Akizungumza leo bungeni, Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amesema uongezwaji wa wigo wa kukusanya mapato kupitia tozo uliibua malalamiko kwenye jamii, hivyo Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi iliagiza upitiwaji upya wa tozo hizi na kuzingatia maoni ya wananchi.
Marekebisho yafuatayo yamefikiwa-
Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu kwa pande zote.
Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja na kutoka benki moja kwenda benki nyingine.
Kutowahusisha wafanya biashara wadogo (merchants) kama ilivyokuwa kweye kanuni ya sasa.
Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki yaani ATM kwenye miamala yenye thamani ya chini ya tsh 30,000/=
Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10-50 kutokana na makundi ya miamala
Marekebisho haya yataanza kufanya kazi Octoba 1, 2022. Aidha Serikali itafuta utaratibu wa kodi ya zuio ya pango inayotaka kukusanywa na mpangaji, hivyo kwa sasa itapaswa kulipwa na mmiliki wa nyumba na siyo mpangaji.
Kwa kuwa pesa hizi zitaipunguzia mapato serikali, Waziri ameelekeza Serikali ianze kubana matumizi yake mfano kwenye vikao, mafunzo ya semina, warsha, safai za ndani na nje, misafara, kukagua miradi n.k
Wataalamu wa wizara ya fedha na mipango ndiyo wamefanya mapitio haya wakiwa ofisini kwa kuwa ni sehemu ya majukumu yao. Taarifa za kuwa kuna tume iliundwa kutoka nje ya wizara ni uzushi.