Mwigulu Nchemba: Tumefuta baadhi ya tozo, nyingine tumepunguza kwa asilimia 10-50
Eti serikali sikivu, kipindi wanaweka hizo tozo uliita jina gani? Serikali Kuweka tozo au hata kodi Kisha kutambua zinaumiza wananchi na kuziondoa huonesha ni namna gani tulivyo na MANANGA katika wizara husika Wala sio usikivu.

Kama wanania njema na pesa za watz wapunguze matumizi kwa vitendo, in this poor country ambayo wewe mleta mada upo serikali unayoiita sikivu inatumia zaidi ya 400 billions Kila mwaka kununua V8 ambazo ni kodi za wananchi.

Acha kushabikia Kila kitu tafakari kwanza, sio sikivu sikivu......
 
Leo tar 20 mpk tar 1oct ni siku 10.
Hizo siku 10 tozo zitakazokusanywa itapigwa abla-kadabla shot-kulia zote ndani mumfuko.
Ndio ianze sheria mpya.
Na hizi ndiyo tabia za watu wenye roho mbaya na mafisadi! Ingekuwa tozo zimeongezwa zingeanza mara moja lakini kwa kuwa Mwigulu anataka kukomoa watu basi amepanga mabadiliko yaanza baada ya siku 10 na ndiyo furaha yake!
 
Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki yaani ATM kwenye miamala yenye thamani ya chini ya tsh 30,000/=
Hiki ni kiini macho maana wanajua watarecover hiyo deficit kwenye miamala inayozidi hiyo 30,000/- . Huu ni ujambazi
 
Alieanzisha Tozo ni Nani!?anaezifuta ni Nani!? Mi Binafsi nina UWEZO wa kuongoza Hii NCHI bila Tozo!!

Tumeshawazoea tabia yao ni hii hapa;-

"Tengeneza Tatizo tatua tatizo halafu jipigie makofi"!

Nakazia

Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA
 
Ushangiliaji wa Wabunge wa CCM leo kwa Dr Mwigullu Nchemba hakukuwa ule uliozoeleka, wameshangilia Kinyonge sana kana kwamba wanalazimishwa

Sijaelewa sababu au ndo makundi yashaanza!!

Karibu Tanzania TAL soma Exodus 14:14
 
Huyo Waziri kwa kuwa alishatutukana watanzania, kuwa asiyetaka tuzo hizo aende Burundi...............

Je ana haja gani ya kutueleza watanzania kuwa wizara yake imepunguza hizo tozo?[emoji3064]

Huyo Waziri hastahili hata kwa dk, moja zaidi, aendelee na wadhifa wake wa uwaziri wa Fedha, kutokana na kiburi alichokionyesha kwa wapiga kura wake na badala yake tunaziomba mamlaka za uteuzi ziweze kumfukuza Kazi. Full Stop
Mwalimu ndie akikuwa ana jali dhamana aliyo kuwa nayo kwa watu wake
 
Wao si ndio inasemekana wamepitisha, sasa waziri amefuta bila maridhio ya waliopitisha. Lazima wawe wanyonge tu
 


Akizungumza leo bungeni, Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amesema uongezwaji wa wigo wa kukusanya mapato kupitia tozo uliibua malalamiko kwenye jamii, hivyo Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi iliagiza upitiwaji upya wa tozo hizi na kuzingatia maoni ya wananchi.

Marekebisho yafuatayo yamefikiwa-
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu kwa pande zote.​
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja na kutoka benki moja kwenda benki nyingine.​
  • Kutowahusisha wafanya biashara wadogo (merchants) kama ilivyokuwa kweye kanuni ya sasa.​
  • Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki yaani ATM kwenye miamala yenye thamani ya chini ya tsh 30,000/=​
  • Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10-50 kutokana na makundi ya miamala​

Marekebisho haya yataanza kufanya kazi Octoba 1, 2022. Aidha Serikali itafuta utaratibu wa kodi ya zuio ya pango inayotaka kukusanywa na mpangaji, hivyo kwa sasa itapaswa kulipwa na mmiliki wa nyumba na siyo mpangaji.

Kwa kuwa pesa hizi zitaipunguzia mapato serikali, Waziri ameelekeza Serikali ianze kubana matumizi yake mfano kwenye vikao, mafunzo ya semina, warsha, safai za ndani na nje, misafara, kukagua miradi n.k

Wataalamu wa wizara ya fedha na mipango ndiyo wamefanya mapitio haya wakiwa ofisini kwa kuwa ni sehemu ya majukumu yao. Taarifa za kuwa kuna tume iliundwa kutoka nje ya wizara ni uzushi.

HAKUNA BUNGE KUNA KUSANYIKO LA WATU SIJUI WANAFANYA NINI HUMO, WANAKIJUA WAO WANACHOKIFANYA .
 


Akizungumza leo bungeni, Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amesema uongezwaji wa wigo wa kukusanya mapato kupitia tozo uliibua malalamiko kwenye jamii, hivyo Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi iliagiza upitiwaji upya wa tozo hizi na kuzingatia maoni ya wananchi.

Marekebisho yafuatayo yamefikiwa-
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu kwa pande zote.​
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja na kutoka benki moja kwenda benki nyingine.​
  • Kutowahusisha wafanya biashara wadogo (merchants) kama ilivyokuwa kweye kanuni ya sasa.​
  • Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki yaani ATM kwenye miamala yenye thamani ya chini ya tsh 30,000/=​
  • Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10-50 kutokana na makundi ya miamala​

Marekebisho haya yataanza kufanya kazi Octoba 1, 2022. Aidha Serikali itafuta utaratibu wa kodi ya zuio ya pango inayotaka kukusanywa na mpangaji, hivyo kwa sasa itapaswa kulipwa na mmiliki wa nyumba na siyo mpangaji.

Kwa kuwa pesa hizi zitaipunguzia mapato serikali, Waziri ameelekeza Serikali ianze kubana matumizi yake mfano kwenye vikao, mafunzo ya semina, warsha, safai za ndani na nje, misafara, kukagua miradi n.k

Wataalamu wa wizara ya fedha na mipango ndiyo wamefanya mapitio haya wakiwa ofisini kwa kuwa ni sehemu ya majukumu yao. Taarifa za kuwa kuna tume iliundwa kutoka nje ya wizara ni uzushi.
Miamala iliyosamehewa inawafeva watu Wa kundi lipi? Je hyo miamala ndo yalikuwa malalamiko makuu au ya awamu ya pili?

Au atusaidie dr, kwan hitaji la msingi haawa ni kufutwa tozo au kuondolewa? Hebu tujiulize kdg tu toza za miamala ya sim zipo toka Mwaka, ila za mabenk miezi 2 tu wamefanyia kazi au kwa kuwa wanotumia bank ni wao?

Kunatitzo kwenye think tank.
 
SHERIA INASEMAJE KUHUSU KUKATA KODI TOKA CHANZO KIMOJA CHA MAPATO YAANI MSHAHARA

Kuhusu wafanyakazi wenye chanzo kimoja cha mapato yaani mshahara, mnakubali kulazimishwa kuhangaika kutoa miamala chini ya Tsh. 30,000 ili msifyekwe tozo


TUCTA wanasemaje kuhusu kuwatetea wafanyakazi wasipate usumbufu au kukatwa tozo pale wanapolazimika kutuma miamala au kutoa pesa zaidi ya Tshs. 30,000

 
Wana maombi ya jf tupange siku za kufunga kumlaani,

Vinginevyo afute tozo zote
 
Ni usanii mtupu,

-Wananchi wengi wa chini hawana akaunti Bank, wengi ni watumiaji wa miamala ya simu za mikononi- kwa hiyo ili mwananchi wa daraja la chini aguswe directly ni lazima tozo ya miamala ya simu iliyoletwa na awamu hii iondolewe.

- Daraja la kati wengi ni wafanyakazi, wafanyabiashara wenye maslahi madogo ambao wanatumia ATM cards, kama serikali ina nia ya kuwasaidia iondoe tozo ambazo yenyewe imeziweka awamu hii.
Hata makato ya simu yamepunguzwa kutoka elf 7 mpaka elf 4
 


Akizungumza leo bungeni, Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amesema uongezwaji wa wigo wa kukusanya mapato kupitia tozo uliibua malalamiko kwenye jamii, hivyo Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi iliagiza upitiwaji upya wa tozo hizi na kuzingatia maoni ya wananchi.

Marekebisho yafuatayo yamefikiwa-
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu kwa pande zote.​
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja na kutoka benki moja kwenda benki nyingine.​
  • Kutowahusisha wafanya biashara wadogo (merchants) kama ilivyokuwa kweye kanuni ya sasa.​
  • Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki yaani ATM kwenye miamala yenye thamani ya chini ya tsh 30,000/=​
  • Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10-50 kutokana na makundi ya miamala​

Marekebisho haya yataanza kufanya kazi Octoba 1, 2022. Aidha Serikali itafuta utaratibu wa kodi ya zuio ya pango inayotaka kukusanywa na mpangaji, hivyo kwa sasa itapaswa kulipwa na mmiliki wa nyumba na siyo mpangaji.

Kwa kuwa pesa hizi zitaipunguzia mapato serikali, Waziri ameelekeza Serikali ianze kubana matumizi yake mfano kwenye vikao, mafunzo ya semina, warsha, safai za ndani na nje, misafara, kukagua miradi n.k

Wataalamu wa wizara ya fedha na mipango ndiyo wamefanya mapitio haya wakiwa ofisini kwa kuwa ni sehemu ya majukumu yao. Taarifa za kuwa kuna tume iliundwa kutoka nje ya wizara ni uzushi.


==========

KAULI YA SERIKALI KUHUSU TOZO IKITOLEWA NA MHESHIMIWA DKT. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU (MB),
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa, katika mwaka wa fedha 2021/22, Sheria ya Malipo ya Taifa, Sura na. 437 (National Payment System Act, Cap.

ilifanyiwa marekebisho kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2021 na kuanzisha tozo ya miamala ya kutuma na kutoa fedha kwa njia ya simu za mikononi yaani, Mobile Money Transaction Levy. Sambamba na tozo hii, tulipandisha tozo kwenye mafuta kwa ajili ya kutunisha mfuko wa TARURA na Mfuko wa Elimu ya juu. Lengo la kuanzisha tozo hizi ni kuunganisha nguvu na umoja wa Watanzania wote katika kuiwezesha Serikali kuongeza kasi ya kutekeleza miradi hasa ile iliyokosa fedha kutokana na ufinyu wa bajeti ili kuwakwamua wananchi dhidi ya ukosefu wa huduma za jamii-msingi kwa kuzingatia kuwa sura ya bejeti yetu karibu kila mahitaji ni mahitaji ya lazima.Mahitaji ya lazima yanayolindwa kwa mfano SGR, TANROADS, Bwawa la Umeme, REA, TARURA, Maji, Elimu, Mikopo ya Elimu ya Juu, Elimu bila Ada, Mishahara, Deni la Taifa, Afya ni takribani 27.9 trilion na makusanyo ya ndani ni takribani 28.01trilioni.

Mheshimiwa Spika, Serikali haina malengo ya kutoza Wananchi wake kodi/tozo kwa ajili ya kuwapa mzigo tu, bali inalenga kuwahusisha Watanzania wote kwa umoja wetu katika juhudi za kujikwamua kimaendeleo. Kwa mfano, tulipofanya uamuzi huu:

Tulikuwa na hali mbaya sana ya barabara za vijijini zilizokosa matengenezo kwa ufinyu wa bajeti, kadhalika, tulikuwa na vijiji ambavyo havijawahi kuwa na barabara ya aina yeyote tangu nchi hii ipate uhuru, akina mama wajawazito walikuwa wakibebwa kwa vitanda kupelekwa hospitali na wengine kupoteza maisha njiani, watoto wa shule wakibebwa na maji kwa vijito tu kukosekana kwa madaraja;

Tulikuwa na kilio kikubwa sana cha ukosefu wa vituo vya afya vya kisasa vijijini, wagonjwa wote walikuwa wanalazimika kutegemea hospitali za wilaya tu, maeneno mengine hata hospitali za wilaya hazikuwepo, sehemu nyingine wananchi walilazimika kwenda hospitali za mikoa jirani. Tulikuwa tunapoteza maisha ya watanzania kutokana na umbali wa kufuata huduma za afya;

Tulikuwa na kilio kikubwa cha uwepo wa maboma ya madarasa na nyumba za walimu yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi na yaliyokaa muda mrefu bila kukamilishwa ilhali kukiwa na uhitaji mkubwa wa madarasa kutokana na ongezeko kubwa la watoto;

Tulikuwa na kilio kikubwa cha wanafunzi waliokosa mikopo ya elimu ya juu wapatao 26,000 wakijumuisha mwaka juzi na mwaka jana. Hawa ni watoto wa kitanzania hasa hasa wanaotoka katika familia masikini ambao ndoto zao za kufika chuo kikuu zilikuwa zinaishia hapo; na

Tulikuwa na kilio kikubwa cha maji hasa hasa vijijini, jambo hili lilikuwa linaathiri sana shughuli za maendeleo kwa mfano kila mtoto abebe galoni ya maji na kuibajeti kwa siku nzima, walimu kufuata maji maeneo ya mbali, vijana wanaotaka kujenga kuingia gharama kubwa kwa kununua maji yanayopimwa kwa ndoo pamoja na kukosekana kwa mahitaji ya maji katika maeneo muhimu kama Hosipitalini.

Mheshimiwa Spika, makusanyo ya tozo ya miamala yameiwezesha Serikali kutoa huduma za msingi za Wananchi wetu katika mwaka wa fedha 2021/22. Mathalani, Serikali ilitumia jumla shilingi bilioni 7 zilitokana na tozo ya miamala kwa ajili kujenga madarasa. Vilevile, Serikali ilitumia jumla ya shilingi bilioni 143.7 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya ambapo kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 117 sawa na asilimia 81.4 ya fedha zote zilitokana na tozo ya miamala. Kadhalika, Serikali ilitumia jumla ya shilingi bilioni 611.3 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu na kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 221.3 zilitokana na tozo. Kwa upande wa TARURA, Serikali ilitumia jumla ya shilingi bilioni 735.7 kwa ajili ya ujenzi wa barabara vijijini ambapo kati ya kiasi hicho shilingi bilioni 13.5 zilitokana na tozo kwenye miamala na kiasi kingine ni tozo kwenye mafuta.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/23, kulikuwa na mahitaji muhimu na ya lazima ambayo yangekosa fedha kutokana na ufinyu wa bajeti. Baadhi ya masuala muhimu ambayo yangeathiriwa kama tungefuta kabisa chanzo hiki ni:

Tungeelekeza fedha za mkopo wa ECF kwenye madarasa mwaka huu, tusingeweza kupeleka bilioni 954 kwenye kilimo zinazolenga kujenga miundombinu ya umwagiliaji, mbegu bora pamoja na block farming. Serikali ilitumia busara ya kiuchumi kupeleka fedha hizo kwenye sekta za uzalishaji ili kutengeneza ajira kwa vijana, na fedha za kutoa huduma za jamii zitafutwe kutoka kwenye tozo;

Tungeelekeza fedha za mkopo wa ECF kwenye ujenzi wa VETA mwaka huu, tusingeweza kupeleka bilioni 145 kwenye mifugo, uvuvi na wamachinga zinazolenga kujenga na kununua boti za uvuvi, kuchochea ukuaji wa sekta ya mifugo na kujenga miundombinu na mitaji kwa wamachinga. Katika suala hili pia, Serikali ilitumia busara ya kiuchumi kupeleka fedha hizo kwenye sekta za uzalishaji na fedha za kutoa huduma za jamii zitafutwe kutoka kwenye tozo;

Tungeelekeza fedha za mkopo wa AfDB kwenye ujenzi wa madarasa na VETA mwaka huu, tusingeweza kupeleka bilioni 150 kwenye ruzuku ya mbolea ili kuwasaidia wakulima wazalishe chakula cha kutosha kwa ajili ya nchi yetu na kudhibiti mfumuko wa bei. Hapa pia, Serikali ilitumia busara ya kiuchumi kupeleka fedha hizo kwenye sekta za uzalishaji na fedha za kutoa huduma za jamii zitafutwe kutoka kwenye tozo; na

Tungeamua kutotoa ruzuku ya shilingi bilioni 100 kwenye mafuta kila mwezi tungeweza kuelekeza fedha hizo kujenga madarasa yote, VETA na mengineyo. Hata hivyo, tungeweza kuwa na mfumuko wa bei ambao ungeleta athari kubwa kwenye uchumi ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha ambazo zisingehimilika hususan kwa wananchi wa kawaida.

Mheshimiwa Spika, Hivyo, Serikali ilitarajia kukusanya takriban shilingi bilioni 500 kutokana na tozo ya miamala ya simu na benki na kuzielekeza katika;

Ujenzi wa madarasa 8,000 nchi nzima ambapo mahitaji ya madarasa bado yanakadiriwa kuwa 17,000;

Kujenga vyuo vya VETA 72 kwenye Wilaya zisizo na vyuo vya ufundi nchini;

Kutekeleza mpango wa elimu bila ada kwa kidato cha tano na sita; na

Kuendelea na ujenzi wa zahanati na vituo vya afya na vifaa tiba katika maeneo ambayo bado hayana huduma hizo. Nawasihi Watanzania wote kuunga mkono juhudi hizi njema za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama yetu, Samia Suluhu Hassan.

Marekebisho ya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2022

Mheshimiwa Spika,
kama unavyofahamu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2021 ilifanya marekebisho kwenye Sheria ya Malipo ya Taifa, Sura ya 437 (The National Payment System Act, Cap 437) kwa kuanzisha tozo ya miamala ya kutuma na kutoa fedha ambapo Kanuni ya Sheria husika (The National Payment System (Electronic Money Transaction Levy Regulations 2021)) ilianzishwa na kuainisha tozo kwenye miamala ya kielektroniki ya kutuma na kutoa fedha kwa njia ya simu. Vilevile, kupitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2022, Kanuni za Malipo ya Taifa (The National Payment System (Electronic Money Transaction Levy) Regulations 2021) zilifanyiwa marekebisho kwa lengo la kuongeza wigowa tozo hiyo kwa miamala yote ya kielektroniki. Marekebisho hayo yalihusisha miamala ifuatayo ya kielektroniki ambayo inalalamikiwa;

Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya Benki ya mtumiaji kwenda mitandao ya simu;

Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya Benki ya mtumiaji kwenda akaunti nyingine ya mtumiaji ndani ya benki husika;

Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki nyingine;

Uhamishaji wa Fedha kimataifa;

Kutoa fedha taslimu kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji au akaunti ya benki kwa mkusanyaji, wakala wa mkusanyaji au mashine ya kuhesabu fedha kielektroniki.

Mheshimiwa Spika, Kuongezwa kwa wigo wa utozaji wa tozo za miamala kumepelekea malalamiko hasi kutoka kwa wadau. Wapo waliodhania gharama zote hizo zimeletwa na Serikali ili hali gharama za kutuma au kutoa fedha zimejumuisha gharama za taasisi husika na nyongeza kidogo ya Serikali. Kwa mfano unapotoa TZS 15,000 ni TZS 2,443, Gharama ya Benki ya Tangu zamani ni TZS 2,200 na tozo ya Serikali yaani gharama mpya ni TZS 243, na kwenye kutuma zaidi ya milioni tatu kielektoniki (T.T) gharama ilikuwa TZS 14,000 ambapo gharama za Mabenki tangu zamani ni TZS 10,000 na tozo ya Serikali ni TZS 4,000.

Mheshimiwa Spika, Kufuatia malalamiko hayo, Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kiliielekeza Serikali kupitia upya tozo za miamala na kuzingatia maoni ya wananchi. Wizara ya Fedha na Mipango kupitia wataalam wake wa Bajeti na wataalam wa Sera wakiwashirikisha wadau wamefanyia kazi maelekezo ya Chama na Maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia upya tozo hizo.

Mheshimiwa Spika, naomba kusisitiza hapa wataalam wa Wizara ya Fedha na Mipango wanaohusika na maswala ya Bajeti na Sera wamefanya mapitio haya wakiwa Ofisini kama Sehemu ya Majukumu yao ya Kila siku tofauti na taarifa zilizozungushwa kuwa kuna tume ya watu 200 imeundwa na inatumia mabilioni ya fedha. Napenda kuwasilisha taarifa kuwa tumefanya mapitio kama ifuatavyo: Kupunguza mzigo wa tozo kwa jamii, Kuchochea matumizi ya miamala kwa njia ya fedha taslimu (cash); Kurahisisha utozaji, na Kuzuia utozaji wa tozo husika mara mbili kwa kuwa utozaji wake kwa sasa unahusisha pande zote mbili yaani mtoaji na mpokeaji.

Marekebisho Yatakayofanyika

Mheshimiwa Spika,
marekebisho yatakayofanyika ni kama ifuatavyo;

Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu (pande zote);

Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja (pande zote);

Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine (pande zote);

Wafanyabiashara (merchants) hawatahusishwa kama ilivyo kwenye kanuni za sasa;

Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000; na

Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50 kufuatana na kundi la miamala. Ikumbukwe kuwa tozo hizo ambapo viwango vya tozo vilishushwa kwa asilimia 30 kutoka kiwango cha juu cha shilingi 10,000 hadi kiwango cha juu cha shilingi 7,000, viwango ambavyo vilianza kutumika tarehe 07 Septemba, 2021. Kadhalika, Mheshimiwa Rais alisisitiza kupunguzwa zaidi tozo ambapo Wizara ya Fedha ilipunguza tozo zaidi kwa kushusha tena kiwango cha juu kutoka 7,000 hadi 4,000.

Mheshimiwa Spika, marekebisho haya yataanza kutumika tarehe 1 Oktoba 2022.

Mheshimiwa Spika, Sambamba na hatua hiyo, Serikali inafuta utaratibu wa kodi ya zuio inayotokana na pango kukusanywa na mpangaji na badala yake jukumu hilo linarejeshwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa utaratibu utakao bainishwa kwenye kanuni. Napenda kusisitiza kuwa kodi ya zuio ya pango siyo ya mpangaji bali inapaswa kulipwa na mpangishaji ambaye ndiye anapokea mapato kutokana na uwekezaji au biashara ya kupangisha. Utaratibu huo umekuwa ukitumika kwa muda mrefu kwenye nyumba za biashara na nyumba zinazopangishwa kwenye makampuni au mashirika yanayofunga ritani za kodi.

HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, mwisho lakini sio kwa umhimu nisisitize mambo mawili:

Ni dhahiri kwamba punguzo hili litapunguza mapato ya Serikali, naelekeza fedha hizi zifidiwe kutokana na kubana matumizi mengineyo ndani ya Serikali ambayo hayataathiri utekelezaji wa majukumu ya Msingi ya mafungu husika. Namwelekeza Mlipaji Mkuu wa Serikali kukaa na Maafisa Masuuli wote kuyaangalia upya mafungu ya matumizi Mengineyo ili miradi ya maendeleo yote isiathirike kwa hatua hii. Tukate kwenye chai, vitafunwa, misafara kwenye safari za ndani na nje kwa maafisa wa Wizara zetu kama Mhe Rais alivyoelekeza, tukate Mafunzo, Semina, Matamasha, Warsha, makundi yanayokwenda kukagua mradi ule ule kwa nyakati tofauti au makundi yanayokwenda eneo lilelile kila mtu na gari lake (Mfano, Wilaya ile ile kila Afisa na gari peke yake, Mkoa ule ule kila Kiongozi na gari pekee yake).

Mheshimiwa Spika,
Naomba kuwasilisha.

Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb.) Waziri wa Fedha na Mipango, Septemba 20, 2022.
Na Dr Steve Nyerere nae anasemaje kuhusu kufutwa kwa tozo kiaina!!??
 
Back
Top Bottom