Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Nikiwa mwananchi mzawa na mwenye uchungu na wajinsi fedha zetu zinavyoteketea kwa kinachoitwa mbio za mwenge,Leo nimeshuhudia aibu pale njombe mwege umepokelewa na watoto wa shule na viongozi wa chama na serikali tu.mh jk nakuomba ufutilie mbali mbio hizi za mwenge.

Kichwa cha habari na wewe mwenyewe ulitaka kuandika nini?
 
Umuhimu wake kwa sasa ni watu wengi wanaambukizwa ukimwi na mimba nyingi zisizotarajiwa zinatungwa!Watoto kama lile lijamaa linene wanazaliwa!

Mwenge leo ndio umedhihirisha kuwa hauna tena mvuto kwa wananchi pale Njombe.Najiuliza hivi hawa wanaokwenda kuupokea na kukuta hali ya kususiwa na wananchi hawaoni aibu?
 
Ingekuwa heshima kubwa hisiyosahaulika kwa mh,jk angeufutilia mbali kabla ya kustaafu.
 
Mmawia wewe Raia wa nchi gani. Mwenge ni muhimu. Ukimaliza kupinga Mwenge utapinga mengine si hajabu hata bendera na wimbo wa Taifa na Mengine mengi
 
Hata watu wasipo changia mwenge wa uhuru unapita!
Jimbo kwa kamanda mkuu wa Singida mashariki hatuchangii mwenge wa uhuru lakini bado unapita na kukesha kabisa!
Juzi kati,mwenge umekuja Makiungu wakati hamna hata ka mradi ka serikali kakufunguliwa,umekesha na kusha na si tukapata night club ya dezo!
Asanteni sana serikali kutuelewa wana Singida mashariki!
 
Wakuu samahani kwa hili jaman naomba kuuliza hvi Mwenge unafaida gani au unasaidia nn katika nchi yetu wakuu maana ukitua sehem na kukesha basi ujue hapo kila vitu vibaya hufanyika. Mfano ulevi, umalaya, wizi na matukio mengine kibao so naomba kuelimishwa zaidi kuhusu hili.



MIMI NI MTANZANIA HALISI NINAE PENDA NCHI YANGU.
 
wakuu samahan kwa hili jaman naomba kuuliza hvi mwenge unafaida gan au unasaidia nn ktk nchi yetu wakuu maana ukitua sehem na kukesha basi ujue hapo kila vtu vbaya hufanyika mf.ulevi,umalaya,wizi na matukio mengine kibao so naomba kuelimishwa zaidi kuhusu hili



MIMI NI MTANZANIA HALISI NINAE PENDA NCHI YANGU.

Hayo uliyoyataja nakuongezea na mengine ofisi za serikali na manispaa hufungwa nawafanyakazi hulazimishwa kwenda uwanjani
Udhibitisho ninao nilikuwa Lindi na Mtwara shughuli zilifungwa kwa siku mbili huu ni uhuni
 
Mwenge wa uhuru umeleta maendeleo sana.
umetuangazia mafisadi sasa tunawajua. wezi wa pesa za serikali tumewajua. majangili arobaini tumewajua. wauza madawa tumewajua. kila mhalifu amemulikwa na kujulikana. mwenge unaunganisha vijana mpaka mimba za nje nje wanapata kwenye mbio za mwenge.
Mwenge JUU JUU JUU ZAIDI
 
Hakuna jibu hapa nipeni watu wanaamua kukashfu bora kupita bila kuacha comment yeyote.
 
sio office tu zilifungwa mkuu na madarasan hatukuingia tulikimbiza mwenge na nyimbo kibao tukauimbia
 
Back
Top Bottom