Ngambo Ngali
JF-Expert Member
- Apr 17, 2009
- 3,517
- 1,363
Wanakijiji wa wawili wa Kijiji cha Masqaroda Wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara wamekamatwa kwa kuhoji matumizi ya michango ya fedha za mwenge.
Mwenge mwaka huu utawashwa Mkoani Manyara
______________________________________
Democracy is the government of the people, by the people, for the people
Abraham Lincoln
Hivi Jamani Kuna Faida Zozote za Kukimbiza Mwenge wa Uhuru? Kila Mwaka Maelfu ya Pesa yanatumika Kukimbiza Mwenge Nchi Nzima. Eti Wanasema kwamba Mwenge unazindua Miradi hivi Kweli bila kuchoma Mafuta ya kukimbiza Mwenge Miradi Haifunguki?
Hamna mkuu hamna. Ni ushirikina tu huo.
Huwezi kuona mwenge unazimwa wala kuona unawashwa kati kati ya safari. Kwa mfano ikitokea ukiwa unasafirishwa njiani ukazima lazima wakajifiche porini tena watu wawili au watatu ili kuuwasha. Ni ushirikina wa aina yake. I wish tungeu abolish. Nadhani ni ushauri tu alianzisha yule mkuu wa kamati yao ya ufundi anaitwa sheik nani sijui.
Mwalimu Nyerere alianzisha wazo la Mwenge kwa nia njema. Lakini sasa kimekuwa chombo cha kifisadi. Huko vijijini wakisikia mbio za mwenge hawalali. Maana ni msimu wa Watendaji kuwakamua pesa. Huna pesa hata mbuzi, kuku, mazao yako vinachukuliwa. Hizo pesa wanazoita za mafuta ya mwenge sijui huwa yanaingia kwenye hesabu ipi? Kama ni mbio za Serikali kwa nini isigharamie? Miradi inayozinduliwa na mwenge mara nyingi ni miradi iliyo kwenye budget ya Serikali au nu miradi ya ubabaishaji inayokoma mara mwenge ukiishapita. Hakuna anayefanya tathmini ya ufanisi wake baada ya hapo. Ni wizi mtupu.Mwenge ni mzuri saana tatizo usanii mwingi
We are buying fuel in forex you know!Mwenge ni mzuri saana tatizo usanii mwingi