiwa na wasaliti? Then, no dhambi watu kupatiwa taarifa sahihi na TL?

OK! Kuhusu makinikia TL hajawaonya before? Mmepewa notisi na ACCACIA sasa tusubiri. Yakitufika utakuwa ni ujinga wa TL?

Vibaraka ni wale wanaowatengezea dili wazungu ili wapate mgawo wao baadae. Na hawa si ndo nyie mnaohangaika na TL kweli? Mnakatisha mikataba wakati mkijua baadae mtawalipa pesa kubwa na nyie mfaidike.

Kama ni kweli basis 'Shame on you all.'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu fikiria mtu unamwita raisi wako hilo neno eti kwasabau tu unatumia Kompyuta ukiwa nje ya Tanzania.

Ni hasira gani hiyo uliyo nayo juu ya huyu kiongozi?

Kila binadamu ana mapungufu yake na hata wewe ungekuwa kiongozi leo ni lazima ungekuwa na kasoro zako.

Lakini kwa hii ya name calling umekwenda too much step brother/ sister.

Tafakari.
Sizani kama ni tusi kama unavyotaka kutuaminisha....ni sawa na kumwita mtu kwa kabila lake

au unaogopa neno nigger....maana yake ni watu wenye ngozi nyeusi chini kusini mwa jangwa la sahara.

na chato ni sehemu anayotokea huyo mtu mweusi kusini mwa jangwa la sahara.

hakuna hoja nzito juu ya malalamiko yako unless unataka kutuaminisha kuwa rais katukanwa.

kwa mujibu wa vipimo vya mkemia mkuu
 
9ca0c18738e25b87b99c24b2d51edbb8.jpg
daah sijui alikuwa nani
 
Ni dhahiri ya kwamba huyo mtu TL anatumika na makampuni yanayonufaika sana kwa wizi warasilimali zetu, na baadhi ya watumishi wa umma na baadhi ya wana ccm kuichafua,kuipinga na kuidhoofisha SERIKALI YA SASA YA CCM. Nina ushahidi wa kutosha juu hujuma hii. Ambaye ataona nimevunja haki yake anipeleke mahakamani.
TL anafanya kazi hii kwa malipo,siyo bure. CCM wanawafahamu hao WASALITI. Iwaanike hadharani na kuwatimu. We cant let things go wrogly like that.Watumishi wa umma wanaofanya kazi ya kutoa taarifa za serikali watafutwe na kutumbuliwa kwa wakati.
Kweli mkuu! Inabidi serikali iwatafute kwa udi na uvumba ili kuangamiza kabisa maadui wa nchi yetu!
 
Nasema kuwa Tundu Lissu asiombe radhi.

Wakati rufaa iliyokatwa na serikali ikitolewa hukumu dhidi ya kampuni ya ujenzi tuliyovunja kandarasi yao, nani alikuwa waziri wa ujenzi?

Kifupi Kawambwa baada ya kuvunja ule mkataba serikali iliposhindwa kesi kwenye mahakama ya ICSID ilikata rufaa na hukumu ikatolewa kuwa tumeshindwa.

Hukumu hiyo ilitolewa wakati Rais John Pombe Magufuli akiwa tayari waziri wa ujenzi, je anayestahili kubeba jukumu hilo ni Kawambwa?
Tusipende kutafuta siasa nyepesi kwenye mambo mazito!

Halafu anayeandika umakinikia huu wa mawazo ni mtu anajitambulisha kwa jina la Dkt eti ni msemaji wa serikali. Hii ni aibu kubwa kwake binafsi kwa kuidhalilisha taaluma kama kweli nayo, na aibu kwa aliyemteua na fedheha kwa taifa. Jambo liko wazi kabisa halafu tunalikingia kifua kisichohitajika. Nadhani kuna mahali nchi hii tumekosea. Athari zake zitakuwa ni kulipa madeni makubwa kwa amri za hukumu za mahakama za usuluhishi kuliko kujenga uchumi wa vi-wonder!.
 
Sizani kama ni tusi kama unavyotaka kutuaminisha....ni sawa na kumwita mtu kwa kabila lake

au unaogopa neno nigger....maana yake ni watu wenye ngozi nyeusi chini kusini mwa jangwa la sahara.

na chato ni sehemu anayotokea huyo mtu mweusi kusini mwa jangwa la sahara.

hakuna hoja nzito juu ya malalamiko yako unless unataka kutuaminisha kuwa rais katukanwa.

kwa mujibu wa vipimo vya mkemia mkuu


Mbona hili jambo limemalizwa huko juu?

Tuendelee tu na kujadili mada husika.
 
Wakati fulani hapa chamani tulikuwa na watu waliojulikana kama wanasheria wa chama na ninamkumbuka mmoja akiitwa Kunambi. Lakini zama hizi sijajua kama bado tunao wanasheria wa chama, ila ningeomba tupate mtu mwenye uwezo wa kujibu na kujenga hoja zitokanazo na changamoto mbalimbali. Haiwezekani leo hii Lissu au Zitto wanaibuka na hoja nyepesi zenye majibu ya kawaida lakini sisi kama chama tunabaki kimya. Leo hii Lissu anawaaminisha watanzania kwamba serikali ikiingia mkataba ni mwiko kuhoji au kuuvunja kwa sababu nchi itashtakiwa, na sisi CCM tumebaki kimya tukumbuke kuwa Lissu ni mwanasiasa na anaongea mambo yote kupitia chama chake chadema, hivyo anapaswa kujibiwa kisiasa na chama kilichounda serikali yaani CCM. Ahsante!
Suala hapa ni kuwa mnapoamua kuuvunja mkataba huo mmejiridhisha kuwa mmetenda hivyo kisheria kulingana na matakwa ya mkataba huo? Nina hakika kila mkataba una jinsi ya kuuvunja pale inapoonekana mambo hayaendi kama yalivyokubaliwa. Au ninyi mnatumia tu ubabe?

Hapa Lissu mnamwonea bure tu. Maana si kwamba anawaaminisha watu hicho anachosema, watu wanayo haki ya kuamua kuamini au la. Na hukumu iliyowapa ushindi hao tulioingia nao mgogoro haikuamriwa na Lissu, na wala sidhani kama Lissu alisimama kama wakili wa hao jamaa. Kwa maana hiyo, inaelekea tulivunja mkataba huo hovyo hovyo ndiyo maana tumepigwa chini.

Na tuivyo na akili nyingi, hata baada ya kukata rufaa na kupigwa chini tena, wakubwa wetu wakaamua "kutumia ubabe" kutolipa deni hilo hadi sasa bilioni 40 zimezaa 50 na kuwa bilioni 90.

Pamoja na yote, bado tunamshambulia Lissu kuwa katutwisha deni hili. Mbona mnampa Lissu some supernatural powers?

CCM tuna akili nyingi.
 
John Magufuli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli



5th President of Tanzania
Incumbent
Assumed office

5 November 2015
Vice President Samia Suluhu
Prime Minister Kassim Majaliwa
Preceded by Jakaya Kikwete
Minister of Works, Transport and Communication

In office
28 November 2010 – 5 November 2015

President Jakaya Kikwete
Preceded by Shukuru Kawambwa
Succeeded by Makame Mbarawa
In office
November 2000 – 21 December 2005
President Benjamin Mkapa
Succeeded by Basil Mramba
Minister of Livestock and Fisheries Development

In office
13 February 2008 – 6 November 2010


Preceded by Anthony Diallo

Succeeded by David Mathayo David

Minister of Lands and Human Settlements

In office
6 January 2006 – 13 February 2008

President Jakaya Kikwete
Succeeded by John Chiligati
Member of Parliament for
Biharamulo East and Chato
In office

November 1995 – July 2015
Succeeded by Kalemani Medard
Personal details
Born
29 October 1959 (age 57)
Chato, Geita, Tanganyika
Nationality Tanzanian
Political party CCM (1977–)
Spouse(s) Janeth Magufuli
Children
Joseph Magufuli

Jesca Magufuli
Residence Ikulu, Dar es Salaam
Alma mater University of Dar es Salaam
Profession Teacher
Nickname(s) Tinga tinga (The Bulldozer)[1]
Twitter handle MagufuliJP
Military service
Allegiance
20px-Flag_of_Tanzania.svg.png
United Rep. of Tanzania
Service/branch National Service
Years of service July 1983–June 1984
John Pombe Joseph Magufuli (born 29 October 1959) is the President of Tanzania, in office since 2015.

First elected as a Member of Parliament in 1995, he served in the Cabinet of Tanzania as Deputy Minister of Works from 1995 to 2000, Minister of Works from 2000 to 2006, Minister of Lands and Human Settlement from 2006 to 2008, Minister of Livestock and Fisheries from 2008 to 2010, and as Minister of Works for a second time from 2010 to 2015.[2]

Standing as the candidate of the ruling CCM, he won the October 2015 presidential election and was sworn in on 5 November 2015




MBONA WAKATI MKATABA UNAVUNJWA HAKUWA WAZIRI WA UJENZI???????
 
Tafakari kwa kina yawezekana Mimi na wewe ndo mbwa wenyewe "tunaoswongomela" mahitaji ya "watoto".Sijamlenga mtu.Ila kwa staili na namna yotote ile ukishindwa kujali ustawi wa watanzania wenzio na Taifa kwa ujumla wake basi huna tofauti na mbwa wanaopewa tafakari katika mada hii.
Shida inaanzia pale MTU mkubwa anapowadhihaki kwa vijembe na maringo wapinzani. Hata Kuwaita vilaza na wanasheria uchwara. Na jamii inaaminishwa kua wao ndio mafisadi waliokosa ajenda nk.

Wapinzani wanapoliamsha "DUDE" wanaonekana sio Wazalendo.

SASA UZALENDO UNAPIMWAJE?
KWA KULETEA HASARA TAIFA AU KUKOSOA UONGOZI UNAOSABABISHA HASARA KWA TAIFA?

..Pambana na hali yako..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini umelitumia hilo andiko ktk masuala ya kuzuiliwa kwa mabilioni ya Tz nchini Canada...????

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimelitumia ili wenye masikio wasikie na wasielewe kuwa wao ndio tatizo na badala yake waendelee kuwaona wabaya ni wale wanaohangaika na kulinda chakula cha watoto. Nimelitumia ili wasikiao wasikie hayo niliyonena na kisha mwangi wake upasue masikio yao.

Nimelitumia andiko hilo,ili wale wenye tabia za kusoma mambo huku wamevaa miwani ya mbao iliyopakwa mkaa wasione maandishi vizuri na hata wakiona wayaone maandishi Kichwa chini miguu juu na hata ikilazimu yakisomeka kutoka kulia kuelekea kushoto.
 
Back
Top Bottom