Mungu wa miujiza mbona sijawahi kumwona? Au kuona miujiza yake?

Kwamba ilikuwa ni biashara ya kuteka imani za watu katika yasiyo onekana?
 
Je unaweza kutrace uwepo wa Mungu katika haya uliyo ya andika kwamba nikikaa tokea asubuhi mpaka jioni nitajua na kuona uwepo wa Mungu?

Na utajua je kuwa kuna creator just by observation?
 
Asante kwa tathmini hii, ndo maana unaambiwa Mungu hayupo nje yako,

Mungu ni awareness ya kujua kitu kina affect maisha yako... Kwamba kuna planes of awareness unakuwa umefikia karibu na God's consciousness.

Je, unaongelea je hii dhana ya watu kuamini kuomba kitu kilicho nje yako na kuponywa? Hii imekaaje? Unadhani kuomba kuwa kuna mtu au kitu kinakusikia nje yako kunasaidia?
 
Dini ni utaratibu wa maisha tu ambapo tumewekewa mtawala ambaye hakuna wa kumuhoji wala kumkosoa. Yeye ni alpha na omega ila hayupo.

Kila jamii ina dini zake na Mungu wake. Tatzo linakuja kwetu sisi badala ya kuabudi babu yako wa kishumundu unaabudu babu wa waisrael Yesu na babu wa waarabu Mohamedi.....
 
Lengo la mtihani ni nini mkuu
Haha jinsi tunavotita mtihani huenda tunakosea? Ila yawezekana ni mtihani maana Avery thing you do needs some sort of figuring things out, hauwezi kujua pasipo experience yenyewe
 
Reactions: Lax
Okay, sasa je huyo aliye nyuma ya pazia ni Mungu na muumba na muwe a wa yote aliyesema tukimwomba atatuponya?

Kama ni kweli je ni kwanini amejifiicha na itokee hata mara moja kujidhihirishfor the betterment of us believers?

Kwanini tukeshe tukio ba kwa kitu kilicho jificha?.

Huoni kuwa tunajidanganya tu, kwa stori za kale ambazo haazijirudii?
 
USIPOTAKA KUMUONA, HUTOMUONA!!!
 
Mungu alishaziumba nafsi zote za waja na zote akazikushanya sehemu moja na zikakiri kwamba hapana mola mwingine isipokuwa YEYE...kisha akazibainishia njia njema na potovu...kisha akazipa uhuru wa kuchagua njia inazozitaka.

Mungu hapendi uchafu wala kufuru.

Nafsi italipwa kile ilichochagua katika maisha haya ya dunia.
 
Maisha ya dunia ni Mtihani wa imani.
Mungu ametuleta hapa duniani kutujaribu imani zetu juu yake na si kwamba alikuwa hajui nafsi zetu toka hapo mwanzo kuwa nini zitakuja kufanya hapa ulimwenguni. La hasha anajua ya nyuma na mbele yetu ila kuna hekima alitaka kuifanya. Nayo ni

*Kudhihirisha Ushahidi Dhidi ya Mwanadamu (Uadilifu wa Kiungu).

Mwenyezi Mungu anajua tangu mwanzo nani atafanya wema na nani atafanya uovu kwa sababu Yeye ana ujuzi wa mambo yaliyopita, yaliyopo, na yajayo (Ilm al-Ghaib). Hata hivyo, humpa mwanadamu uhuru wa kuchagua na kufanya vitendo hivyo ili:

• Ushahidi uwepo: Siku ya Kiyama, mtu asihukumiwe kwa kile ambacho Mungu alikuwa anajua angekifanya, bali ahukumiwe kwa kile alichokifanya yeye mwenyewe kwa mikono yake.

. Kama Mungu angewapeleka watu motoni au peponi kabla hawajaja duniani kwa kisingizio cha "Najua mgefanya hivi," wanadamu wangepinga wakisema: "Mbona hukutupa nafasi ya kujaribu? Tungefanya wema!" Dunia ni uwanja wa kudhihirisha vitendo hivyo ili mtu asione ameonewa.


Na jambo la kusema kuwa Mungu katuleta duniani ili atujaribu aone nani mwenye vitendo vyema haimaanishi kuwa Mungu alikuwa hajui nini tutakuja kukifanya hapa duniani.

Msingi hapa si kwamba Mungu anajifunza kitu kipya ambacho alikuwa hakijui. Badala yake, maana yake ni: "Ili kukuwekeni katika hali ambayo sifa zenu halisi (za wema au ubaya) zidhihirike wazi machoni penu na machoni pa viumbe wengine."

• Ni sawa na mwalimu anayejua darasani kwake nani ni mwanafunzi hodari na nani ni mvivu. Lakini mwalimu hawezi kutoa maksi au kufelisha mtu bila kutoa mtihani wa karatasi. Mtihani huo unalenga kudhihirisha ukweli wa uwezo wa mwanafunzi kwa vitendo.
 
Pia uelewe kuwa Mungu ni mfalme.hivyo apokei amri,ushauri wala mapendekezo kutoka kwa yeyote...YEYE anafanya alitakalo.

Alishaamua kuwa wanadamu wala majini tusiweze kumuona katika maisha haya ya dunia. Imagine tungekuwa tunamuona Mungu ni nani angekufuru, nani angempinga Mungu...? nadhani dunia nzima ingekuwa na wachamungu...Ila kaamua tusimuone ili aone tutamuamini pasi na kumuona.? Ndio tunarudi ile kauli ya kwenye Quran kuwa...tumeumbwa ili tuje kufanyiwa majaribio.

Kitendo cha Mungu kuonekana kusingekuwa na maana ya kuumbwa Pepo na Moto, Kusingekuwa na maana ya kifo, kusingekuwa na maana ya uwepo wa siku ya Qiyama n.k
 
Anayezaliwa leo hii viungani hapo vatican, na anayezaliwa leo hii viungani hapo mecca. , huwezi sema wana chance sawa, wewe unaona wanachamce sawa hawa?

Yani mtu azaliwe sudan, gaza au hata viunga vya kongo hapo useme wanachance sawa na wengine
Kwenye Quran, Mungu amesema kuwa hamdhulumu mja bali mja hujidhulumu mwenyewe.

Swali lako linalenga kugusa dhana za uadilifu wa Mwenyezi Mungu (Al-Adl), uhuru wa kuchagua (Free Will), na jinsi binadamu anavyohukumiwa katika Uislamu.

Kijuujuu, inaweza kuonekana kama mtoto wa Kiislamu amependelewa. Hata hivyo, vyanzo vya Kiislamu (Qur'ani na Hadithi) vinaonyesha kuwa nafasi na fursa za kupata radhi za Mungu ziko sawa na kwa usawa kabisa, kwani kila mtu anahukumiwa kulingana na mazingira na kiwango cha maarifa alichopewa.

Kuna misingi minne inayofafanua usawa huo ila sitaki andiko liwe refu, nitakupa misingi miwili ya uadilifu wa Mungu katika jambo hili

1. Kila Mtoto Anazaliwa Katika "Fitrah" (Maumbile Safi ya Kiislamu)

Katika Uislamu, hakuna mtoto anayezaliwa akiwa Mkristo, Myahudi, au Mpagani. Kila mtoto anazaliwa akiwa na mwelekeo wa asili wa kumtambua Mungu mmoja (Fitrah). Mazingira na wazazi ndio wanaombadilisha baada ya kuzaliwa.

Kutoka kwenye Hadithi:

Mtume Muhammad (S.A.W) alisema:
"Kila mtoto anazaliwa katika maumbile safi (Fitrah), kisha wazazi wake humfanya kuwa Myahudi, au Mkristo, au Majusi (Mwabudu moto)..." — (Sahih al-Bukhari)

Hii ina maana kwamba machoni pa Mungu, watoto wote huanza mstari mmoja wa mwanzo wakiwa wasafi na sawa kabisa.

2. Kanuni ya "Hukumu Kulingana na Viwango vya Mtihani"

Mwenyezi Mungu habadilishi kanuni ya mtihani; anatoa mitihani tofauti lakini kwa uadilifu ule ule. Mtu aliyezaliwa kwenye mazingira ya Kiislamu ana mtihani tofauti na yule aliyezaliwa kwenye mazingira ya Kikristo:

• Mtihani wa Mtoto wa Kikristo: Mtihani wake ni "Kutafuta Ukweli" (The Test of Seeking Truth). Ikiwa atatumia akili yake vizuri, akahoji, na kutafuta ukweli kwa nia safi, Mungu humwongoza. Katika Uislamu, mtu anayetoka kwenye dini nyingine akasilimu hupata thawabu mara mbili (kwa mujibu wa Hadithi katika Sahih al-Bukhari), kwa sababu ya juhudi kubwa aliyofanya kupenya vikwazo vya kifamilia na kijamii.

• Mtihani wa Mtoto wa Kiislamu: Mtihani wake ni "Kulinda na Kutenda" (The Test of Preservation and Action).

Kuzaliwa Mwislamu hakukuhakikishii kwenda Peponi. Mara nyingi, watu wanaozaliwa kwenye Uislamu huchukulia dini kama mazoea (cultural Muslims). Mtihani wao ni mkubwa zaidi kwa sababu tayari wanajua sheria lakini wasipozifuata, au wakifanya madambi kama unafiki, adhabu yao inaweza kuwa kali zaidi kwa sababu walikuwa na elimu lakini hawakuifanyia kazi.
 
yote kwa yote suala la mungu tumezaliwa tumekuta hadithi za uwepo wake the same na mababu zetu ambao wamefaliki hatujawakuta mfano leo hii ukiambiwa uthibitishe kama walikuwepo ilihali hujawaona
 
Mungu yupo ila sio kama wanadamu wanavyomfikiria.
 
HAyo unayoyasema wewe unaona yanatekelezeka mpaka mwaka huu wa 2026, yametekelezeka kwa kiwango gani
 
Mashairi mazuri
 
There is no first event, no start, and no uncaused beginning
Doesn't that prove kuwa Mungu ni alpha na omega...

Kama ilivyo energy isiyo weza kutengeneza wala kuvunja bali hubadilisha form moja kwenda nyingine?
 
Maisha yako tangu kuzaliwa hadi sasa ni muujiza mkubwa kuliko hiyo unayoitafuta.

Mshukuru na Kumtukuza Mungu kwa kkila hatua ya maisha yako. Wengine wameishia njiani na wengine ghafla mno wakiwa wanatembea.

Be Thankful to Thee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…