Mwigulu Nchemba: Tumefuta baadhi ya tozo, nyingine tumepunguza kwa asilimia 10-50
Wangapi wanalipa Kodi. Tozo ndio suluhu Kwa wakwepa Kodi. Ni sawa na Simba kumvizia nyumbu kwenye bwawa la maji. Nchi zingine watu hujisikia fahari kulipa Kodi. Tofauti na watu wa ufipa. Wafanyakazi wanakatwa Kodi lakini utakuta jitu kubwa Zima Lina mihela na majumba Kila mtaa lakini tin number halina

Nchi nyingine wanaona fahari kulipa kodi maana zinatumika vizuri. Hapa unalipa kodi ili viongozi na watumishi waishi maisha ya kifahari.
 
This is Magufurilistic...

"Kwa kuwa pesa hizi zitaipunguzia mapato serikali, Waziri ameelekeza Serikali ianze kubana matumizi yake mfano kwenye vikao, ...
Una uhakika Magufuri alibana matumizi?
 
Serikali sikivu ya Rais Samia Suluhu Hassan ilisikiliza maoni ya wananchi kuusu suala la Tozo na imefanyia kazi maoni ya wananchi kwa kufuta na kupunguza tozo.

Waziri wa fedha Dr Mwiguru Nchemba amesema leo bungeni kwamba hizi ni baadhi ya sehemu zilizofanyiwa kazi;

-Kufuta tozo ya kuhamisha kutoka benk kwenda mitandao ya simu (pande zote).

-Tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja.

-Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benk moja kwenda nyingine.

-Wafanyabiashara (merchats) hawatahusishwa kama ilivyo kwenye kanunu za sasa.

-Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benk na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000.

-Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50 kufuatana na kundi la miamala. ikumbukwe kuwa tozo hizo ambapo viwango vya tozo vilishushwa kwa asilimia 30 kutoka kiwango cha juu cha shilingi 10,000 hadi kiwango cha juu cha shilingi 7,000 viwango ambavyo vilianza kutumika tarehe 7 September 2021.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu alisisitiza kupunguzwa zaidi tozo ambapo wizara ya fedha ilipunguza tozo zaidi kwa kushusha tena kiwango cha juu kutoka 7,000 hadi 4,000.

Rais Samia Suluhu alisema lengo lake ni "KUMUINUA MWANANCHI NA SIO KUMDIDIMIZA" mwenyezi Mungu aendelee kumuongoza
 
KAZI nzuri ya CCM. Imesikia kilio hiki. Tozo sio tatizo lakini shida Ilikuwa ni kiwango Cha tozo.

Hakuna nchi duniani inaweza kuhudumia watu wake bila kulipa Kodi na tozo zinazostahili. Hata kama ni chadema(japo waameishiwa hoja) wakibahatika kupata serikali labda kuanzia miaka ya 2150 watatoza tozo.

Nimpongeze sana bwana nchemba Kwa kusikia kilio hiki na maelekezo ya CCM.
Yaani Kuingiza CCM kwenye hili la kutoa ama kupunguza tozo ni unjingaa kabsaa. Maana kwa mtu mwenye akili ninani aliingiza hizi tozo?

Kwa fikra zangu kwanini umpokenze alieingza wazo la kuumiza wananchi Kwa kivuli cha tozo ili hali badaya kusoma upepo yamemshinda halafu anataka apongezwee?

mnatembelea migari ya kufuru na hamtaki kuiachia ,yaani baada kuacha kutumia magar ya anasa bado mnakimbilia vitu vidgvdg eti semina, warsha nk.

Futliia mbalii mishangingi hyo mnayotembelea, punguza mishshara ya wabunge ya mamilioni, pungza mishahara ya mawaziri kama mtu hataki akalme..Kelele za wananchi ztawanyoosha siku moja.
 
Daah nafkiri watumiaji wa miamala ya simu ni wengi na wa hali ya chini kuliko wanaotumia bank, hivyo basi naona bado msaada haujawafikia hawa ambao wanapenda kuwaita wanyonge ila wamewafariji tu kwamba wasihofu watanyonya kesho
 
-Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benk na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000.
Stupid, unamsamehe mtu kwa kuwa ulikuwa unaniibia? Rubbish. Serikali inawaibia watu halafu mnasema kuwa mmetusamehe kutuibia!
 
Ni jambo jema
Tengeneza tatizo, tatua. Watu wakupigie makofi
Hizi ni kiki za kijinga sana. Hizo tozo wanazokusanya na kuzitumia kwenye anasa zao wameona watanzania tuna hela sana. Sasa hivi siyo mbuga za wanyama, siyo madini n.k ni tozo ndiyo ina jenga nchi. Kila siku CCM wanabuni mbinu mpya ya kuweka tozo.

Hii nchi imekua ya kijinga sana
 
Ni usanii mtupu,

-Wananchi wengi wa chini hawana akaunti Bank, wengi ni watumiaji wa miamala ya simu za mikononi- kwa hiyo ili mwananchi wa daraja la chini aguswe directly ni lazima tozo ya miamala ya simu iliyoletwa na awamu hii iondolewe.

- Daraja la kati wengi ni wafanyakazi, wafanyabiashara wenye maslahi madogo ambao wanatumia ATM cards, kama serikali ina nia ya kuwasaidia iondoe tozo ambazo yenyewe imeziweka awamu hii.
 
KAZI nzuri ya CCM. Imesikia kilio hiki. Tozo sio tatizo lakini shida Ilikuwa ni kiwango Cha tozo.

Hakuna nchi duniani inaweza kuhudumia watu wake bila kulipa Kodi na tozo zinazostahili. Hata kama ni chadema(japo waameishiwa hoja) wakibahatika kupata serikali labda kuanzia miaka ya 2150 watatoza tozo.

Nimpongeze sana bwana nchemba Kwa kusikia kilio hiki na maelekezo ya CCM.
Tengeneza tatizo halafu tatua. Wajinga watakupigia makofi wakiamini unawajali sana. Tuna kizazi cha kijinga sana
 
Sasa hivi tuna mkoloni mweusi. Ukipata 10,000 ya mkoloni mweusi 7,000 na ya kwako 3,000.
Sasa hivi tunakoelekea Tanzania itashika namba 1 kwa nchi ambazo wananchi wake hawana furaha.
Unga kilo 1 = 1,800
Mchele kilo 1 = 2,800

1 GB = 3,000 Internet ni anasa kwa sasa. Nikasema hii serikali ni ya kizalendo, nikaingia TTCL. Nilishika kichwa. Kila siku wanatuhubiria uzalendo.

Uliza vipato vya wananchi wake sasa. Ndiyo utajua kuna viongozi wanajiangalia wenyewe, kiongozi analipwa milion 2, anapewa gari na nyumba ya bure, akienda ofisini WIFI ya TTCL ya bure anafikiri watanzania wote tunaishi kama yeye.

Hata kodi akipanga anakifikiria kama tunaishi kama yeye.
 
Leo tar 20 mpk tar 1oct ni siku 10.
Hizo siku 10 tozo zitakazokusanywa itapigwa abla-kadabla shot-kulia zote ndani mumfuko.
Ndio ianze sheria mpya.
 
Back
Top Bottom