Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Huu mwenge wawashie viongozi maana ndo wanakosa uzalendo kwa ufisadi wanaoufanya, kwa wananchi unaenda kufanya nini?
 
Huu ni ufisadi wa hali ya juu, mwenge unafungua miradi hewa, wanasema unamulika maovu na kuleta matumaini, ile hali ufisadi unazidi kuongezeka tena saizi wanafanya mchana kweupe, sioni faida ya mwenge, tuache kuishi kwa mazoea, hospitali hazina madawa, miundo mbinu mibovu vijini ndio usiseme, maambukizi ya ukimwi yanazidi kuongezeka kutokana na mikesha ya mwenge, wanajua kinachofanyika ndio maana wanagawa kondom bure kwenye mkesha wa mwenge, sihitaji kusikia habari ya mwene, mabilioni ya fedha hizo huwa zinatumika vipi, tupinge mbio za mwenge kuzuia ufisadi huu mkubwa kwa kisingizio cha mwenge.

Umenena muungwana!
 
Tanzania tunajiua wenyewe kwa ujinga na uwoga wa kuchukua hatua dhidi ya serikali
 
Nataka kutahadharisha. huu mwenge huenda ni ushirikina yaani kuna masharti ya kiganga ndiyo maana hata watu wapige kelele, pia pamoja na hasara jamaa hawataki kuacha. kwa hiyo usishangae hata wapinzani wakichukua nchi watashindwa kuuondoa maana 'kama' nao wanaamini waganga watawaambia mkiuondoa yatatokea madhara haya na haya. kwa hiyo tuombe Mungu sana atupatie viongozi wasio na imani za kishirikina.
 
Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu

Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu

all over the world kila nchi inatunu zake
Umajununi ni kuamini kuwa kila akifanyacho mzungu basi ni kizuri na lazima mswahili akifanye pia.
 
Mradi mwingine wa kifisadi kabisa Je!Ni nani anayehakiki mabilioni hayo ya wananchi? Mabilioni hayo huliwa na UV-CCM na ccm maana shughuli za mwenge ziko chini ya vijana wa CCM.

Siye tusiokuwa vijana wa ccm kwa nini tuuchangie kupitia mapato yetu na kodi zetu?
 
Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu

Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu
Hata hao Wa-ingereza hawaufagilii huo ufalme na siku zake zinahesabika.
Pitia kidogo hapa kama unao muda;Britain's royal family: cut this anti-democratic dynasty out of politics | Seumas Milne | Comment is free | The Guardian
Mambo mengine kuyakumbatia ni upuuzi na ni upumbavu zaidi iwapo sababu ya kuyakumbatia ni kuwa eti kuna mtu,taifa au mwenzako mwingine nae anayakumbatia.
Kujitambua ni kufanya yako kwa wakati wako,kwa faida yako na bila shurti.
 
Umefika wakati sasa wananchi lazima tuanze kuwahoji wabunge wetu mambo kama hayo. Pesa hizo zingeweza kufanya mengine muhimu kama katika elimu au afya. Tusiwaachie wabunge waje kutudanganya tena tuwapigie bila kuonyesha wanafanya jitihada gani kuziba mianya hatari kama hii.
 
Ukimwi watu wanapata kwa uhuni na umalaya wao hata ww isitoshe huwa unafanya ngono hata mwenge usipokuwepo! Acheni kusingizia mwenge.na hata hivyo mwenge ni alama muhimu sana haifai kufutwa faida nyingi kuliko hasara!
 
Naomba nikumbushwe MBIO ZA MWENGE NI KILA MWAKA AU IKOJE? IKIWA NI KILA MWAKA FIKIRIA ni miaka mingapi imepotea wakati izo hela ingekua zinapelekwa kuendesha shughuli za vijiji ikiwemo elimu na makaazi bora kwa wakulima ISINGESAIDIA. pia Hela hizo Zingefanyiwa jambo la Muhimu zaidi kwa maslahi ya nchi ambayo ni endelevu. HAYA MAMBO YA KUA NA SHEREHE KUBWA WAKATI WATU WANAISHI KWA SHIDA NDIO YANAYOTUHARIMU TANZANIA NI KWASABABU TUNAPENDA KUIGA IGA KUFATAFATA.

Kweli wanafurahi siku Moja wanajuta Mwaka Mzima...
 
hii nchi ya ajabu sana gharama zote za kazi gani sasa, unatumia mabilioni kuzindua miradi ya mamilioni halafu tunalalamika nchi haina fedha! hii ni sawa na kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku.
Nanukuu.. ‘Mbio za mwenge wa uhuru hutumika kuhimiza miradi mbalimbali kwa njia ya kuweka mawe ya msingi au kuzindua miradi iliyowekewa jiwe la msingi mwaka uliopita na pia kuhamasisha moyo wa Wazalendo na kujitolea kwa vijana hasa kuonyesha umuhimu na nafasi yao katika kudumisha nchi yao, kulinda uhuru na kuleta maendeleo ya nchi yao’ Mwisho wa kunukuuu
 
Mradi mwingine wa kifisadi kabisa Je!Ni nani anayehakiki mabilioni hayo ya wananchi? Mabilioni hayo huliwa na UV-CCM na ccm maana shughuli za mwenge ziko chini ya vijana wa CCM.

Siye tusiokuwa vijana wa ccm kwa nini tuuchangie kupitia mapato yetu na kodi zetu?
Khaa!! Kwani ni nani anayechangia M4C na matamasha mengine?? Tumia akili acha watu wale. kama huwawezi ungana nao.. ni rahisi hivyo tu :baby:
 
Yaani ushauri wangu wangeuweka uwo mwenge kwenye makumbusho mwenye shida akauangakie huko unamakiza ela2 ndo maana kila kukicha zinazinduliwa kodi mpaya
 
Wakale wapi. Kama mwenge ni njia ya kuongeza ufisadi kama tunu ya taifa na iwe hivyo. Hao ndio ccm.
 
Nikiwa mwananchi mzawa na mwenye uchungu na wajinsi fedha zetu zinavyoteketea kwa kinachoitwa mbio za mwenge,Leo nimeshuhudia aibu pale njombe mwege umepokelewa na watoto wa shule na viongozi wa chama na serikali tu.mh jk nakuomba ufutilie mbali mbio hizi za mwenge.
 
Back
Top Bottom