Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Unajua hata najiulizaga huu mwenge unafaida zipi?? Kwa nini hizo pesa za maandalizi wasingejenga maktaba na maabara kwenye shule hata moja tu ya kata!??? Ni maajabu haya...
 
kukua kwa ajira ya walinzi. kukua kwa biashara ya sigara na karanga.

pia ni sehemu ya kuongeza marafiki
 
Kushabihikia mbio za mwenge Tanzania ni sawa kuugua homa ya Dengue, wako waliowahi kusema wakiukwaa uraisi ndani ya nchi hii watapiga marufuku mbio za mwenge kwakua umepitwa na wakati na kuuweka huo mwenge kwenye jengo la makumbusho.
 
Interahamwe na mwenge damdam mwana lazima watumishi michango ilhali mwenge una bajeti yake wanaiba escrow hadi mfukoni mwa watumishi wa serikali na wananchi
 
Umuhimu wake kwa sasa ni watu wengi wanaambukizwa ukimwi na mimba nyingi zisizotarajiwa zinatungwa!Watoto kama lile lijamaa linene wanazaliwa!
 
Mmanyema mmoja alisema badala ya kukimbiza kale ka koroboi kanakotoa moshi na kusababisha pollution ni bora kumkimbiza Jei kei nchi nzima ili ajionee uhalisia wa maisha ya wenye nchi waliompigia kura kwa kishindo ili anavyotoa takwimu zake za mafanikio yake toke aingie madarkani hadi alipo aweze kuzungumza kwa takwimu badala ya kusubiri hizi za maisha bora anazoletewa na wakimbiza koroboi!
 
Leo nilianzisha thread yenye kichwa: Magazeti yasusia mbio za Mwenge.Habari za mwenge zimepotezewa kabisa na waandishi wa habari.
 
Umuhimu upo sana! Sasa hivi mwenge unatakatisha miradi ya watiu binafsi kama guest houses zilizojengwa kwa pesa za kifisadi.
 
Back
Top Bottom