Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
kwa vile umezaliwa miaka hii ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ni vigum kuelewa DRC mpaka leo hawajuani na hawana Lugha moja.
Hebu hamia Rwanda au Somalia ukaone UNAGUZI WA DINI AU UKABILA
MWENGE uache ulivyo kwani hata usiposhiriki huwezi shitakiwa
na hata Upinzani hawajaanza leo liwa na nia ya kutawala alianza Mtukila akaja Sefu na CUF sasa Padri na ndoto bado kutawala km hawatawashirikisha Watanzania wote na vijiji vyote km mwenge unavyopita labda 2025

Kwa sasa tuna lugha moja nchi iko connected mwenge wa nini?
Udini umeshamiri,rushwa ndo usiseme,ubadhilifu wa fedha.ubaguzi katika kupata huduma muhimu wenye nacho ndo wanapata huduma bora.mpaka ajira ni za watoto wa wakimbiza mwenge.Tanzania udugu ni wa majukwaaani tu wanakimbizq mwenge tenda zote serikalini za makampuni yao na watoto wao.bado mnasema nchi tuna umoja????
 
Nawasi wasi na maswali yako!Kajiangalie kwenye kioo,sidhani kama kuna Mtz asiye jua umuhimu wa mwenge,,,,hao opposition kwani wapo

Hata mimi naomba nisaidie kujua faida za Mwenge.. Manake kama ni kuzindua miradi ya maendeleo, hiyo sioni kama ni kazi ya Mwenge as haileti miradi ya maendeleo bali inaenda kusherekea tu miradi ya maendeleo.. Hii haiwezi kweli kuwa gharama inayoweza kuepukika hasa ukizingatia malalamiko juu ya matukio yanayotokea kwenye mbio za mwenge..?

Tusaidiane, tushauriane na tujadiliane....
 
Mwenge ni uchawi wa ccm waendelee kutawala hauna faida yoyote kwa mtanzania wa kawaida.Anayetetea atueleze kwa mara ya kwanza unawashwa walifanya nini na kutamka maneno yapi?
 
mwenge unaeneza ukimwi

Kazi ya kukusanya kondomu zilizotumika inaendelea hapa viwanja vya furahisha. DC Amina Masenza ameishasema hataki kuona kondomu hata moja imetupwa chini ingawa serikali imegawa kondomu bure pale kwenye mkesha. Kumbuka katika kila watu kumi wanaopigana ngunga nane huwa ni kavu aka stereo bila kondomu
 
Whats the point ya kuwa na huu mwenge?

Je una ulazima gani?

Je unamnufaisha vipi mwananchi wa kawaida?

Je gharama zake ni kiasi gani kwa mwaka?

Hizo pesa zinatoka wapi?

Je serkali inachangia hizi pesa?> Kiasi gani?

Je wananchi wanayo haki ya kutoshiriki kwenye hizi sherehe?

Je tukiwa na devolved governance na baadhi ya counties zikakataa haya mambo watashtakiwa?

Je kila mwenge ukienda kwnye mikoa au wilaya serikali hukosa kiasi gani kwa sababu wafanya kazi wameenda kuupokea na kuuzima huu mwenge?


Je OPPOSITION tanzania wana misimamo gani kuhusu huu mwenge?

Je pesa zinazotumika kwa ajili ya mwenge kwa mwaka zinaweza kujenga hospitali ngapi?

Je zipo break down za shughuli nzima za mwenge? nazungumzia ma sub contractors wa uniform, mafuta, sim etc?

Mwenge kazi yake ni kuangaza.illumination.be blessed!
 
Nawasi wasi na maswali yako!Kajiangalie kwenye kioo,sidhani kama kuna Mtz asiye jua umuhimu wa mwenge,,,,hao opposition kwani wapo

Naomba wewe unayejua umuhimu wake utuelezee! na kama unafahamu pia historia yake utuambie sisi kizazi cha sasa tuliojaa maswali mengi kuhusu huo mwenge!
 
Kwa sasa tuna lugha moja nchi iko connected mwenge wa nini?
Udini umeshamiri,rushwa ndo usiseme,ubadhilifu wa fedha.ubaguzi katika kupata huduma muhimu wenye nacho ndo wanapata huduma bora.mpaka ajira ni za watoto wa wakimbiza mwenge.Tanzania udugu ni wa majukwaaani tu wanakimbizq mwenge tenda zote serikalini za makampuni yao na watoto wao.bado mnasema nchi tuna umoja????
km unaona mwenge hauunganishi watanzania ila kwa Lugha tu basi jaribu kutupia jicho hapo DRC, ANGOLA KENYA
MSUMBIJI ZIMBABWE na nchi nyinginezo ni watoto wote wanapata opportunity unazozitaka?
Majimbo na Mikoa hawaelewani unaweza ingia DRC ukanunua Mlima / Mgodi na Serikali isijue kwani unaweza lindwa na majeshi ya Nchu za Nje 9Wakati TZ huwezi hata kupata kipande cha ardhi sq meter moua)
Raia wa Nchi hizo wanaibiwa madini na vito na Majasusi ya Nchi za Nje (TZ hiyo hakuna km ni wizi ni Watanzania wanajumuishwa kwenye wizi huo)
Huwezi ingiza mambo ya kidini bila watanzania kukumaizi kuwa lengo lako si ukimbizi bali ni Al-Shabab
Ndugu yangu km huwezi kuungalia mwenge au kuusikia zima macho na masikio

Sisi tunaka kuuwasha Mwenge Kuuwasha Mwenge
Na kuuweka juu ya Mlima, Mlima kilimanjaro
Kuwasha mwenge kuwasha mwenge .............
 
jamani mi naomba japo maelezo mafupi ya faida anayoipata mwananchi wa kawaida kwa hizi mbio za mwenge za kila mwaka.
 
ZAIDI ya kusambaza UKIMWI NA KUONGEZA IDADI YA WATOTO WA MITAANI SIJAONA KINGINE .
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikitafakari bila kupata jibu,hivi mwenge una faida gani kwa taifa,nakumbuka wimbo huu tangu nikiwa mtoto,"mwenge choma,chomaaa...walanguzi choma,mafisadi chomaaaa...wahalifu wamejaa nchi nzima mwenge umeshindwa kuwachoma,mafisadi yamejaa serikalini lakini mwenge hauyachomi,mwenge unalindwa kuliko wanyamapori,dhahabu,Tanzanite,almasi na raslimali zingine,wanyama wetu wanauawa kila siku hawana ulinzi wowote wa maana,ilikuja ndege ikawabeba tena ya jeshi la uarabuni,lakini ajabu mwenge unapewa ulinzi mkubwa na msafara wa magari mengi ajabu,gharama ya kutembeza mwenge kwa siku ni zaidi ya mil 45,huu mwenge una faida gani kwa taifa hili? hebu naomba na wenzangu mchangie au ni ushirikina wa ccm kuendelea kutawala?
 
Back
Top Bottom