NYABISHABO
Member
- Oct 27, 2011
- 50
- 57
Huu mwenge wawashie viongozi maana ndo wanakosa uzalendo kwa ufisadi wanaoufanya, kwa wananchi unaenda kufanya nini?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huu ni ufisadi wa hali ya juu, mwenge unafungua miradi hewa, wanasema unamulika maovu na kuleta matumaini, ile hali ufisadi unazidi kuongezeka tena saizi wanafanya mchana kweupe, sioni faida ya mwenge, tuache kuishi kwa mazoea, hospitali hazina madawa, miundo mbinu mibovu vijini ndio usiseme, maambukizi ya ukimwi yanazidi kuongezeka kutokana na mikesha ya mwenge, wanajua kinachofanyika ndio maana wanagawa kondom bure kwenye mkesha wa mwenge, sihitaji kusikia habari ya mwene, mabilioni ya fedha hizo huwa zinatumika vipi, tupinge mbio za mwenge kuzuia ufisadi huu mkubwa kwa kisingizio cha mwenge.
na wapinzani wanaona sawa tuu
Ngono, wizi wa fedha za walala hoi, maambukizi ya ukimwi na U-CCM
Umajununi ni kuamini kuwa kila akifanyacho mzungu basi ni kizuri na lazima mswahili akifanye pia.Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu
Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu
all over the world kila nchi inatunu zake
Mambo mengine kuyakumbatia ni upuuzi na ni upumbavu zaidi iwapo sababu ya kuyakumbatia ni kuwa eti kuna mtu,taifa au mwenzako mwingine nae anayakumbatia.Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu
Hata hao Wa-ingereza hawaufagilii huo ufalme na siku zake zinahesabika.Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu
Pitia kidogo hapa kama unao muda;Britain's royal family: cut this anti-democratic dynasty out of politics | Seumas Milne | Comment is free | The Guardian
Nanukuu.. Mbio za mwenge wa uhuru hutumika kuhimiza miradi mbalimbali kwa njia ya kuweka mawe ya msingi au kuzindua miradi iliyowekewa jiwe la msingi mwaka uliopita na pia kuhamasisha moyo wa Wazalendo na kujitolea kwa vijana hasa kuonyesha umuhimu na nafasi yao katika kudumisha nchi yao, kulinda uhuru na kuleta maendeleo ya nchi yao Mwisho wa kunukuuuhii nchi ya ajabu sana gharama zote za kazi gani sasa, unatumia mabilioni kuzindua miradi ya mamilioni halafu tunalalamika nchi haina fedha! hii ni sawa na kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku.
Khaa!! Kwani ni nani anayechangia M4C na matamasha mengine?? Tumia akili acha watu wale. kama huwawezi ungana nao.. ni rahisi hivyo tu :baby:Mradi mwingine wa kifisadi kabisa Je!Ni nani anayehakiki mabilioni hayo ya wananchi? Mabilioni hayo huliwa na UV-CCM na ccm maana shughuli za mwenge ziko chini ya vijana wa CCM.
Siye tusiokuwa vijana wa ccm kwa nini tuuchangie kupitia mapato yetu na kodi zetu?