Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Kipindi cha mwalim toka mwenge uanzishwe, hawakuwepo mafisadi wengi sana kama ilivyo kwasasa hivi, hivyo inaonyesha kadri siku zinavyo kwenda mafisadi wanazi kuongezeka na mwenge unashindwa kuwachoma hawa mafisadi. Hivyo mimi naona mwenge una faida ya kuzaa mafisadi wazidi kuongezeka zaidi. na kula hela za mlipa kodi. Gharama hiyo inayo tumika kutembeza mwenge 45mil kwa siku zinatosha hata kwa kuweka umeme wa sola kwenye zanati ambako akina mama wanajifungua kwa vibatali!! ni wazi mwenge unazaa mafisadi na kadri siku zinavyo kwenda mwenge utakuwa na wajukuu!!!!
 
Mwenge ulikuwa na faida wakati wa jk nyerere kwani wakati huo viongozi walikuwa na maadili sio sasa ambapo kila kiongozi ajifanyia analojisikia.
 
Mwenge ni mtaji wa CCM na mafisadi wake tu hakuna kingine!
 
kati ya vitu sivipendi kabisa maisha mwangu ni huu mnaita mwenge hivi unamulika nini, wapi na nani??
 
kati ya vitu sivipendi kabisa maisha mwangu ni huu mnaita mwenge hivi unamulika nini, wapi na nani?? na faida ya nani??
 
Msilolijua ni kama kiza....there's something behind it...ni siri kubwa kwa taifa ndo maana wanaung'ang'ania..wenzetu wanadini wanaita maagano
 
hilo ni chaka la watu kujipigia fedha si unajua bajeti yake ilivyo kuwa nono
 
nakujibu jawabu ya uhakika kabisa.
katika taifa hakuna faida ila ni hasara. kwa wale watembezaji hupata fedha na kutekeleza shughuli zao za kimaisha.
 
Je kuna msaada wowote ambao unaletwa na mwenge wa uhuru ?
Au ni mojawapo ya matumizi mabaya ya pesa za serikali?
Upo umuhimu wowote wa kuendelea kuwepo kwa huu mwenge wa uhuru?
Wana jukwaa naomba kujuzwa??
 
Nawasi wasi na maswali yako!Kajiangalie kwenye kioo,sidhani kama kuna Mtz asiye jua umuhimu wa mwenge,,,,hao opposition kwani wapo

umeambiwa mm mkuwait?
huo Mwenge uzimwe na uwashwe kwa kauli mbiu na baada ya mda flani sio kunenepesha watu na kuzindua miradi ambayo hata kiongozi wa wilaya wa naweza Fanya
umbulula huu.
 
It is time to stand still and SAY NO TO MWENGE. Hii kimbiza kimbiza bila maelengo yake kutimizwa ni dharau kwa waanzilishi wa hii kitu.
 
Mpaka hapo nimepata jibu Kamili ni kwamba mwenge unachangia kwa asilimia nyingi zaid kuharibu nchi yetu na kutumia pesa nyingi za serkali ambazo zinge saidia kufanyia shuhuli zingine za maendeleo
 
Back
Top Bottom