Mtoto wa shangazi ana kiburi kwenye kufata sheria zangu nyumbani kwangu, nitatue vipi?

Fukuzilia mbali hiyo takataka,yanini kujipa masononeko yasiokua na maana.
Ama mpe mambata tu kila unapomuona anafanya hivyo ataondoka mwenyewe.
 
Acha kumhenyesha huyo dogo, aisee Watanzania mbona tunapenda kupeana tabu katika haya maisha? Yani mtu ukishakuwa na mji wako basi utataka kila anayekuja umuhenyeshe kwa namna flani!

Kama ulishampa muongozo ila hataki kufuata inatosha we usimlazimishe. Acha tu aishi anavyoona sahihi maana anaelewa kabisa yupo kwa kaka yake na sio kwao.
 
Naona kuna watu wanadhihaki na wengine ku-support kinachofanywa na huyo dogo. Wengine wanapinga utaratibu wa mleta mada. Lakini haohao siku si nyingi watarudi hapa kulalamika kwamba walikwenda halmashauri kutaka huduma lakini muhudumu yuko buzy anachezea simu. Watatoa mapovu hapa mpaka display zetu chapachapa. Watanzania bado hatuelewi.
Keep up the good job kaka. Adabu ndio msingi wa mambo mengi. Ongea na shangazi kwanza kabla hujambana. Ukipata support go ahead. Ikishindikana tafuta namna ya kuwaelekeza wanao wasifate tabia za huyo dogo. Nakuhesabu kama mjenzi wa kweli wa taifa. Mwalimu alisema ujenzi wa kweli wa taifa ni kuwekeza kwa watu na siyo mabarabara. Vitu vyenyewe ni kama hivyo. Discipline, adabu.
 
Unawaekea watu sheria unadhani wamekua ...Ng’ombe au mbwa wako , acha ushamba na ulimbukeni wa kuiga komaa na familia yako huyo ana 20 yrs unajua ana mitazamo gani , BEBERU tumia busara. Hii ni karne ya 21
 
Mpe muda,mazoea yana tabu,
Imagine we uende kwa shangazi alafu akawambie ndani kwake kulala ni saa1 jioni wote,utaweza?
Naamini mwanzo utapata tabu ila badae utazoea na kuadopt so mpe muda nae dogo huyo!
 
Anza msako wa kukagua simu kwa kila anaeenda kuketi mezani kabla ya chakula atakayebainika huyo atakula simu kwa siku hiyo mbona atanyooka tu, kama hataki arudi kwao au akajitegemee si ashafikisha umri wa utu uzima huyo....

Ila sheria zingine bwana ni miiba kwanza yeye kuchezea simu kunakusababisha usishibe au?? Utakuwa na hulka za uchoyo wewe.
 
Ukiona hivyo ujue hamna mazoea kihivyo.

Mtoto anakula Hana wa kupiga naye Stori hivyo anakuwa bored. Simu ndio inampa kampani.

Wakati WA Kula jaribu kumpisha Stori Kwa kumpa mada za kuchangia Kama vile mpira, muziki, n.k.

Hata Mimi ningekuwa kwako wakati WA Kula alafu sina wakupiga naye Stori huenda ngefanya hivyo hivyo.

Alafu chukulia huyo Kwa sasa ni mtu mzima, miaka 20 ni mingi.

Sio ulete sheria za wakati Kula hakuna kuongea ukadhani kanuni hiyo inatumika Kwa watu wazima piah
 
Ni bora kuwa mkoloni utawale na kuongoza nyumba yako kuliko kuwa mtumwa kwako mwenyewe.
Kuna vitu vidogo vitawatoa roho, sasa ukoloni hata kwenye vitu vidogo tu simu mnataka mtengeneze makanuni utafikiri katiba ya nchi, nini wazee kweli binafsi sioni la msingi hapo, mtafanya watoto wenu wawe waoga nakukosa amani wakimuona baba karudi.. Na familia tajiri hutakuta ujinga wa hivi
 
Kuna watu wana roho za kutu... Mimi sijawahi kuona Kwenye familia zilizoendelea mambo kama haya... Masheria ya kiduanzi utafikiri yanafanya familia iwe imara kumbe ni upupu tu, kwanza wanafanya watoto wawe waoga na kukosa amani wanapomuona baba mzee wa masheria
 
Sherisheria za nini, mambo ya kiswahili Swahili ni ujinga uliopitiliza.
Unaweza sheria nyumbani ili iweje? Ishi maisha ya amani vingine vyote vitaenda.
Mara sijui hakuna kushika simu mara sijui tukae pamoja, Ni ulimbukeni na uswahili wa kizamani.
Mimi ningekua huyo mtoto wa shangazi, ningekufurahisha na hakuna rangi ungeacha kuiona hata Kama upo kwako.
Ningekunyoosha hadi naondoka hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…