white hat
JF-Expert Member
- Dec 16, 2016
- 3,321
- 2,488
mwenge wenyewe ni uchawi tosha sasa Anayeupenda lazma awe mchawi au kama sio mchawi atakuwa kalogwaanaeuchukia mwenge atakua mchawi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mwenge wenyewe ni uchawi tosha sasa Anayeupenda lazma awe mchawi au kama sio mchawi atakuwa kalogwaanaeuchukia mwenge atakua mchawi
hawezi kudhibitisha kwa sababu yeye sio mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikaliUnaweza kudhibisha " hiyo bajeti ya bilioni 400 kuwa ni sahihi.!
umeandika ujinga gani hapa kenge we!Mnaoupenda Mwenge ndiyo mmekubuhu kwa uchawi na Mauaji.
ina maana hujui faida za mwenge? MWENGE unakuza sana uchumi kwa mfano kila sehemu unapokwenda wiki moja kabla haujafika wajasiriamali wanakusanyika sehemu utakapolala wanafanya biashara kuanzia mama ntilie,wauza vinywaji , nguo n.k unakuza sana uchumi wa nchi na miradi mingi ya maendeleo inazinduliwaMwenge ulipofikia ni kama phrase ya 'Beauty is in the eyes of beholder' ni special kwa serikari tu hila unapoteza maana kadri siku zinavyoenda na support ya walipa kodi. Wakati as national symbolism za freedom na umuhimu wake kwa taifa it bears huge significance.
Tatizo la mwenge ni jinsi unavyouzwa kwa walipa kodi kwa wengi ni kuukimbiza tu na kufungua miradi mahala unaposimama bila ya kujua mantiki yake haswa. Lets face it kama ni kufungua miradi kila siku viongozi wanakata ribbon bila ya mwenge kukatiza so what special with mwenge; na hapa ndio tatizo lilipo.
Kwa wenzetu vitu kama hivi propaganda za utaifa zinafanywa kwa jicho la hoteliers na huduma zao, uwezi kutoza kulala sh 200,000 kwa siku na mwingine akatoza sh 30,000 kwa huduma ambayo ni perishable kama umeweka kitu tofauti ni lazima yule anaenunua hiyo huduma aielewe sio wewe uliobuni hiyo huduma. Na ndio sababu watu wanaenda to great length with SERVQUAL methods to show why they are different from 30,000 sh night sleep to justify their hidden special services which enhances your overnight stay.
Ndio tulipo umeweka budget ya sh 400b as yet hakuna promotion campaign zozote za umuhimu wake as a symbol ni mwenge tu unakimbia ovyo watu wanabadilishana, kulazimishana kuupokea kwa kusimama barabarani without awareness to the meaning. Wenzetu wanatumia hela nyingi sana kwenye media programs kuonyesha significance ya national ritual na umuhimu kwa nationalism, ni nini wanachokubushana na hiyo ritual kama taifa. Ndipo hela inapoenda huko kuliko kweye posho za viongozi kwa sababu walipa kodi lazima waelewe sababu za gharama zingine zinazotumika kwenye hizo ritual.
Sasa kumwita Dr Bana sijui Humphrey Polepole kwenda kutoa simulizi sio propaganda, you need clever programmes za wanachi unapopita na maelezo yake unaamasisha vipi maendeleo sehemu tofauti with moving images, you need historical anecdotes programs the sort of 'Mohammed Said' stories to invoke emotions za wazee na mambo mengi luluki propagandists wanayotakiwa kufanya kuweza ku justify matumizi na kuufanya mwenge uweze kuonekana muhimu na kupata support ya kujitakia sio kulazimishana.
Habari wadau!
Leo Makamu wa rais Zanziber kazindua mbio za mwenge wa uhuru wakiwa na kauli mbiu ya maendeleo ya Viwanda.
Naomba anaye fahamu umuhimu wa kukimbiza mwenge na matumizi ya zaidi ya bilioni 400.
Nini faida yake?
Kimsingi, Mwenge unatumia gharama kubwa mno, kiasi kwamba fedha hizo zingetumika kufanya shughuli za maendeleo, baadhi ya kero kwa wananchi ama zingekwisha au kupungua kwa kiasi kikubwa.
Inashangaza kuona kuwa Mwenge ule ulikabidhiwa katika eneo la shule ambayo haikuwa na madawati.
Njia nzima katika Wilaya ya Manyoni, Singida, tangu tumepokea Mwenge, shule zote njiani wanafunzi walikuwa wamejipanga barabarani, hawakusoma siku hiyo. Lakini hata Mwenge haukusimama njiani.
Wananchi wa Lusilile na vijiji jirani waliniambia kuwa kulikuwa na msako maalumu kwa wananchi watakaokiuka kuhudhuria mbio za Mwenge, hivyo walilazimika kujipanga barabarani tangu asubuhi na baadaye kupigwa na jua kali, njaa na kiu zao hadi Mwenge ulipopita.
Wapo waliolazimishwa kucheza ngoma ili ionekane wanaufurahia Mwenge. Kifupi, wapo wananchi ambao hawakufanya kazi za kujiingizia kipato ili kuheshimu amri ya kuhudhuria mbio za Mwenge
Kuna mambo mengine ni kwa ajili ya identity ya nchi hufanyika bila kuangalia direct benefit kwenye uchumi, ila kama mwanzilishi wa mada hii alivyosema kwa mambo ya aina hiyo inabidi yaangaliwe sana gharama zake. Gharama za mambo kama haya zinapokuwa kubwa kupiltiliza watu wanaanza kuhoji umuhimu wake.
Hata hivyo, katika mbio za Mwenge, Mwenyekiti wa CCM na katibu wake, pamoja na viongozi wa Umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM) ni watu wa kuheshimiwa kuliko hata askari wa cheo cha juu.
Kuna bajeti ya kuweka mafuta gari ya Mwenyekiti wa CCM, Katibu wa CCM, wa UWT, na UVCCM, japo wanahadaa kuwa Mwenge ni wa kitaifa. Ni uongo, kuthibitisha hili, huwezi kuona popote risiti ya mafuta kwa magari ya wenyeviti wa mikoa wa TLP, NCCR, CUF, CHADEMA, NLD.
Kichefuchefu kingine ni kwamba kuna fungu la kununua nguo za mapokezi ya Mwenge, zipo tofauti kati ya ofisi ya mkuu wa mkoa, ofisi ya katibu tawala wa mkoa, ofisi ya mkuu wa wilaya Ofisi ya TAKUKURU, ofisi ya Usalama wa Taifa na viongozi wengine.
Pia unakuta kuna sare za mapokezi ya Mwenge zingine za kimbizia Mwenge. Fungu la suti hizo zilitosha kununua madawati kwa ajili ya darasa moja la shule waliyoenda kukabidhiana Mwenge ambayo haikuwa na madawati.
Mwenge unatembezwa na kaulimbiu za “kumulika wezi na wala rushwa,” nilishtuka zaidi tulipokuwa Manyoni Mjini, ukarabati wa mnara wa Mwenge, mnara ambao umejengwa miaka mingi huko nyuma, mnara ulipigwa rangi na kuandikwa kaulimbiu ya “Tumethubutu, tumeweza, na Tunasonga mbele” kwa gharama ya Sh. 2.5 milioni. Haiingii akilini. Watanzania tuache kuhalalisha wizi wa kimachomacho kama huu.
Mwenge ni nini? Kwanini unatumika kama alama katika mavazi na kadi za UVCCM? Mwenge una msafara mrefu kuliko hata msafara wa rais?
Katika msafara wa Mwenge, kuna kundi kubwa la askari polisi, sijui wote hao wanalinda nini? Hivi katika Tanzania nani anaweza kuwa na wazo la kuiba Mwenge? Na akiuiba ataufanyia nini?. Polisi wanaolinda Mwenge wapo makini zaidi kuliko hata wale wanaolinda benki.
Tunaambiwa wanaangalia usalama wa Mwenge, je Mwenge huwa unaugua? Mwenge unaweza kuwekewa sumu? Mwenge na TAKUKURU au uhamiaji zina uhusiano gani? Mwenge na mkuu wa Magereza, vina uhusiano gani? Mkuu wa gereza anahusika na wafungwa, je kwenye Mwenge kuna wafungwa? Mwenge na Uhamiaji lini na wapi? Mwenge na Jeshi la Wananchi ambalo jukumu lake ni kulinda mipaka, lini na wapi na kwa nini? Wote hawa wanalipwa pesa kuhalalisha mbio hizi.
Hivi hatuwezi kufungua shule mpaka Mwenge uje? Hatuwezi kupanda miti mpaka Mwenge uje? Hatuwezi kuzindua majengo mpaka Mwenge upite. Miaka zaidi 50 ya Uhuru tumegandamizwa kiakili na Mwenge, kwanini?
Hakika Mwenge sasa unaunguza wazalendo, unanyonya wanyonge, unanyanyasa walipakodi. Unamaliza fedha lukuki bila kuwa na tija. Rais anayebana matumizi ya hovyo amebariki ukimbizwe. Ajabu.
Ni vyema Mwenge nao ukafutwa na kuzikwa kabisa, kwani nalo ni jibu, tena limekomaa, tayari kwa kutumbuliwa
Kuna watu wamejiajiri kupitia mbio za mwenge!?hata ukizuiliwa bado watu mtalalama tu.
oooh kulikua kuna watu wamejiajiri kupitia mbio za mwenge. na mambo mengine kedekede
Waswahili sisi tuna jema.
Wengine wameletwa mjini na mbio za Mwenge.Kuna watu wamejiajiri kupitia mbio za mwenge!?
Habari wadau!
Leo Makamu wa rais Zanziber kazindua mbio za mwenge wa uhuru wakiwa na kauli mbiu ya maendeleo ya Viwanda.
Naomba anaye fahamu umuhimu wa kukimbiza mwenge na matumizi ya zaidi ya bilioni 400.
Nini faida yake?
Kimsingi, Mwenge unatumia gharama kubwa mno, kiasi kwamba fedha hizo zingetumika kufanya shughuli za maendeleo, baadhi ya kero kwa wananchi ama zingekwisha au kupungua kwa kiasi kikubwa.
Inashangaza kuona kuwa Mwenge ule ulikabidhiwa katika eneo la shule ambayo haikuwa na madawati.
Njia nzima katika Wilaya ya Manyoni, Singida, tangu tumepokea Mwenge, shule zote njiani wanafunzi walikuwa wamejipanga barabarani, hawakusoma siku hiyo. Lakini hata Mwenge haukusimama njiani.
Wananchi wa Lusilile na vijiji jirani waliniambia kuwa kulikuwa na msako maalumu kwa wananchi watakaokiuka kuhudhuria mbio za Mwenge, hivyo walilazimika kujipanga barabarani tangu asubuhi na baadaye kupigwa na jua kali, njaa na kiu zao hadi Mwenge ulipopita.
Wapo waliolazimishwa kucheza ngoma ili ionekane wanaufurahia Mwenge. Kifupi, wapo wananchi ambao hawakufanya kazi za kujiingizia kipato ili kuheshimu amri ya kuhudhuria mbio za Mwenge
Hata hivyo, katika mbio za Mwenge, Mwenyekiti wa CCM na katibu wake, pamoja na viongozi wa Umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM) ni watu wa kuheshimiwa kuliko hata askari wa cheo cha juu.
Kuna bajeti ya kuweka mafuta gari ya Mwenyekiti wa CCM, Katibu wa CCM, wa UWT, na UVCCM, japo wanahadaa kuwa Mwenge ni wa kitaifa. Ni uongo, kuthibitisha hili, huwezi kuona popote risiti ya mafuta kwa magari ya wenyeviti wa mikoa wa TLP, NCCR, CUF, CHADEMA, NLD.
Kichefuchefu kingine ni kwamba kuna fungu la kununua nguo za mapokezi ya Mwenge, zipo tofauti kati ya ofisi ya mkuu wa mkoa, ofisi ya katibu tawala wa mkoa, ofisi ya mkuu wa wilaya Ofisi ya TAKUKURU, ofisi ya Usalama wa Taifa na viongozi wengine.
Pia unakuta kuna sare za mapokezi ya Mwenge zingine za kimbizia Mwenge. Fungu la suti hizo zilitosha kununua madawati kwa ajili ya darasa moja la shule waliyoenda kukabidhiana Mwenge ambayo haikuwa na madawati.
Mwenge unatembezwa na kaulimbiu za “kumulika wezi na wala rushwa,” nilishtuka zaidi tulipokuwa Manyoni Mjini, ukarabati wa mnara wa Mwenge, mnara ambao umejengwa miaka mingi huko nyuma, mnara ulipigwa rangi na kuandikwa kaulimbiu ya “Tumethubutu, tumeweza, na Tunasonga mbele” kwa gharama ya Sh. 2.5 milioni. Haiingii akilini. Watanzania tuache kuhalalisha wizi wa kimachomacho kama huu.
Mwenge ni nini? Kwanini unatumika kama alama katika mavazi na kadi za UVCCM? Mwenge una msafara mrefu kuliko hata msafara wa rais?
Katika msafara wa Mwenge, kuna kundi kubwa la askari polisi, sijui wote hao wanalinda nini? Hivi katika Tanzania nani anaweza kuwa na wazo la kuiba Mwenge? Na akiuiba ataufanyia nini?. Polisi wanaolinda Mwenge wapo makini zaidi kuliko hata wale wanaolinda benki.
Tunaambiwa wanaangalia usalama wa Mwenge, je Mwenge huwa unaugua? Mwenge unaweza kuwekewa sumu? Mwenge na TAKUKURU au uhamiaji zina uhusiano gani? Mwenge na mkuu wa Magereza, vina uhusiano gani? Mkuu wa gereza anahusika na wafungwa, je kwenye Mwenge kuna wafungwa? Mwenge na Uhamiaji lini na wapi? Mwenge na Jeshi la Wananchi ambalo jukumu lake ni kulinda mipaka, lini na wapi na kwa nini? Wote hawa wanalipwa pesa kuhalalisha mbio hizi.
Hivi hatuwezi kufungua shule mpaka Mwenge uje? Hatuwezi kupanda miti mpaka Mwenge uje? Hatuwezi kuzindua majengo mpaka Mwenge upite. Miaka zaidi 50 ya Uhuru tumegandamizwa kiakili na Mwenge, kwanini?
Hakika Mwenge sasa unaunguza wazalendo, unanyonya wanyonge, unanyanyasa walipakodi. Unamaliza fedha lukuki bila kuwa na tija. Rais anayebana matumizi ya hovyo amebariki ukimbizwe. Ajabu.
Ni vyema Mwenge nao ukafutwa na kuzikwa kabisa, kwani nalo ni jibu, tena limekomaa, tayari kwa kutumbuliwa
huyo jamaa anaakili ya mwenge.Kudhibisha=kuthibitisha
Hahahahahahaahahahahaah nimecheka mpaka roho imechomoka nipo kwenye ambulance nawahi kituo cha afya call me jei
umeandika ujinga gani hapa kenge we!